in , , ,

Kwanini Moyes hakustahili kuvaa viatu vya Sir Alex, Man U!

Moyes, amekalia kuti kavu Man Utd…

Nianze kwa kusema kwamba David Moyes ni kocha mzuri sana na amefanya kazi ya ajabu iliyowapendeza wadau wa Everton.
Moyes alikabidhiwa timu ambayo ilikuwa kawaida yake kuwa nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi, na kubwa walilokuwa wakifanya ni kupigania kutoshuka daraja, na amewawezesha kumaliza katika nafasi nzuri.
Hata hivyo, pamoja na sifa zake anazomwagiwa, kuvaa viatu vya kocha maarufu kama Sir Alex Ferguson hakuhitaji tu mtu aliyepata kuwa kwenye ligi kuu, akafundisha na kutambia uzi wanaovaa makocha wenzake. Anatakiwa aliyepigania kweli mataji ya ligi kila msimu.
Moyes ana historia mbaya dhidi ya zile zinazoitwa ‘Bif Four’ tangu aanze kazi Goodison Park miaka 11 iliyopita. Safari zake zote za kwenda Anfield kukipiga na Liverpool; Old Trafford kwa Manchester United, Highbury na kisha Emirates nyumbani kwa Arsenal na Stamford Bridge kwa Chelsea zilikuwa patupu!
Raia huyo wa Scotland aliyetangazwa kumrithi Mskochi mwenzake, Alex Ferguson anayeng’atuka mwisho wa msimu huu hakupata kushinda hata mechi moja dhidi ya vigogo hao, ameambulia sifuri huko, amekuwa akitoka kaputi!
Hiyo si rekodi nzuri, hasa ikizingatiwa aina ya timu na wachezaji ambao Everton wamekuwa nao kwa miaka nenda rudi. Hiyo ndiyo aina ya misingi kwamba United wanatakiwa kushinda kwa uwiano mkubwa kabisa kati ya mechi zao.
Kubwa zaidi hapa ni kwamba, Man U wana dhamira ya kushinda Kombe la Mabingwa Ulaya – mashindano ambayo uelewa wake kwa Moyes unamzidi kimo (Everton walipoteza mechi ya kufuzu dhidi ya Villarreal 2005). Hebu tuambizane ukweli, Ferguson mwenyewe ilimchukua miaka kama saba hivi kuweza kuelewa na kujizoeaza kiufundi kwenye mashindano hayo. Washabiki wa United watakumbuka vipigo walivyoambulia, kama kile cha Gothenburg na Monaco. Je, klabu hii kubwa itakubali kipindi cha mpito cha kutokuwa tena tishio Ulaya? Tuje kwenye suala zima la usajili; japokuwa si kosa lake, kutumia kitita cha mapesa kupata wachezaji wazuri kwa Moyes ni kitendawili bado, yaani haelewi mambo hayo makubwa, kwa sababu Everton alitengewa kiasi kidogo mno kwa kazi hiyo na alikisahau mapema.
Ni kweli kwamba Moyes ambaye ni mdogo kiumri kwa Fergie kwa miaka 21 alionesha uerevu wa aina yake kwa kuweza kusajili watu wa aina ya Phil Jagielka, Tim Cahilland, Kevin Mirallas kwa kuwataja wachache. Itakuwaje anapotakiwa kuweka dau la wale wachezaji wa pauni milioni 20 au 30? Na je, katika bei hiyo, uamuzi wake utakuwa vipi?
Zaidi ya hapo, wachezaji kama Robert Lewandowski na Gareth Bale wamekuwa wakitajwa kuhusishwa na United siku za karibuni. Je, Moyes ataweza kuwavutia na kushawishi wachezaji wa kiwango hicho kujiunga Man U kwa namna ambayo angefanya Fergie au Jose Mourinho au Jupp Heynckes? Jamani, tusisahau kwamba kwa namna fulani ni Ferguson aliyemshawishi Robin van Persie kuwatosa Manchester City alikokaribia kusajili msimu uliopita wa kiangazi.
Iwe iwavyo, Moyes anao uwezo wa kadiri kama ambavyo amefanikiwa kuibadilisha Everton hadi kuwa timu ya kwenye ‘Nane Bora’ bila kutwaa kombe lolote. Ieleweke tu kwamba, uteuzi wake ni sawa na kutupa karata, hasa baada ya kipindi kirefu cha mafanikio walichokuwa nacho Manchester United. Sidhani kwamba United wapo tayari kupokea athari hasi zitakazotokana na kuwapo Moyes kwao; hebu waangalie kwa watani wao wa kweli wa jadi wa miaka nenda rudi, Liverpool kuona wanachotakiwa kufanya.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI TFF SEPTEMBA 29

Chelsea wahitaji pointi moja