in ,

Man U kileleni, Arsenal safi

 

*Man City waoga kichapo, Chelsea wanusurika

 

Manchester United wamekalia usukani wa Ligi Kuu ya England (EPL) kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja, baada ya kuwachapa Sunderland 3-0.

Man U wameendeleza mserereko wa kushinda mechi za EPL ambapo nahodha wao Wayne Rooney alifufuka na kufunga bao sambamba na Memphis Depay na Juan Mata, huku kocha Louis van Gaal akisema anajihisi furaha sana kukalia uongozi wa ligi.

Kwa ushindi huo, Man U wamefikisha pointi 16, huku wakizidi kuwakandamizia Sunderland katika mkia wa ligi, kocha Dick Advocaat akibaki kujiuliza cha kufanya baada ya  kuambulia pointi mbili tu katika mizunguko saba.

Arsenal nao walifanya vyema kwa kuvunja rekodi ya Leicester ambao walikuwa hawajapata kufungwa msimu huu, na Arsenal walifanya hivyo kwa staili ya aina yake, wakiwashindilia mabao 5-2.

Matatu kati ya hayo, yaani hat trick, yalifungwa na mchezaji wa Chile aliyekuwa akisuasua msimu huu, Alexis Sanchez huku yale mengine mawili yakifungwa na Theo Walcott aliyeanza kupewa fursa ya ushambuliaji wa kati na Olivier Giroud aliyeingia baadaye kipindi cha pili, baada ya Arsene Wenger kusema yeye si lazima awe chaguo la kwanza kwenye ushambuliaji wa kati.

Manuel Pellegrini aliugulia jana baada ya Manchester City kuambulia kipigo cha mbwa mwizi, tena kutoka kwa timu ambayo haikutarajiwa kuwa na uwezo huo – Tottenham Hotspur waliowapiga mabao 4-1.

Advertisement
Advertisement

City kwa kupoteza mechi ya pili mfululizo wameshushwa hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 15, nafasi ya tatu ikishikiliwa na West Ham wenye pointi 13 sawa na Arsenal lakini West Ham wana uwiano mzuri zaidi wa mabao.

Kwingineko, Chelsea walinusurika kufagiliwa na mafuriko ya Newcastle baada ya kuchomoa mabao mawili waliyokuwa wameshafungwa, wakielekea kulala zikiwa zimebaki dakika 11, wakafanikiwa kuokoa jahazi.

Kwa sare hiyo, vijana wa Jose Mourinho wamebaki katika nafasi ya 15, wakionekana kutokuwa na makali kwenye ushambuliaji wasipokuwa na mshambuliaji wa kati wa Hispania, Diego Costa aliyefungiwa kucheza mechi tatu baada ya kuonesha mchezo mbaya kwenye mechi dhidi ya Arsenal.

Newcastle kwa upande wao, sare hiyo imewafikishia pointi ya tatu tu, wakiwa mkiani juu ya Sunderland, lakini wanaelekea kufufuka na kocha wao Steve McLaren aliwapongeza kwa kuonesha nia na kujiamini, lakini haikuwa bahati yao kushinda.

Katika mechi nyingine za Jumamosi hii, Liverpool walipambana hadi kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Aston Villa, hivyo kumpunguzia shinikizo kocha Brendan Rodgers. Southampton waliwanyuka Swansea 3-1, Stoke wakawazidi nguvu Bournemouth 2-1 na West Ham wakaambulia sare ya 2-2 kwa Norwich. Jumapili hii Watford wanacheza na Crystal Palace.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

YANGA WAWATWANGA WATANI

Tanzania Sports

Platini naye kikaangoni FIFA