in , , ,

Man City mdomoni mwa PSG

Manchester City wamepangwa kuchuana na mabingwa wa Ufaransa, Paris
Saint-Germain (PSG) katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
(UCL).

City, pekee waliobaki kwa upande wa England katika mashindano ya Ulaya
wataonekana kufurahi kutopangwa dhidi ya ama Bayern Munich wa Pep
Guardiola au Barcelona wanaotamba na mapacha watatu – Lionel Messi,
Neymar na Luis Suarez kwenye mashambulizi.

Ni watatu hao waliosababisha kilio Arsenal kwa kuwatoa kwa jumla ya
mabao 5-1, wakiwafunga Emirates na kwao Nou Camp, siku chache baada ya
Arsenal kutolewa na Watford katika robo fainali ya Kombe la FA.

Barca watakabiliana na Wahispania wenzao, Atletico Madrid wanasumbua
pia kwenye La Liga wakifundishwa na Diego Simeone, Bayern wakipangwa
na Benfica huku Real Madrid wanaosaka sana kombe hilo wakiwa uso kwa
uso na Wolfsburg.

PSG wametwaa ubingwa wa Ufaransa miezi miwili kabla ya Ligue 1
kumalizika na watawakaribisha vijana wa Manuel Pellegrini kwanza
jijini Paris kwa mechi ya mkondo wa kwanza Aprili 6 na marudiano na
Aprili 12 dimbani Etihad, Manchester.

Timu mbili hizo zimepata kukutana mara moja tu, na mechi yao
ilifanyika Manchester, ikiwa ni ya Kombe la Uefa, ikamalizika kwa
suluhu. Klabu hizo hazikuwa zikifahamika sana enzi hizo, City wakiwa
adogo kabla Sheikh Mansou hajamwaga fedha za mafta na PSG walikuwa
miaka mitatu kabla ya kutwaliwa na wamiliki wao wa Qatar.

PSG wanaofundishwa na Mfaransa Laurent Blanc, tangu hapo wametokea
kuitawala soka ya Ufaransa kwa kutwaa ubingwa mara nne mfululizo. Hata
hivyo, kama ilivyo kwa City, matajiri hao wa Paris hawajaweza kung’ara
sana kwenye UCL, wakiishia katika robo fainali misimi mitatu
iliyopita.

City katika mechi dhidi ya PSG enzi hizo ilikuwa na wachezaji kama
Benjani, Elano and a Daniel Sturridge akiwa mdogo, japokuwa nyota wa
sasa pia, Joe Hart, Pablo Zabaleta na Vincent Kompany walicheza.

Pellegrini ambaye nafasi yake itachukuliwa na Guardiola kiangazi
kijacho, ameeleza kwamba ni faraja kuanzia ugenini na kumalizia
nyumbani. Barcelona watakuwa wanajaribu kuwa timu ya kwanza kutwaa
mara mbili mfululizo ubingwa wa Ulaya.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Neymar hatiani

Tanzania Sports

Leicester kama wanamsukuma mlevi