Msimu mpya wa Ligi Kuu Italia maarufu kama Serie A umeanza wikiendi iliyopita. Fiorentina walikumbana na Torino, kisha Hallas Verona wakamenyana na AS Roma. Timu hizo ndizo zilifungua dimba, lakini zipo habari nyingi za kuzungumzia katika Ligi hiyo hadi kukamilika kwake. Ni nini mabingwa watetezi Juventus watafanya msimu huu? Je Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic wataendelea kucheza kwa viwango vya juu? Na vipi kiungo kutoka Marekani, Weston McKennie ataleta ladha gani katika Ligi hiyo? Vipi kocha mpya Andre Pirlo ataleta miujiza mipya Juventus ama taji lao litawatoroka? Tanzaniasports inakuletea majibu ya maswali yote.
MBIO ZA UBINGWA
JUVENTUS: Halitakuwa jambo la ajabu Juventus wakitafuta ubingwa wa kumi mfululizo wa Serie A. hii itakuwa timu ya kufuatiliwa mno msimu huu, hasa ikiwa na kocha mpya ambaye alikuwa miongoni mwa wanakandanda wakali dimbani, Andrea Pirlo. Juventus wameanza msimu huu bila wachezaji Gonzalo Higuain na Miralem Pjanic ambao wamehamia Inter Milan na Barcelona. Naye Blaise Matuidi ameondoka Juventus. Msimu huu utaonesha kama wamemerika zaidi au wameshuka.
Arthur Melo amewasili Serie A atakuwa sehemu ya kikosi cha Pirlo. Mbrazil huyo aliawahama miamba ya soka Barcelona baada ya kukosa namba kikosi cha kwanza pamoja na msimu mbovu wa timu hiyo. McKennie kuhamia Juventus nako ni habari kubwa ingawa mabosi wa Turin wanaona usajili wa Herculez Gomez ni spesho kwao kuliko McKennie.
INTER MILAN: hawa walishika nafasi ya pili msimu uliopita. Wananonelewa na kocha Antonio Conte, nao wana nafasi ya kutwaa ubingwa wa Serie A. Antonio Conte anatakiwa kuleta ubingwa klabuni hapo, vingine vyo hataweza kutwaa tena taji hilo. Arturo Vidal amewasili Inter Milan akitokea Barcelona. Sandro Tonali ataungana na Vidal kuimarisha eneeo la kiungo, wakati Achraf Hakimi aliyewika Bundesliga alipokuwa Borussia Dortmund kwa mkopo msimu uliopita, naye ni sehemu ya kikosi cha Antonio Conte akitokea Real Madrid. Conte amefanikiwa kumbakiza mshambuliaji wake Lautaro Martinez ambaye ndiye chachu ya mafanikio klabuni hapo.
ATALANTA: Inaonekana kama vile mechi ya watani wa jadi Serie A m,aarufu kama Derby d’Italia zitakuwa ngumu zaidi, kwa sababu huwezi kuiweka kando Atalanta ambao wamekuwa wkwenye kiwango bora kwa misimu miwili sasa. Msimu uliopita walibakiza dakika chache kucheza nusu fainali kabla ya kutolewa na PSG.
TATU; Timu tatu za Napoli,Roma na AC Milan nazo zinafanya jitihada za kuboresha vikosi yao., lakini wana kazi ya ziada ili kuzifikia timu tatu tulizozitaja hapo awali.
LAZIO: Wakati huo huo Lazio nayo itakuwa tayari kwa mashindano wakiwa na mataumini msimu huu ni nafasi yao ya kunyakua ubingwa. Lazio wameingia msimu huu wakiwa na maumivu baada ya kumkosa David Silva katika dakika za lala salama baada ya nyota huyo wa zamani wa Manchester City kubadili uamuzi na kurejea La Liga katika klabu ya Real Sociedad ya Hispania. Uamuzi huo ulimkera mkurugenzi wa ufundi wa Lazio, Igli Tare.
RONALDO AU ZLATAN?
Mastaa wawili wenye sifa kemukemu katika soka wataziwakilisha klabu zao za Juventus na AC Milan. Ni rahisi kusahau namna wanavyocheza katika umri wao wa sasa, lakini msimu uliopita Ronaldo alipachika mabao 31 katika mechi 33 za Serie A akiwa na Juventus waliotwaa ubingwa. Kwahiyo kulingana na takwimu hizo, tunaweza kumwongelea Ronaldo wa msimu mpya na Juventus yake, wataleta nini zaidi?
Mabosi wa Jeventus wanaamini Ronaldo bado hajaonesha kiwango chake kikubwa. Juventus wanatafuta mchezaji sahihi anayeweza kushirikiana na Ronaldo katika safu ya ushambuliaji. Mchezaji ambaye atafanya kazi ya kumtengeneza Ronaldo nafasi za kufunga. Juventus wanataka kuona kombinesheni kama ya Ronaldo na Karim Benzema iliyowapa mataji Real Madrid.
Ronaldo ana miaka 35 kwa sasa, ana nguvu nab ado anaonekana mpambanaji akiwa amebakiza misimu minne kabla ya kutundika daruga. Upande mwingine yupo Zlatan Ibrahimovic ambaye katika mchezo wa kwanza alipachika mabao mawili kwa AC Milan kwenye mechi ya kwanza ya Serie A msimu huu. Zlatan ana miaka 38, lakini anaonekana bado ana vitu vya kuwanufaisha AC
Milan.
