in , , ,

Liverpool wawazuia Arsenal

*Man U nao wakwama kwa Villa

Wakati Liverpool wamepigana hadi dakika ya mwisho ya nyongeza na kufanikiwa kuepuka kichapo cha nane katika Ligi Kuu ya England (EPL), Manchester United wameshindwa kuendelea wimbi la ushindi.
Arsenal walikuwa na kiwango kidogo zaidi cha umiliki wa mpira (36.5%) msimu huu walipokuwa wageni wa Liverpool kule Anfield, wakiwa pia na kumbukumbu mbaya ya kuchapwa 5-1 kwenye mechi ya msimu uliopita.

Liverpool walipania kuondokana na mwenendo mbaya tangu mwanzo, ambapo kocha Brendan Rodgers na nahodha Steven Gerrard walikuwa wakisisitiza kabla ya mechi kwamba lazima wacheze kama wanaume, hasa baada ya kutandikwa 3-0 na Manchester United mechi iliyotangulia.

_79879132_liv_lineup(1)

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Wafaransa, beki Mathieu Debuchy na mshambuliaji wa kati, Olivier Giroud wakati ya Liver yalifungwa na Coutinho na Martin Skirtel ambaye kabla aliumia kichwa akipogongana na Giroud na kutibiwa kwa muda mrefu.

Fabio Borini wa Liverpool alilambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu kwa mchezo mbaya dhidi ya Santiago Cazorla kwa kurusha daluga kifuani pake kiasi cha kuchana jezi na kumsababishia mchubuko.

Katika mechi nyingine ya ushindani wa jadi Jumapili hii, Sunderland walifanikiwa kuwafunga Newcastle 1-0 kupitia kwa Adam Johnson katika dakika ya 90 na kuwafanya wawe hawajapata kupoteza mechi tano dhidi ya jamaa zao hao.

_79879131_arsenal'sstartingxivsliverpool

Jumamosi Man United walisimamishwa na Aston Villa kwa kwenda sare ya 1-1, mabao yakifungwa na Christian Benteke na Radamel Falcao akawasawazishia vijana wa Louis van Gaal aliyesema sare hiyo imetibua safari yao kwenda juu ya msimamo wa ligi.

Hull walilala nyumbani 0-1 kwa Swansea, QPR pia wakalambwa 3-2 na West Bromwich Albion, Southampton wakafufuka kwa kuwapiga Everton 3-0, Tottenham Hotspur wakawashindwa Burnley 2-1 wakati West Ham waliwatandika Leicester 2-0. Chelsea ni wageni wa Stoke Jumatatu hii.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

ARSENE WENGER AZUNGUMZIA UGUMU WA LIGI YA ENGLAND

Chelsea wawanyuka Stoke