Imebaki siku moja tuu kufika tarehe 29 April Jumapili ambayo inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka Tanzania na nje. Ni siku anbayo huenda ikaamua bingwa wa VPL kwa msimu wa 2017/2018.
Kuelekea mchezo huo utakaopigwa katika dimba lá uwanja wa Taifa Simba inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo kutokana na form walionayo. Lakini kwenye uhalisia mchezo bado ni mgumu kwa pande
Tumekuletea sababu tano ambazo zitaipa ushindi timu ya Yanga katika mchezo dhidi ya Simba;
Presha ya matokeo!
Simba SC wanaingia uwanjani wakihitaji matokeo ya ushindi ili kutangaza ubingwa mapema. Kwa jinsi ligi ilivyo na ‘gape’ la point lilivyo, Simba wanaingia uwanjani wakiwa na shauku ya kuifunga Yanga hivyo kurahisisha safari yake ya ubingwa.
Kwa Simba, wataingiaa uwanjani wakiwa na presha ya kutopoteza mchezo ili kuifanya Yanga iachane na ndoto za ubingwa na kuweka nguvu katika Kombe la Shirikisho Africa.
Yanga watafaidika na presha ya Simba katika mchezo huo na kuwafanya wacheze bila presha kama Ilivyo kwa wachezaji wa SimbaSc.
Yanga wanaingia kama “underdogs”
Kwa msimamo wa ligi na matokeo ya hivi karibuni kunaifanya Yanga kuingia kama wanyonge mbele ya Simba iliyo kwenye form ya hali ya juu msimu huu.
Hivyo basi wachezaji wa Yanga wataingia kwa nia ya kupambana toka mwanzo ili kupata matokeo. Kwa simba wao wataingia wakiwa wanajiamini na hivyo kucheza kwa “kurelax” kwa kuamini wanaiweza Yanga. Kwa kutumia faida hii Yanga wanaweza kupata ushindi na kuendelea kupunguza gape la point baina yao.
Beki ya Simba SC
Moja ya tatizo la Simba Sc katika msimu huu ni mfumo wake wa kucheza 3:5:2 ambapo kunakua na mabeki watatu nyuma. Lakini ukiangalia kwa makini mara nyingi mabeki wa SimbaSc hawapendi kusumbuliwa na wakikutana na washambuliaji wasumbufu huwa ni rahisi kufanya makosa. Mechi za Lipuli, Al-masry na Stand UTD zimeonyesha jinsi beki ya Simba inavyoweza kupitika.
Kwa aina ya uchezaji wa Chirwa utakua na faida sana kwa Yanga na kupata magoli kuipa matokeo timu yake. Presha katika eneo la ulinzi la Simba ni tatizo na Chirwa akishirikiana na Ajibu ni wachezaji wazuri kwa aina hiyo haswaa kutokana na kasi yao pia
Eneo la kiungo la SimbaSc.
Moja ya timu inayosifika kwa kua na viungo wazuri ni Simba, kwenye eneo lake la katikati ina wachezaji mahiri kama Ndemla, Mzamiru, Niyonzima, Kazimoto na Mkude. Lakini kwa siku za hivi karibuni kocha Mfaransa amekua akitumia viungo wa kati wenye asili ya ukabaji.
Amekua akitumia pacha ya kiungo ya Jonas Mkude na Shomary Kapombe/ Asante Kwasi au James Kotei, pia Erasto Nyoni hutumika kama kiungo wakati mwingine, hii humaanisha Simba inacheza kwa kudefence zaidi.
Kwa aina hiyo ya viungo kunaifanya SimbaSc kucheza bila kua na kiungo halisi wa ushambuliaji, ambapo Ndemla, Niyonzima na Kazimoto hawapewi nafasi siku za karibuni.
Kutokana na mfumo na upangaji timu wa Simba katika eneo la kiungo huenda ikaipa faida Yanga kutawala eneo la kiungo na hivyo kua rahisi kwao kupata matokeo.
John Bocco na Emmanuel Okwi
Unazungumzia wachezaji walifunga zaidi ya magoli 30 mpaka sasa, lakini pia ndio wanaongoza katika chati ya ufungaji bora mpaka sasa. Form nzuri ya Simba msimu huu inaendana na form nzuri ya upachikaji mabao ya Bocco&Okwi.
Hawa wawili ndio muhimili mkubwa wa safu ya ushambilliaji wa SimbaSc.
Kwa kuweza kuwazuia hawa ni sawa kuwazuia Simba wasipate ushindi. Mara nyingi SimbaSc imekua ikiwategemea hawa ili kupata ushindi na kushindwa kwao kufunga inaifanya Simba Sc kupata wakati mgumu kupata matokeo.
Andrew Vincent, Kelvin Yondani na Abdallah Ninja wakiweza kuwadhibiti hawa watu Yanga huenda ikapata matokeo.