in , , ,

Liverpool, Manchester  kicheko tu

*Everton, Hull, Newcastle, Norwich safi

Klabu za Manchester City, Manchester United na Liverpool zimefanikiwa kupata ushindi katika mechi zao muhimu za Ligi Kuu ya England wikiendi hii.
Wakati Liverpool waliwanyoa Cardiff kwa mabao 6-3 na kupanda hadi nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kwa pointi zao 65, Manchester City waliwabomoa Fulham 5-0 na kushika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 63 lakini wana michezo miwili mkononi.

Ilikuwa wikiendi iliyoshuhudia karamu ya mabao kwenye viwanja vingi, kwani katika mchezo wa mchana Jumamosi hii, Chelsea waliwafunga Arsenal 6-0 na kupaa kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 69 wakati Arsenal waliporomoka hadi nafasi ya nne kwa kubaki na pointi zao 62.

Pamoja na ushindi wao, bado Man United wamebaki mbali katika nafasi ya saba kwa kufikisha pointi 51, zikiwa ni 11 pungufu ya wanaoshika nafasi ya nne – wanaotakiwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Everton nao walipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Swansea na kupanda na kufikisha pointi 54 na wanashika nafasi ya tano wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Katika mechi nyingine, Hull waliwafunga West Bromwich Albion 2-0, Newcastle wakapata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace wakati Norwich walipata ushindi muhimu wa 2-0 dhidi ya sikio la kufa – Sunderland.

Kwa matokeo ya Jumamosi hii, Fulham bado wanaburuta mkia kwenye msimamo wa ligi kwa pointi zao 24, zikiwa ni moja tu pungufu ya Cardiff walio nafasi ya 19 wakati Sunderland wana pointi 25 katika nafasi ya 18, wote katika hatari ya kushuka daraja wasipojiondoa humo kwa kushinda mechi zijazo.

Leo Tottenham Hotspur watawakaribisha Southampton katika mchezo wao wa 31 kwenye ligi hii, yakiwa ni majaribu zaidi kwa kocha Tim Sherwood, baada ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Arsenal na kutupwa nje ya Ligi ya Europa Alhamisi hii.

Spurs ambao wamekuwa wakifukuzia nafasi ya nne miaka nenda rudi ili washiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, wapo katika nafasi ya sita wakiwa na pointi 54 lakini wakicheza leo watakuwa wamewazidi wenzao (isipokuwa Chelsea) kwa mchezo mmoja.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Chelsea wawaadhibu Arsenal 6-0

Yanga wawapumulia Azam