in , , ,

Liverpool wa Klopp hoi

Georginio Wijnaldum

Liverpool wanatakiwa kujipanga upya kama kweli wanataka kupata nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England (EPL).
Walianza chini ya kocha mpya kwa kusotea sare kisha kufungwa halafu wakaonesha mwenendo mzuri kiasi cha kuwafunga hata waliokuwa vinara wa ligi – Manchester City.

Lakini Jumapili hii wamechezea kichapo cha 2-0 kutoka kwa Newcastle walio chini karibu na eneo la kushuka daraja.
Newcastle wanaofundishwa na Steve McClaren walishangaza kufufukia kwa Liverpool, na hii ni faraja kubwa kwa kocha huyo ambaye tayari pamekuwapo mjadala juu ya kumwondosha au la wakati ni msimu wake wa kwanza.

Georginio Wijnaldum alichochea ushindi huo wa tatu msimu huu kwneye ligi na sasa wamepanda hadi nafasi ya 18 baada ya shuti la Wijnaldum kumparaza mlinzi Martin Skrtel kwenye goti na kutinga wavuni.

Mdachi huyo aliendelea vyema na mchezo na kuiwapatia Newcastle bao la pili katika dakika za majeruhi. Liverpool wapo nafasi ya saba wakiwa na pointi 23 sawa na West Ham walio ya sita huku vinara Leicester wakiwa nazo 32 baada ya wote kucheza mechi 15.
Liver wamshinda mechi saba kati ya nane zilizopita za EPL, lakini Jumapili hii walionekana dhahiri kuwa dhaifu.

James Milner: ‘ Hii club, imezoea kushinda mataji, hatuwezi kuendelea kuwa wasindikizaji tu, ni lazima tubadilike...
James Milner: ‘ Hii club, imezoea kushinda mataji, hatuwezi kuendelea kuwa wasindikizaji tu, ni lazima tubadilike…

Hata hivyo, walinyimwa bao lililofungwa na Alberto Moreno, ikionekana kwamba mwamuzi msaidizi alikosea katika uamuzi wake akidai alikuwa ameotea. Klopp sasa amefungwa mara mbili katika mechi 12.

Vijana wake walifanikisha kulenga mashuti mawili tu golini, tena la kwanza likiwa dakika ya 89 kutoka kwa Dejan Lovren katika mechi ambayo haikuwa na kiwango kizuri.

McClaren wiki iliyopita alieleza kwamba kujiamini kulikuwa kumepungua sana katika klabu yake, baada ya kuruhusu mabao manane katika mechi mbili zilizopita.

Wijnaldum amefikisha mabao saba msimu huu, baada ya kuwa amenunuliwa kwa pauni milioni 14.5 kutoka PSV Eindhoven Julai mwaka huu.

Liverpool hawakutarajiwa kucheza hovyo kiasi hicho, ikizingatiwa kwamba walitoka kuwacharaza Manchester City 4-1 na kisha kwenye Kombe la Ligi Jumatano iliyopita wakawatandika Southampton 6-1.

Pengine Klopp atajilaumu kwa uamuzi wake wa kufanya mabadiliko sita kwenye kikosi chake, ikiwa ni pamoja na kuwaondosha washambuliaji Daniel Sturridge na Divock Origi waliofunga mabao matano dhidi ya Saints.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Chelsea, Man City chali

Tanzania Sports

PSPF yatoa msaada wa vitanda Temeke Hosp