in

Kwanini uwanja wa Yanga usiitwe GSM ?

yanga

Ile dunia ya ujamaa iliondoka na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na haitoweza kurudi tena. Tuko kwenye dunia ya kibepari. Dunia ambayo inaruhusu vitu vingi kufanyika katika jicho la kibiashara zaidi na kuliko kujuana.

Dunia ambayo ina lenga faida zaidi kuliko kutoa. Kila anayetoa kwenye hii dunia hutazamia apate faida. Ni ngumu kuirudisha dunia ya ujamaa kwa sababu imeshapita muda mrefu.

Jambo pekee ambalo mwanadamu anatakiwa kulifanya ni kufikiria namna gani ya kuishi kwenye dunia ya ubepari na kuacha kufikiria namna ya kurudisha ujamaaa.

Hapa ndipo Yanga inapoanza kukosea. Yanga muda mwingi inatengeneza mazingira ya kuishi kiujamaa na siyo mazingira ya kibepari  (kibiashara).

Muda mwingi hutumia kuwaaminisha watu kwenye kuchangia klabu ndiko kuna mafanikio makubwa . Kitu ambacho ukweli wake ni mdogo sana.

Hakuna anayekataa utaratibu wa kuichangia klabu ipate pesa lakini swali kubwa unaichangiaje hiyo klabu? Unatumia njia gani kuendesha huo mchango?

Hiyo njia ina faida yoyote kibiashara kwa mtu anayetoa pesa yake kwa klabu ? Huyo mtu ametengenezewa mazingira yapi ya kibiashara anapotoa pesa yake?

Hili ni swali kubwa ambalo Yanga wanatakiwa kulifikiria vyema. Juzi wametangaza utaratibu wa kuichangia klabu ili iweze kujenga uwanja wa mazoezi kule kigamboni.

Kitu hiki kilinishangaza sana. Nilifikiria kwenye dunia hii ya kibiashara , dunia ambayo kila mfanyabiashara anatamani bango la biashara yake lionekane kwa watu.

Lionekane kupitia sehemu ambayo inatazamwa sana. Yanga ni sehemu moja wapo inayotazamwa sana hapa nchini kwa sababu ya kuwa na mashabiki wengi sana.

Mfanyabiashara yoyote atatamani kuweka pesa yake ili aonekane kwa kiasi kikubwa na apate faida kutokana na kuweka pesa yake hiyo sehemu.

Kwanini Yanga wasitengeneze mazingira ya wao kuita wafanyabiashara wakubwa wajenge uwanja wao kwa makubaliano ya kibiashara.

Makubaliano ambayo yataendana na jina la uwanja wa Yanga kuitwa jina la bidhaa ya mfanyabiashara aliyejenga huo uwanja.

Mfano kama GSM atapata nafasi ya kujenga huo uwanja basi uwanja uitwe GSM Stadium kwa makubaliano ya muda fulani kama ni miaka mitano au zaidi.

Kuliko kuita mchango kwa ajili ya kitu ambacho hakijasimama kibiashara.  Watengeneze mazingira mazuri ya kibiashara,  mazingira ambayo yatawapa nafasi wadhamini kunufaika kuliko kuwachangisha bila kunufaika.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

69 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply
  1. Wakati mwingine ni bora kujiwekea malengo mtambuka kwa kuwa na uwanja mkubwa utakaotumika katika mashindano ya VPL na mechi za kimataifa , wafanyabiashara pamoja na wadau wengine wapewe fursa kwa kwa maslahi ya club .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Chelsea

Chelsea tayari kupigania ubingwa msimu huu?

Msimu mpya

Tutarajie nini msimu mpya wa soka?