in , , ,

MAENEO YATAKAYOAMUA MECHI YA FAINALI KATI YA REAL MADRID NA JUVENTUS

Zinedine Zidane na Massimiliano Allegri wote kwa pamoja wanaingia
fainali yao ya pili ya ligi ya mabingwa barani ulaya ndani ya miaka 3.

Tofauti inayokuja kati yao ni moja, Massimiliano Allegri alipoteza
fainali iliyopita ya mwaka 2015 dhidi ya Barcelona wakati Zinedine
Zidane alifanikiwa kuchua fainali yake ya mwisho msimu uliopita.

Yafuatayo ni baadhi ya maeneo ambayo yataamua mechi ya leo.

Rekondi ya mwaka AC Milan ina nafasi gani katika mechi ya leo ?

Tukumbuke Ac Milan ndiyo timu pekee iliyobeba kikombe hiki mara mbili
mfululizo ikifanya hivo mwaka 1989 na mwaka 1990.

Hii itaifanya Real Madrid kuingia uwanjani wakitaka kufikia rekodi ya Ac Milan .

Hii inaweza ikawa na faida na hasara.

Faida ni kuwa wachezaji wa Real Madrid wataingia na Morali wa kupigana
ili wawe moja ya watu ndani ya historia hii.

Hasara moja wapo hapa ni kuwa hii inaweza kuwafanya waingie kwa
kukamia, kukamia huku kutawafanya wao kukosa umakini na wakikosa
umakini utulivu ndani yao huondoka na utulivu ukiondoka kutawapa
nafasi kubwa ya wao kufanya makosa mengi binafsi kitu ambacho kinaweza
kuwanufaisha Juventus kama wakitumia hayo makosa.

Ukuta imara dhidi ya Safu kali ya ushambuliaji.

Katika mechi 12 zilizopita za hizi timu, Juventus imefungwa goli tatu
tu wakati Real Madrid ikifunga kila goli kwenye mechi hizo 12.

Hii inaonesha Juventus ina safu imara ya ulinzi ambayo haina wastani
wa kufungwa hata goli moja kwenye mechi 12 zilizopita na hii inatoa
tafasri kuwa Real Madrid watakuwa na kazi ngumu kwao kupata goli.
Lakini kazi haiwezi kuwa rahisi kwa beki za Juventus kwa sababu ya
ukali wa safu ya ushambuliaji ya Real Madrid.

Isco au Bale ? Dani alves au Cuadrado ?

Bale amekuwa nje tangia mwezi wa nne anarudi tena baada ya kuwa
majeruhi ila anarudi akikuta Isco akiwa katika hali nzuri kwani katika
mechi nane zilizopita amefanikiwa kufunga goli 5 na hii ni kutokana na
yeye kucheza katika eneo huru kitu ambacho kinamsaidia sana yeye
kuonesha ubora alionao.

Wote wawili wana umuhimu katika maeneo tofauti.

Kwa mfano uwepo wa Isco katika eneo huru na kumfanya acheze kama
mchezaji huru kutawapa shida wachezaji wa Juventus kumkapa.

Pia uwepo wa Bale unafaida sehemu moja, yeye siyo mtu aliyezoea
kucheza eneo huru. Ni mtu ambaye amekuwa akicheza katika eneo la
pembeni hii itawafanya Wingbacks wa Juventus hasa hasa Dani Alves
kupanda kwa tahadhari kuhofia uwepo wa Bale hivo kupunguza uwezekano
wa Juventus kushambulia sana.

Ukimtaja Dani Alves unamtaja mchezaji ambaye katika mechi tatu
zilizopita za ƙligi ya mabingwa katoka msaada wa magoli 2 na kufunga
goli 1 kitu ambacho kinatia ugumu pia ni nani anafaa kuanza kama
Wingback katika mechi ya leo katika eneo la kulia kati ya Cuadrado na
Dani Alves ?

ƳUwepo wa Dani Alves utamlazimu Massimiliano Allegri atumie mabeki 4
na hii itakuwa na faida nzuri kwao kwani Dani Alves ni mzuri kuleta
uwiano wa kushambulia na kuzuia kuliko Cuadrado.

Kuwa na medali ya ligi ya mabingwa kwa Dani Alves na kutokuwa na
Medali ya ligi ya mabingwa kwa Buffon kuna nafasi gani katika mechi ya
leo ?

Buffon ana miaka 39 mpaka sasa na ameshacheza mechi nyingi za
ushindani , mwaka 2015 alifanikiwa kuingia fainali dhidi ya Barcelona.

Wakati huo Dani Alves alikuwa mchezaji wa Barcelona na Barcelona
walifanikiwa kuchukua ubingwa .

Ni tukio lililokuwa ƙlimebeba furaha kwa Dani Alves na huzuni kwa
Buffon ambaye ndiyo medali pekee ambayo hana na maisha yake ya soka
yanahesabika kwani ameshatangaza mara baada ya kombe ƙla dunia la
mwaka 2018 atastaafu kucheza mpira.

Kwa hiyo hii itakuwa nafasi kubwa kwake kupata hii medali na atakuwa
kama chachu ya kuwafanya wachezaji wa Juventus wapigane zaidi huku
Dani Alves akichagiza utamu wa kushinda kombe hili.

Pjanic na Dyabala.

Hawa ndiyo ambao hufanya Juventus iwe hai.

Pjanic amekuwa mzuri sana kuleta uwiano mzuri wa eneo ƙla kiungo cha
kuzuia na eneo la kiungo cha kushambulia, wakati Dyabala amekuwa mzuri
sana katika kuleta uwiano wa eneo la kiungo cha ushambuliaji na eneo
la ushambuliaji la Juventus.

Ubunifu wa mbele umekuwa ukitoka kwa Dyabala na kumfanya Higuain
kuwa na kazi kubwa ya kufunga goli tu.

Ronaldo ndiyo nafasi pekee ya kujihakikishia Ballon D’or ?

Hapana shaka ushindi wa leo wa Real Madrid na kiwango kizuri cha
Ronaldo leo kitampa nafasi kubwa ya yeye kubeba tuzo ya Ballon D’or.

Hii itamfanya apigane kufunga leo ili kuipa ubingwa timu yake na
kumpindua Messi kwenye kinyang’anyiro cha mfungaji bora wa UCL.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Wenger: Arsenal ubingwa tu

Tanzania Sports

SHIKENI KALAMU YENYE MACHO, MASIKIO NA AKILI YA KISHERIA.