in , , ,

Liverpool mwendo mdundo

Mbio za ubingwa wa England zimeendelea kushika kasi baada ya Liverpool kujizolea pointi tatu muhimu na kupanda hadi nafasi ya pili kwa pointi zao 68 walipowafunga Sunderland usiku wa Jumatano.

Nahodha Steven Gerard aliendelea kufunga, lakini safari hii si kwa penati bali kwa shuti la umbali wa yadi 23 kutokana na mpira wa adhabu uliotokana na Santiago kumchezea rafu mbaya Luis Suarez.

Daniel Sturridge naye alifunga bao lake la 20 katika ligi hii, lakini ushindi haukuwa rahisi kwao licha ya kucheza nyumbani Anfield, kwa vile Sunderland walionekana tishio kwao, na walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Ki Sung-Yueng’.

Liverpool walijitahidi kulinda ushindi wao katika robo saa ya mwisho ili kuhakikisha kwamba wanawapita Manchester City waliokuwa wakishikilia nafasi ya pili kabla ya mechi hiyo. Hata hivyo, City wenye pointi 66 wana mechi mbili mkononi.

Kwa upande mwingine, kipigo hicho ni kichungu kwa Sunderland kwa sababu kimewaacha katika nafasi ya 18 wakiwa na pointi 25 kutokana na mechi 29 walizocheza. Nafasi ya 19 inashikwa na Cardiff wenye pointi sawa na Sunderland huku Fulham wanashika mkia kwa pointi 24. Hata hivyo, Sunderland wana mechi mbili mkononi.

Chelsea wanabaki wakiongoza ligi kwa pointi zao 69 baada ya mechi 31 sawa na Liverpool na Arsenal wanaoshika nafasi ya nne.

Katika mechi nyingine, West Ham waliwafunga Hull 2-1 katika mechi ambayo licha ya ushindi na kucheza nyumbani, walizomewa, kitu kilichomchukiza Kocha Sam Allardyce.  West Ham walikuwa na wakati mgumu, na mabao yao yalitokana na penati na jingine Hull kujifunga wenyewe.

Kipa wa Hull, Allan McGregor alipewa kadi nyekundu kwa kumwangusha Mohamed Diame. Hii ni kadi nyekundu ya pili kwake na anakuwa kipa wa kwanza katika msimu huu wa ligi kuu kuoneshwa kadi mbili nyekundu hadi sasa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Bayern watwaa ubingwa Ujerumani

Kichapo chawaduwaza Real Madrid