in , ,

KIPI WAKIFANYE SIMBA ILI WASHINDE MECHI DHIDI YA AZAM?

Inawezekena tatizo walilonalo Azam lipo kwa Simba pia. Kwa hizi siku
za karibuni tangia mzunguko wa pili uanze, safu ya ushambuliaji ya
Simba imekuwa butu sana.

Mzunguko wa kwanza viungo wengi wa Simba walikuwa wanahusika sana
katika ufungaji wa magoli yani kina ( Kichuya, Mohammed Ibrahim na
Mzamiru Yasin).

Hali hii imetoweka katika mzunguko huu wa pili.

Kitu kimoja ambacho Simba wanatakiwa wakifanye ili kuwezesha uwezekano
wa viungo wao na washambuliaji wao kuhusika kwenye magoli.

Cha kwanza ni namna ya Kumchezesha Mzamiru Yasin. Siku zote kama
unataka uone huduma ya Mzamiru ikiwa bora unataka umfanye awe huru
kwenye nafasi yoyote anayocheza.

Mfano ,kama utamchezesha pembeni unatakiwa umpe uhuru wa yeye kuwa
anaingia eneo la katikati mwa uwanja na eneo la box ya timu pinzani
akitokea pembeni.

Kitu hiki amekuwa akikikosa sana kwa mechi za hivi karibuni kwani
amekuwa akikaa zaidi pembeni bila kuwa na uhuru wa kutembea maeneo ya
katikati mwa uwanja na pembeni mwa uwanja.

Sasa kipi kinachotakiwa kifanywe leo?

Kwa jinsi ninavyoona kama Mzamiru Yasin atacheza kama false namba 9
pamoja na mshambuliaji ambaye hakai sana eneo la box la timu ya Azam
ili iwe rahisi kwao kubadilishana nafasi katika eneo hilo.

Kumchezesha kama false 10 kutampa uwezo kwake yeye Kuwa anachukua
mipira katikati mwa uwanja na pia kutampa uwezo wa kukaa karibu na
eneo la kumi na nane ya Azam. Kwani tumeona amekuwa mzuri sana kwenye
mipra ya re-bound, hivyo kumpa uhuru wa kukaa karibu na Kumi na nane
ya Azam kutamfanya awe na uhakika zaidi wa kufunga.

Hapo juu nimezungumzia kuhusu Simba Kumchezesha Mshambuliaji ambaye
hatulii mara kwa mara kwenye eneo la kumi ya nane ya Azam.

Nimesema hivi kwa sababu ukuta wa Azam ni mgumu, na mabeki wa kati wa
Azam ni wazuri kwa mipira ya juu hata kinguvu ni wazuri na hawafanyi
makosa yasiyo na msingi.

Hivo Simba wanatakiwa kuwalazimisha mabeki hawa kufanya makosa.

Sasa watawalazimishaje kufanya makosa?

Kumchezesha Mshambuliaji kama Ajib pale mbele, pembeni ukamweka
Kichuya na Mnyate. Nyuma ya Ajib akawepo Mzamiru Yasin, hii itakuwa
na maana kubwa sana kwa sababu watu hawa wote watakuwa na uwezo wa
Kubadilishana nafasi pale mbele kitu ambacho kinaweza kuwachanganya
mabeki wa kati wa Azam na kuwalazimu kufanya makosa binafs.

Kwa pamoja Simba na Azam wamekuwa na safu imara ya ulinzi ila tatizo
lao wote wamekuwa butu kwenye eneo la ushambuliaji.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

KIPI WAKIFANYE AZAM ILI WASHINDE MECHI DHIDI YA SIMBA?

Tanzania Sports

NILICHOKIONA KWENYE MECHI YA AZAM NA SIMBA