HAKIKA msimu ujao utakuwa na kukata na shoka. Kila timu inasajili nyota wa kuongeza nguvu huku wengine wakitupiwa virago wakiwemo Nyota wa Liverpool.
Kabla ya Liverpool imethibitisha kuwatimua mastaa ambao hawatakuwa sehemu ya timu msimu wa 2023/2024, huku ukionesha wazi viwango vyao vimeshuka pamoja na hasira za kufanya vibaya kwa klabu hiyo msimu ulioisha ni Sababu zinazowaondoa mastaa hao.
Liverpool wamemtangaza kuondoka kwa wachezaji 11 katika kikosi chao cha kwanza wakiwa wachezaji huru. Ni Kama vile Liverpool wametimua Nyota hao kwani wangeweza kuwaongezea mikataba ya kuendelea kukipiga katika dimba la Anfield.
Wachezaji walioondolewa ni pamoja na kiungo mkongwe, mshambuliaji wa Brazil na nyota wa zamani wa Arsenal. Uamuzi wa kuwatupia virago wachezaji hao ni kukabiliana na Sera mpya ya usajili ambayo inalenga kujenga timu mpya Liverpool na ambayo itakuwa na mafanikio makubwa kama ilivyokuwa miaka mitano iliyopita.
Majina manne makubwa ya Nyota wanaoondoka ni pamoja na mkongwe wa England.
Jurgen Klopp inaonekana amepania kuunda timu mpya baada ha kumaliza msimu wakiwa nafasi ya tano na msimu ujao watakosa kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hasira za kukosa kushiriki UEFA msimu ujao zimeleta matunda baada ha kukamilika dili la usajili wa kiungo mshambuliaji Alexis Mac Allister ambaye anajiunga Liverpool akitokea Brighton kwa ada ya pauni Milioni 35.
Kundi la wachezaji wanaoondoka ni wale ambao waliaminika mbele ya Klopp na kuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa UEFA mwaka 2019, lakini sasa wanalazimika kuondoka klabuni kupisha mwelekeo mpya.
JAMES MILNER anaondoka klabuni hapo akiwa ni kiungo aliyecheza mechi 857 katika maisha yake ya soka
ROBERTO FIRMINO
Ni nyota mwingine aliyeng’ara Liverpool yangu alipojiunga akitokea klabu ya Hoffenheim ya Ujerumani mnamo mwaka 2015. Akiwa Liverpool, Firmino ametwaa mataji 7.
ORODHA KAMILI
Roberto Firmino, Naby Keita, James Milner, Roberto Firmir Naby Keita, Alex Oxlade-Chamberlain.
Nyota wengine kutoka Akademi yao ambao wanaaondoka ni Jack Bearne, Liam Hughes, Charlie Hayes-Green, Oscar Kelly, Fidel O’Rourke, Oludare Olunfunwa, Iwan Roberts.
Reply to allReplyForward |