Msweden huyo anaonekana ni mfalme wa San Sirro. Baada ya kujiunga na AC Milan Januari mwaka huu akiwa chini ya Stefano Pioli alichangia mabao 10 kati ya mechi 18 alizocheza na anaonekana bado ana vitu adimu vya kusaidia klabu hiyo. Wengi wanaweza kusema wanatarajia msimu huu utakuwa wa Ronaldo tena, lakini Zlatan huwa ana matukio ya kusisimua zaidi.
SURA MPYA ZA KUTAZAMA
Jumla ya pauni milioni 540 zimetumika kufanya usajili wa wachezaji 129 hadi wakati yanaandikwa makala haya. Dirisha la usajili Italia litafungwa Oktoba 5 mwaka huu.
Arthur Melo; Juventus wamelipa kiasi cha pauni milioni 64 kutoka Barcelona. Atakuwa mchezaji mwenye uchu wa kufanya kazi na Andrea Pirlo, akitarajiwa kuunda kombinesheni na Weston McKennie na Dejan Kulusevski aliyesajili januari mwaka huu.
Achraf Hakimi; usajili wenye kila aina ya pongezi kwa Inter Milan, ambao wamenunua beki huyo wa kulia kwa pauni milioni 36 kutoka Real Madrid. Hakimi alikuwa nyota msimu uliopita
pale Borussia Dortmund na alikuwa mmoja w amabeki wanaosakwa zaidi barani Ulaya. Inter Milan walichukua uamuzi wa haraka na makini kumsajili nyota huyo.
Barella na Sensi; Aleksandar Kolorov ni beki wa akiba upande wa kushoto, lakini eneo hilo limeongezewa nguvu kwa usajili wa Nicolo Barella na Stefano Sensi kutoka Vagliari na Sassuolo.
Vedat Muriqi; Lazio wao wameirisha kikosi chao kwa kuwasajili washambuliaji Vedat Muriqi kutoka Kosovo. Awali Muriqi alisajiliwa na Napoli, lakini baada ya kumnasa Victor Osimhen kutoka Lille kwa pauni milioni 63 wakaamua kumuuzaMuriqi. Kikosi cha Genaro Battuso kitanufaika na usajili wa Muriqi.
Kwingineko AS Roma wamemsajili Pedro kutoka Chelsea, lakini wana kazi ya kuboresha kikosi chao. Fiorentina wamemsajili Spfyan Amrabat kutoka Verona, na Cagliari wamekuwa kwenye hekaheka za kukamilisha usjaili wa Diego Godin, wakati AC Milan wameongeza mkataba wao na Zlatan, wakati Brahimi Diaz amechukuliwa kwa mkopo.
VITA YA NDUGU WAWILI
Filipo Inzaghi alikuwa mshambuliaji hatari uwanjani. Amewahi kuzichezea Atalanta, Parma, Juventus na AC Milan na mshindi wa kombe la dunia mwaka 2006, pamoja na Ligi ya Mabingwa mara mbili. Lakini ndugu yake Simone Inzaghi hakufanikiwa kama kaka yake Filipo. Simone alitumia muda wake kucheza klabu ya Lazio ambako alitwaa mataji ya Serie A na UEFA Cup, lakini hakuwa na mafanikio zaidi.
Kwa sasa wapo ndugu wawili Simone Inzaghi na Filipo Inzaghi ambao ni makocha. Simone Inzaghi ana miaka 44 aliteuliwa kuwa kocha wa Lazio mwaka 2016 kuchukua mikoba iliyoachwa na Marelo Biesla. Tangu awe kocha wa Lazio amechukua mataji matatu; Coppa Italia mara moja na Italian Supercoappa mara mbili. Lazio wamekuwa washindani wa Juventus katika kipindi ambacho kibibi kizee cha Turin kimeshika hatamu Serie A.
Filippo Inzaghi ana miaka 47, alianza maisha ya ukocha mwaka 2014 baada ya kukabidhiwa mikoba ya AC Milan, kabla ya kufukuzwa baada ya miezi 12 baada ya timu yake kushika nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi. Baadaye alikuwa kocha wa Venezia iliyofanikiwa kutwaa taji la Ligi daraja la Pili. Baadaye alihamia Bologna lakini alifukuzwa baada ya kushinda mechi 2 kati ya 21. Mbaya zaidi alifugwa mabao 2-0 na kikosi cha mdogo wake Simone Inzaghi, Lazio. Msimu uliopita Filipo Inzaghi alikuwa kocha wa Benevento ya daraja la pili ilitotwaa taji hilo na kufanikiwa kutengeneza falsafa yake ya kucheza.
MATAJIRI WA MAREKANI
Serie A imeshuhudia kuibuka vipaji kutoka Marekani katika uongozi na uwnajani. Juventus wamemsajili McKennie kwa dau kubwa la kihistoria Marekani. Msimu huu umeshuhudia
matajiri wa Marekani, Kyle Krauser akinunua Parma na Dan Friedkin ikiinunua AS Roma. Matajiri hao wa Marekani wameungana na Paul Singer aliyenunua Fiorentina
USIKOSE MECHI HIZI
Juventus vs Napoli; Oktoba 10
Inter Milan vs AC Milan; Oktoba 17
AC Milan vs Juventus; Januari 1, 2021
Lazio vs Roma; Januari 17, 2021.
Inter Milan vs Juventus; Mei 16, 2021
Comments
Loading…