in , , ,

LVG: De Gea ni tatizo

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kwamba kipa wake namba moja, David De Gea ni tatizo katika klabu hiyo.

Ametoa kauli hiyo baada ya kipa huyo anayetaka kuhamia Real Madrid kuruhusu mabao mawili kwenye mechi dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG).

Van Gaal anasema kwamba ameona tatizo katika mikono ya kipa huyo raia wa Hispania baada ya kuonesha kiwango duni kwenye mechi, ambapop PSG walishinda 2-0 kwenye dimba la Soldier Field barani Amerika.

LVG alimtoa De Gea baada ya dakika 45 za kwanza, ambapo Madrid wameanza upya mchakato wa kutaka kumchukua, baada ya kumzuia beki wao wa kati, Sergio Ramos kuhamia Man United waliokuwa wakimtaka kwa udi na uvumba.

De Gea amecheza dakika 107 tu katika mechi za maandalizi ya msimu mpya, ambapo LVG anasema hana uhakika iwapo atabaki Old Trafford na tayari wamemsajili kipa Sergio Romero kutoka Argentina.

De Gea ‘alipelekwa marikiti’ wakati PSG walipofunga bao la kwanza, huku walinzi wake, Luke Shaw na Phil Jones wakihangaika bila mafanikio kulinda lango.

Wauaji wa United walikuwa Blaise Matuidi na Zlatan Ibrahimovic waliotumia makosa ya ngome na kipa wa United kucheka na nyavu.

Kocha Van Gaal amesema kwa hali ilivyo ana kazi kubwa ya kufanya akisema kwamba hali si shwari kwa De Gea, akisema kwamba suala la habari za yeye kuhusishwa na Real Madrid nalo linaongeza matatizo.

“Tunataka masuala haya yamalizike. Tupo kwenye hali ambayo si nzuri kwa David De Gea, kwetu wala kwa klabu (Real Madrid) ambayo huenda anataka kwenda. Siwezi kusema hakuwa na kiwango kwenye mechi hii, ni kwamba alifanya makosa tu.

“Kila mtu hufanya makosa lakini inapokuwa ni kipa basi kosa hilo mara nyingi husababisha mfungwe bao na hiyo ndiyo tofauti na wachezaji wa ndani,” anasema.

Katika ziara ya kabla ya msimu, ni kipa wao mdogo na wa akiba, Sam Johnstone aliyecheza muda mwingi zaidi, lakini anatarajiwa kupelekwa Preston kwa mkopo baada ya kurejea nyumbani.

LVG pia alipoulizwa juu ya winga aliyevunja rekodi ya usajili England, Angel Di Maria aliko, alidai kwamba hajui kabisa yuko wapo raia huyo wa Argentina.

Di Maria amekuwa akihusishwa na kujiunga na PSG na hakuambatana na United kwenye ziara hiyo ya Amerika. Awali, Van Gaal alidai kwamba hajui kwa nini Di Maria hakuwa kwenye ndege na wachezaji wenzake wakati wa safari hiyo

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Platini kuwa bosi wa Fifa?

Stopilla Sunzu aenda Lille