in

Mauzo Newcastle: Utata kisheria

Newcastle United

Nyaraka mpya za kisheria zilizotolewa na Bodi ya Ligi Kuu ya England (EPL) zinazua utata mpya ikiwa mpango tata wa kuuza klabu ya Newcastle, na kuacha maswali mengi iwapo mchakato wa dili la mauzo ya klabu hiyo unaweza kuendelea.

Mmiliki wa klabu hiyo – Mike Ashley alifanya mazungumzo na kusema walikuwa katika hitimisho la mauzo ya Newcastle kwa matajiri wa Saudi Arabia kwa kitita cha pauni miliuoni 300, wakiungwa mkono na Mwana Mfalme Mohammed bin Salman anayesimamia kupata asilimia 80 ya hisa klabuni hapo.

Inatambulika kwamba wanasheria wa Bodi ya EPL walikuwa wakipitia nyaraka muhimu na kutazama taarifa zinazodaiwa kuthibitisha uhusiano thabiti kati ya Serikali ya Saudi Arabia na maharamia wa nchini humo ambao kwa muda sasa wamekuwa wakiiba matangazo ya televisheni ya mechi za EPL na kurusha bila haki wala kulipa gharama kwa EPL au England.

Maharamia hao walio chini ya jukwaa la BeoutQ wamekuwa wakirusha mechi hizo nchini Saudia, lakini pia katika eneo pana zaidi la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Mbali na EPL, maharamia hao wamekuwa wakirusha mechi na matukio ya Wimbledon na ‘Six Nations’.

Hatice Cengiz tells Premier League the proposed deal is incompatible with its charter
Hatice Cengiz tells Premier League the proposed deal is incompatible with its charter

Serikali ya Saudia inadaiwa kuwawekea kauzibe wanasheria wa Serikali ya Uingereza walipojaribu kama mara tisa kufungua kesi nchini humo ili kuzuia wizi huo wa matangazo ambao mbali na kurushwa na televisheni, hutiririshwa kwenye mitandao ya jamii – ambapo haki ingetumika, EPL na klabu wangepata kiasi kikubwa cha fedha katika haki za matangazo ya televisheni.

Pamekuwapo mwito kwa EPL kuzuia kuuzwa kwa klabu hiyo kwa watu wanaoihujumu. Ushahidi huo mpya unamaanisha kwamba uamuzi wa kuidhinisha mfuko wa umma wa uwekezaji wa Saudi unaoungwa mkono na serikali ya huko kuichukua Newcastle huenda ukakwama au kuzuiwa kwa muda.

Mfuko huo unahusisha Reuben Brothers na Amanda Staveley – na idhinisho la mauzo ya klabu hiyo lilitarajiwa kukamilishwa ndani ya siku chache tangu nyaraka za kisheria zilipowasilishwa kwenye Bodi ya EPL. Staveney na wenzake wanatarajiwa kununua hisa zilizobaki Newcastle.

Bodi ya EPL sasa itapitia tena kujiridhisha ikiwawa kundi hilo la kampuni hiyo inakidhi vigezo na masharti ya kuuziwa klabu nchini England wakati kuna kigezo kinachosema kwamba uharamia wa kidijiti ni marufuku. Mtihani hapo utakuwa mzito.

Jamaa wanaotarajiwa kuchukua asilimia kubwa ya hisa klabuni Newcastle wenyewe wamekana kuwa na uhusiano wowote na uharamia wa BeoutQ. Kimsingi, kanuni za Bodi ya EPL zinasema kwamba waombaji wa ununuzi hawatakiwi, kwa namna yoyote kutoa taarifa zisizo sahihi, za uongo au zinazopotosha.

Saudia ilipata kudai awali kwamba BeoutQ ina asili yake Cuba na Columbia. Hata hivyo, Januari mwaka huu, taifa hilo la Ghuba ya Uajemi lilitajwa kwenye ripoti ya Kamisheni ya Ulaya kwa kushindwa kubomoa na kuua jukwaa hilo la kiharamia.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) na Bodi ya Ligi Kuu ya Hispania – La Liga ni kati ya vyombo vya michezo vilivyokwisha jaribu kuchukua hatua za kisheria kwa ajili ya kulifunga jukwaa hilo la kiharamia nchini Saudia, lakini kampuni tisa za uwakili za huko Saudia zimekataa kuwafanyia kazi hiyo.

Wakati hayo yakiendelea, Saudi Arabia inabaki kwenye orodha ya kipaumbele inayotazamwa na Marekani – kwamba ni moja ya masoko yenye sifa mbaya kutokana na bidhaa bandia na uharamia.

Hivi karibuni, Mtendaji Mkuu wa BeIN, Yousef al-Obaidly, aliiandikia barua Bodi ya EPL na klabu zake kuelezea juu ya hatari iliyopo kwa kuruhusu Wasaudia kuchukua klabu hiyo, ikitiliwa maanani kile alichokieleza kwamba ni ushiriki moja kwa moja wa Saudia kwa vitendo haramu vya BeoutQ juu ya maslahi kwenye EPL.

Rais wa La Liga, Javuer Tebas, aliitaka Bodi ya EPL kufikiria jinsi vitendo vya kiharamia vya BeoutQ vinavyoharibu picha nzuri ya ligi hiyo, kabla ya kuamua juu ya mauzo ya Newcastle kwa Wasaudia.

Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu – Amnesty International pia limetaka ligi hiyo maarufu zaidi duniani kufikiria kuzuia mauzo kwa Wasaudia, likisema kwamba mfuko unaotaka kuinunua unasimamiwa na Mwana Mfalme Salman ambaye anahusika na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Timu ya Arsenal kwenye mchezo wa kirafiki

Mechi zioneshwe bure

Tanzania Sports

Who will win the VPL