in

Mastaa wanaokosa kombe la dunia 2022

Milan Škriniar

Hekaheka za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la dunia ziliendelea wiki katika viwanja mbalimbali. kutoka bara la Afrika hadi Ulaya, Amerika kusini hadi Amerika kaskazini na Asia. Kote huko mataifa yalikuwa kwenye mbio za kuwania kufuzu fainali hizo zinazotarajiwa kufanyika nchini Qatar ifikapo Desemba 2022.

Hadi sasa mataifa yaliyofanikiwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 ni wenyeji Qatar,Ujerumani,Denmark,Brazil,Ubelgiji, Ufaransa, Croatia, Hispania, Serbia, Uswisi, England,Uholanzi na Argentina. Baadhi ya timu zitaongezeka baada ya mechi za mtoano katika mabara yote. 

TANZANIASPORTS inakuletea uchambuzi wa mastaa ambao wamekuwa wakitikisa katika soka barani Ulaya, Afrika,Amerika na Asia lakini watakosekana katika michuano ya Kombe la dunia kwa sababu nchi zao hazikifanikiwa kufuzu.

ERLING HALLAND 

Huyu ni mshambuliaji mahiri anayetamba katika ufungaji wa mabao akiwa anakipiga katika klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki Bundesliga nchini Ujerumani. Halland ana thamani kubwa katika soko la mauzo ya wachezaji na anawindwa na vigogo kama vile Manchester Uniterd,Mancherster City,Liverpool,Real Madrid,Bayern Munich na Barcelona, lakini nchi yake Norway imeshindwa kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2022. Norway walishindwa kutamba mbele ya wababe wa soka Ulaya, Uholanzi.

FRANCK KESSIE

Ni miongoni mwa wacheaji wanaowakilisha vema bara la Afrika katika soka duniani akiwa anakipiga kwa kigogo wa soka Seire A, AC Milan. Lakini Kessie hataonekana katika michuano ya Kombe la dunia mwaka 2022 baada ya nchi yake Ivory Coast kushindwa kufuzu. Ivory Coast walikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka Cameroon.

PIERRE EMERIK AUBAMEYANG

Ni nahodha wa Gabon na klabu ya Arsenal. Ni jina kubwa katika kandanda barani Ulaya na Afrika, ambalo litakuwa miongoni mwa yatakayokosekana kwenye fainali za Kombe la dunia mwaka 2022 huko Qatar.

EDIN DZEKO

Nyota mwingine maarufu duniani. Ni mshambuliaji mwenye mabao ya kutosha katika klabu ya Lazio inayoshiriki Ligi Kuu Italia. Dzeko atakosekana kwenye fainali za Kombe la dunia mwaka 2022 baada ya nchi yake Bosnia and Herzegovina kushindwa kufuzu.

JAN OBLAK

Ni nyanda maarufu sana La Liga na barani Ulaya. Lakini jina hilo litakuwa miongoni mwa yatakayokosekana katika Fainali za Kombe la dunia mwakani huko Qatar baada ya nchi yake Slovenia kushindwa kufuzu kwa michuano hiyo. 

NABY KEITA

Ni staa wa Liverpool ambaye anatesa katika dimba la katikati. Ni staa wa kutumainiwa wa taifa la Guinea pia. Lakini katika fainali za Kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar atakosekana kutokana na nchi yake kushindwa kufuzu kwa michuano hiyo. 

MILAN SKRINIAR

Ni nyota kutoka Slovakia ambaye amejikuta akitupwa nje ya fainali za Kombe la dunia mwaka 2022 huko Qatar. Mashabiki watakosa umahiri wake uwanjani, naye atabaki nyumbani kutazama michuano hiyo kwa njia ya televisheni.

GARETH BALE

Nyota huyu wa Real Madrid ameshindwa kuiwezesha nchi yake ya Wales kufuzu fainali za Kombe la dunia mwaka 2022. Bale ndiye nahodha wan chi hiyo, na amekuwa alama ya mafanikio. Licha ya kufundishw ana staa wao wa zamani Ryan Giggs imeshindwa kufurukuta. 

LUIS SUAREZ na EDINSON CAVANI

Washambuliaji pacha na mahiri wa muda mrefu katika timu ya taifa ya Uruguay ni majina yatakayokosekana katika fainali za Kombe la dunia mwaka 2022. Luis Suarez anakipiga katika klabu ya Atletico Madrid na Edinson Cavani anacheza katika klabu ya Manchester United. Wote wawili wameshindwa kuiokoa Uruaguay ambayo imechapwa mechi nne mfululizo na kupoteza nafasi ya kucheza mchezo wa mtoano kufuzu fainali hizo. Kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Bolivia kilizima ndoto za kufuzu fainali hizo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Bila fedha Ligi zetu zitakuwa nyanya

Pablo Franco

Mavituzi ya Pablo Franco bado Simba