in , ,

KIPI WAKIFANYE AZAM ILI WASHINDE MECHI DHIDI YA SIMBA?

Kitu pekee cha kujivunia kwenye kikosi cha Azam ni safu yao ya ulinzi
inavyocheza kwa ushirikiano mkubwa.Katika mechi 7 zilizopita
hawajaruhusu hata goli moja.

Wakati Yakubu na Morris wakiwa na maelewano makubwa na kufanya kuwa
imara kwenye safu yao ya ulinzi, hali ni tofauti kwa washambuliaji
wao.

Yahaya na Bocco kwenye mechi 7 zilizopita kwa pamoja wamefunga goli
mbili tu. Na hii ni kwa sababu kati yao hakuna anayeweza kucheza kama
mshambuliaji wa pili.

Wote kwa pamoja wanasifa za kucheza kama washambuliaji wa kati kwa
sababu wana nguvu, uwezo mkubwa wa kucheza mipira mirefu inayokuja
kwao, kucheza mipira ya kichwa na mwisho wote wanauwezo wa kufunga.

Mshambuliaji wa pili ni mtu anayekosekana katika timu ya Azam FC na
hii ndiyo sehemu ambayo Azam FC wanatakiwa kuifikiria zaidi kuelekea
mchezo wa Simba.

Mshambuliaji wa pili siku zote ana majukumu ya kuchukua mipira eneo la
kiungo wa kati na pembeni kisha kuisambaza kwa mshambuliaji wa kati.
Pia mshambuliaji wa pili haishii kutoa huduma za mipira pekee kwa
mshambuliaji wa kati ila anatakiwa awe na uwezo wa kufunga pia.
Sasa nani anafaa kuziba udhaifu huu wa Azam ?

Kwanza eneo la kiungo cha ulinzi kibaki chini ya Stephano. Himid Mao
au Frank Domayo mmoja wao anaweza akacheza na Stephano.

Mahundi na Sureboy wamekuwa wakileta uwiano mzuri kwenye kiungo cha
ushambuliaji cha Azam kwani mara nyingi huwa wanaingia eneo la
katikati ya uwanja wakitokea pembeni.

Kwa umbo la Bocco, uzoefu wa mechi za Simba, uwezo wake wa kufunga
ndicho ambacho naonelea kimfanye acheze kama mshambuliaji wa kati,
huku mshambuliaji wa pili awe Ramadhani Singano.

Kumchezesha Ramadhani Singano kama mshambuliaji wa pili kitakuwa na
faida zifuatazo kwa Azam. Kwanza Kutakuwa na mbadilishano wa majukumu
na nafasi kati ya Sure boy, Mahundi, Singano. Wote watatu kwa
nyakati tofauti watakuwa na uwezo wa kucheza kwa kubadilishana mfano
wakati Singano akienda pembeni mmoja kati ya Sureboy au Mahundi
anauwezo kwenda kucheza katika eneo la mshambuliaji wa pili.

Hii itamsaidia sana Bocco kupata huduma nyingi kutoka kwa hawa watu wa
tatu Singano, Mahundi, Sureboy.Na kwa sababu Bocco ni mzuri zaidi
kwa kufunga nina uhakika Azam watapata magoli mengi.

Pia hii itawapa uhuru kina Singano, Mahundi na Sureboy kucheza kama
wachezaji huru katika eneo la mbele na inaweza ikawa faida kwa mmoja
wao kufunga goli.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Liverpool bila Mane si kitu?

Tanzania Sports

KIPI WAKIFANYE SIMBA ILI WASHINDE MECHI DHIDI YA AZAM?