Lipo swali moja muhimu kwanini Klopp na mkurugenzi wa michezo wa Liverpool Jorg Schmadtke wammeamua kumsajili Wataru Endo?
IMEFICHUKA kuwa marafiki,makocha na wachezaji wenye uhusiano wa karibu na kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp walimtumia ujumbe mfupi na kumpigia simu kuhusu ubora wa Wataru Endo. Nyota huyo ambaye ni amekuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Liverpool msimu huu ameibua maswali, kwanini Klopp amekubali kumleta katika kikosi chake. TANZANIASPORTS inakuleta tathmini yake, juu ya umahiri na ubora wa nyota huyo ambaye licha ya kuwa na umri wa miaka 30 ametua klabuni hapo kama ingizo jipya linalotarajiwa kubadili hali ya mambo klabuni.
ASKARI WA SAMURAI
Bila shaka umewahi kusikia kitu kinachoitwa Samurai. Kwenye mpira wa miguu kuna jina la Blue Samurai ambalo ni la Timu ya Taifa ya Japan. Basi tunakufahamisha nyota huyo alizaliwa kwao Japan. Samurai ni kikosi cha askari wa zamani vitani ambao walipigania ukombozi wa Japan. Sasa Liverpool wamesajili damu ya Kijapan inayotokana na Samurai. Nyota huyo amempa kiburi Klopp na kuamini kuwa hajakosea kumleta Liverpool. Klopp anaungwa mkono na makocha wengine kutoka Mainz na Borussia Dortmund kuwa Wataru Endo ni mchezaji mahiri ambaye ameweka alama katika klabu ya Stuttgart na Bundesliga.
DAU DOGO, KIPAJI KIKUBWA
Ingawa marafiki wa Klopp kutoka Ujerumani wanamsifia uamuzi wa kumsajili Wataru Endo, mwenyewe anaamini kuwa wamelipa fedha nzuri na rahisi kwa kipaji kikubwa. Endo amesajiliwa kwa pauni milioni 16.2 na mkataba wake utadumu hadi mwaka 2027.
SIRI TATU ZA ENDO
Lipo swali moja muhimu kwanini Klopp na mkurugenzi wa michezo wa Liverpool Jorg Schmadtke wammeamua kumsajili Wataru Endo? Zipo siri kuu tatu; Endo anaweza kucheza beki zote mbili za pembeni yaani beki wa kulia na kushoto. Pili, anaweza kucheza beki wa kati bila wasiwasi wowote akisaidiana na nahodha wake mpya Virgil na kuimarisha ukuta wa Liverpool. Tatu; ni mwili wa chuma ambao hauna matatizo ya majeraha ya mara kwa mara. Endo anasifiwa kutokuwa na mhanga wa kuumia na rekodi zake za kupata majeraha ni za kiwango cha chini hali ambayo inawapa matumaini kuwa atakuwa hivyo kwenye kikosi cha Liverpool.
MBABE WA BUNDESLIGA
Tangu msimu wake wa kwanza akiwa Bundesliga, Wataru Endo amepata asilimia nyingi kutokana na uwezo mkubwa wa soka. Endo amekuwa mchezaji wa tatu mwenye rekodi bora za ulinzi ikiwemo kutibua mipango ya adui. Ametibua mipango mara 254, ameokoa hatari za juu mara 219, amezuia mashuti kuelekea lango mara 175 na kupiga vichwa mara 105. Pia ni mwepesi wa kuelewa mifumo ya uchezaji wa timu.
NAHODHA WA SAMURAI
Ifahamike yeye nidye bosi wa wachezaji wakiwa ndani ya uwanja katika timu ya Taifa ya Japan. Yaani nidye nahodha wa kikosi cha Blue Samurai. Akiwa kwenye kikosi cha Liverpool amekuwa mchezaji wa tano ambao manahodha wa timu zao za Taifa. Manahodha wengine ni Andy Robertson (Scotland), Dominik Szoboszlat(Hungary),Virgil Van Dijk (Uholanzi) na Mohammed Salah (Misri). Wataru Endo amecheza mechi 50 za Timu ya Taifa ya Japan.
MAPAFU YA MBWA
Umewahi kusikia wachezaji wenye mapafu ya mbwa? Hawa ni wachezaji ambao hawachoki na wana mwendelezo katika uchezaji wao wa kandanda. Wataru Endo amekuwa na rekodi za kusisimua kwani katika misimu ya airbuni ya Stuttgart hajacheza mchi mbili tu. Mechi moja alikosa sababu ya ugonjwa wa korona na mwingine ulikuwa sababu ya masharti ya mtu aliyeambukizwa.
MZEE KAMA MILNER
Wengi wanashangaa kwanini Klopp amemsajili mchezaji mwenye umri mkubwa. Lakini Klopp mwenyewe anawajibu kwa ufupi sana. “James Milner alijiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka 29, na hakuna aliyemwelewa Milly. Ni mchezaji mzuri na mwenye haiba ya aina yake. Sasa Wataru Endo ni mchezaji tofauti lakini anaweza kuleta matokea mazuri kwa timu. Kilichotokea kwa Milner katika kikosi chetu ndicho Endo anaweza kukifanya.
ENDO MNAZI
Unaujua mnazi au sio. Lakini kwenye mpira wa miguu ukiambiwa mnazi maana yake mchezaji mrefu zaidi. Endo ana urefu wa Fti 5 na inchi 10 ana uwezo wa kuruka kwenda juu. Huyu ni mchezaji anayekwenda kuongeza ukuta mgumu wa Liverpool ambao msimu uliopita uligeuzwa nyanya na timu pinzani. Bila shaka anachukua nafasi ya Gomez au Joel Matip ambao wamekuwa wakipata nafasi ya kucheza kwa tabu huku msimu uliopita wakiwa chanzo cha kugeuza lango lao kuwa kapu la magoli. Je Endo atafanikiwa kuwanyamazisha washambuliaji hatari wa EPL? Ni jambo la kusubiri na kuona.
Comments
Loading…