in , , ,

KUFUZU KWA YANGA KUTUMIKE KIBIASHARA

Ndani ya miaka mitatu Yanga imefanikiwa kuingia katika hatua ya
makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika mara mbili.

Miaka hii mitatu ilikuwa na majira yanayotofautiana kabisa. Nyakati za
leo kwa Yanga zina majira magumu sana.

Hapana shaka hali ya uchumi wa Yanga ni mbaya, hakuna pesa nyingi kama
kipindi kile walipofanikiwa kuingia katika hatua ya makundi ya kombe
la shirikisho chini ya Yusuph Manji.

Leo hii hawana Manji, hakuna anayeweza kuwasimamisha tena , hakuna
anayeweza kuwasababisha wakimbie wakiwa na shibe.

Njaa ndilo vazi walilo nalo, vazi ambalo wamelikubali na kulipokea
kisha wakalivaa na kukimbia nalo.

Hawaoni soni , kitu cha muhimu kilichopo kichwani mwao ni kupigana kwa
ajili ya timu bila kujali magumu wanayopitia.

Wamefanikiwa kufuzu kwenda kwenye hatua ya makundi, unaweza kuwabeza
walikutana na timu dhaifu lakini kiuhalisi mpira wa Afrika kwa sasa
hauko hivo ndiyo maana Zamaleki ilitolewa na hawa ambao unaweza
ukawaona dhaifu.

Kwenye michuano hii ya kimataifa, Yanga imekuwa na wachezaji ambao
wanaonekana wa kawaida, lakini ndiyo hao hao ambao wameifikisha timu
hapo ilipo.

Leo hii wana Yanga wanayo furaha, na furaha yao ni kupata hizo milioni
600 baada ya kufanikiwa kuingia katika hatua ya makundi ya kombe la
shirikisho.

Kuna kitu kichwani mwangu kinaniambia Yanga wanatakiwa watumie nafasi
hii kibiashara kuliko kufurahia kuzipata hizo milioni 600.

Kwa namna gani wanaweza wakaitumia nafasi hii kibiashara?

Kuna njia nyingi ambazo mimi nimeziona zina tija kama watu
wakiwezekeza akili na muda wao kwenye hizo njia.

Kwenye Masoko (Marketing) four ( 4) Ps kuna vitu vifuatavyo.

-Product ( Bidhaa)
-Promotion
(Matangazo)
-Place ( sehemu)
-Price ( gharama)

Kufuzu kwa Yanga kwenda katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho
viongozi wa Yanga wanatakiwa wachukulie ni Product (bidhaa).

Hakuna kosa kubwa kibiashara kama wakichukulia kufuzu kwao katika
hatua ya makundi ya ƙkombe la shirikisho kama kitendo. Wakichukulia
kama kitendo ukawaida utakuwepo ndani yao hivo watachukulia vitu
kawaida tofauti na kama wakichukulia kama bidhaa hapa mtazamo wa
kuchukulia kawaida hautokuwepo.

Baada ya wao kuchukulia kama bidhaa kufuzu kwao katika hatua ya
makundi ya kombe la shirikisho wanatakiwa kuwekeza katika kuitangaza
bidhaa hii ya kufuzu kwao.

Promotion ( matangazo) yalenge vitu vifuatavyo. Moja kuwafanya
mashabiki wa Yanga kuona thamani kubwa ya bidhaa hii, waone ni jambo
kubwa na la kujivunia kama shabiki wa Yanga.

Pili, ilenge kujenga wateja loyal wa bidhaa hii, unawaletea bidhaa ya
Yanga kufuzu katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani
Afrika kipi watakipata cha ziada ambacho hakitokuwepo kwenye timu
zingine hapa Tanzania?

Wakimaliza hapo, wafikirie kuhusu mkataba wa Macron ambao unaanza
rasmi baada ya Yanga kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho
barani Afrika. Yanga watavaa jezi zilizotengenezwa na kampuni la
Macron na pia Macron watauza jezi hizi.

Hivo hapa ndipo kuna umuhimu wa ile “P” ya pili yani Promotion
(matangazo) , ushawafanya mashabiki wajivunie bidhaa yao ya kufuzu
hatua ya makundi na wakawa wateja loyal kwako kinachofuata wekeza
msukumo mkubwa katika kuhamasisha ununuzi wa jezi za klabu
zitakazouzwa na Macron katika utaratibu mzuri kibiashara ili wazitumie
kuja nazo uwanjani.

Yanga wana mechi tatu ( 3 ) za nyumbani katika michuano hii ya
kimataifa, hivo wanatakiwa kufikiria kutengeneza mazingira mazuri ya
kuuza tiketi na kuwashawishi mashabiki wengi uwanjani.

Mfano wakiwa na kampeni maalumu ya kwenda na Yanga kimataifa,
wakawatumia watu maarufu ambao ni mashabiki wa Yanga, wakatumia
mitandao ya kijamii, vyombo vya habari kuhamasisha na kuwahimiza watu
kuja uwanjani kwa ajili ya kusafiri na Yanga kimataifa, klabu itapata
pesa nyingi kupitia mapato hayo.

Kampeni hii iende sambamba na skafu zenye jumbe mbalimbali za kutia
moyo mfano , safiri na Yanga mpaka fainali hii itatia moyo kwa
mashabiki na wachezaji wa Yanga kwa kuonesha kuwa lengo la timu ya
Yanga siyo kuishia hatua ya makundi peke yake , lengo ni kufika
fainali. Umoja huu utaleta madhara chanya kwenye timu ( faida chanya
kwenye uchumi wa klabu na matokeo mazuri ya timu ndani ya klabu).

Tukumbuke vyote hivi vitaenda sambamba na Price (gharama) na Place( eneo)

Umeshatambua bidhaa yako (product), ukaifanyia Promotion (matangazo) ,
unaitafutia sehemu ya kuiuzia kisha unatenga gharama ya kuiuzia (
price).

Gharama za tiketi ziwe ambazo zinaweza kuwafanya watu wa kariba yote kumudu.

Baada ya hapo Yanga wanatakiwa kufikiria kitu kimoja, kipindi hiki
wamefika katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Michuano hii itaonekana sehemu kubwa, hivo kuonekana kwa sehemu kubwa
kwenye michuano hii inatoa tafasri moja nayo ni kuwa Yanga
wametengeneza soko kubwa kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa zao kupitia
Yanga.

Hivo basi, Yanga wanatakiwa kukaa chini na kuandaa ushawishi ambao
utamwezesha mfanyabiashara aje kutangaza bidhaa yake kupitia jezi ya
Yanga.

Hakuna mfanyabiashara asiyependa bidhaa yake itangazwe sehemu kubwa
ili kupata wateja wapya na bidhaa yake ijulikane sehemu tofauti, hivo
hii ni nafasi ambayo Yanga wanaweza kutumia kuwashawishi wafanya
biashara kuja kuwekeza kwao kipindi hiki.

Na hii itafanya kesho yao kuwa bora zaidi kuliko leo yao yenye thamani
ya milioni 600.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

WENGER NI LAZIMA AENDE ILI ARSENAL WAWE WASHINDANI WA KWELI

HATIMAYE WENGER KANG’OKA ARSENAL