in , , ,

Mambo hadharani Brazil

Ilikuwa miaka, miezi, wiki, siku na sasa ni saa tu kwa mambo kuwa hadharani nchini Brazil katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia.

Katika taifa hilo la wachawi wa soka na samba, Brazil wanaanza kwa kucheza na Croatia usiku wa Alhamisi hii.

Brazil wanatarajiwa kuingiza dimbani kikosi kile kile kilichowanyoa Wahispania kwenye fainali ya michezo ya Kombe la Mabara.

Kiungo mchezeshaji, Oscar, anatarajiwa kuanza licha ya kutokuwa katika kiwango cha hali ya juu huku vyombo vya habari vikimpigia debe mchezaji mwenzake wa Chelsea, Willian.

Croatia wanaanza bila mpachika mabao, Mario Mandzukic anayetumikia adhabu ya kukosa mechi moja, hivyo Nikica Jelavic au Eduardo watashika nafasi yake.

Sime Vrsaljko atacheza katika beki ya kushoto badala ya majeruhi Danijel Pranjic

Sherehe za ufunguzi zinakuja baada ya mechi 820 za kufuzu zilizoshirikisha timu 202 kutoka mabara yote na kuchujwa hadi kufikia timu 32 tu zilizoingia kwenye fainali hizi.

Hizi ni fainali ambazo ni za gharama kubwa zaidi katika historia ya Kombe la Dunia na baadhi ya wananchi wa Brazil waliandamana kupinga matumizi hayo, wakidai kwamba bora fedha zingeelekezwa kuboresha maisha yao, jambo ambalo limebezwa na wananchi wengi pamoja na viongozi wao.

Mchezo wa usiku huu unakuja wakati ambapo historia ikionesha hakuna nchi mwenyeji iliyopata kupoteza mechi ya ufunguzi, hivyo shinikizo lipo kwa Brazil.

Kocha wa Vroatia, Niko Kovac amesema kwa kuwa wakweli ni kwamba Brazil wanapewa nafasi ya kushinda mechi hiyo kutokana na uenyeji lakini pia kwa uwezo wa wachezaji wake wenye vipaji.

“Tumekuja kwa ajili ya kucheza, kushindana na tutaonesha uwezo wetu wote uwanjani. Wachezaji wana ari kubwa kwa mechi hii inayosubiriwa na mamilioni ya watu kote duniani. Wataonesha kiwango cha hali ya juu,” anasema Kovac.

Mechi ya mwisho iliyokutanisha timu hizi ilifanyika 2006 ambapo Brazil walishinda 1-0 kutokana na bao la Kaka jijini Berlin, Ujerumani.

Agosti 2005 timu hizo zilitoka sare 1-1 katika mashindano mengine, na nchi hizi hazijakutana tena.

Brazil wameshinda mechi zao tisa zilizopita wakifunga mabao 30 na kufungwa mawili tu, hivyo kuonesha jinsi walivyo na uwezo mkubwa. Wamefungwa mechi moja tu kati ya 21 zilizopita.

Brazil ni nchi pekee ambayo haijakosa hata fainali moja ya Kombe la Dunia tangu kuanzishwa kwake.

Katika mashindano hayo wameshinda mechi 67, wakafunga mabao 210 lakini ni wachezaji sita tu katika kikosi cha sasa ambao wamepata kushiriki michuano hii, ambapo wanafundishwa na Luiz Felipe Scolari ‘Big Phil’ ambaye ni Mbrazili.

Tangu Kovac awe kocha wa Croatia, hawajafungwa katika emchi tano ambapo wameshinda tatu na kwenda sare mbili.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Carlos Vela anarudi Arsenal

Man United yawakataa Cavani, Fabregas