in , , , ,

Manchester City nje Ulaya

Manchester City wametolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp na kuaga kwa jumla ya mabao 1-4.

Vijana hao wa Manuel Pellegrini walishindwa kukabiliana na muziki wa Barcelona, ambapo Lionel Messi alifunga dakika ya 67 kabla ya Pablo Zabaleta kutolewa nje kwa kadi nyekudnu dakika 12 kabla ya mchezo kumalizika.

Zabaleta alikuwa akimlalamikia mwamuzi kwa kutojali pale Gerard Pique alipoonekana kumfanyia faulo mbaya Edin Dzeko. Tayari Zabaleta alikuwa na kadi ya njano, hivyo akatolewa nje.

Kadi hiyo nyekundu ni ya 26 kwa timu pinzani wa Barca nay a 10 kwa timu ya England, hivyo kujenga nadharia kwamba kuna namna ya kuwapendelea Wahispania hao, japokuwa mara nyingi marefa huweza kujitetea kwa aina ya makosa ya wachezaji.

City, hata hivyo, walipambana na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 89 kupitia kwa nahodha wao, Vincent Kompany likionekana wazi lingekuwa la kufutia machozi tu kwani bado wangehitaji mengine matatu ili kusawazisha mambo. Mbaya zaidi, Dani Alves alifunga bao la pili katika muda wa majeruhi na kuwarejesha City nyumbani.

City watajilaumu kwa jinsi walivyocheza pasipo kujituma katika mechi ya kwanza nyumbani Etihad na pia kwenye mechi ya usiku huo wa Jumatano walikosa nafasi ya mapema ya kupata bao kupitia kwa Samir Nasri ambaye shuti lake liliokolewa na kipa Victor Valdes.

City waliokuwa wamedhamiria kutwaa mataji manne sasa wamebakiwa na uwezekano wa kutwaa mawili ya Ligi Kuu ya England na Kombe la Ligi.

Hata hivyo wana hofu juu ya mchezaji wao, Sergio Aguero aliyeshindwa kuingia kipindi cha pili kwa maumivu na wanasubiri vipimo kujua kama ataweza kucheza mechi za karibuni.

England imebakisha timu mbili kwenye mashindano hayo, Chelsea watakaorudiana na Galatasaray Jumanne ijayo jijini London na Manchester United watakaorudiana na Olympiakos.

United walifungwa kwenye mechi ya kwanza. Arsenal walitolewa na Bayern Munich kwenye michuano hiyo. Katika mechi ya kwanza nchini Uturuki walitoka sare.

 Katika mechi nyingine ya UCL Jumatano hii, Paris Saint Germain waliwatoa Bayer Leverkusen kwa kuwatandika jumla ya mabao 6-1 katika mechi mbili walizocheza.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal pigo mara mbili

Ronaldo mwanasoka tajiri zaidi