in , , ,

Kipa Begovic na rekodi ya Guinness 

 
*Ni kwa kufunga bao la mbali zaidi

Golikipa wa Stoke City, Asmir Begovic ameingia kwenye vitabu vya rekodi kutokana na bao lake alilofunga akiwa mbali na goli.

Begovic alifunga bao hilo dhidi ya Southampton Novemba mwaka jana, na baada ya vipimo kukamilishwa, imetangazwa kwamba ndilo bao la mbali zaidi.

Ataingizwa rasmi kwenye ‘Guinness World Records 2015 Book’, akishikilia rekodi ya mchezaji aliyefunga bao akiwa mbali zaidi na goli la adui.

Alifunga bao hilo katika sekunde ya 23 ya mechi, ambapo alipiga mpira uliozungushwa kwa upepo umbai wa mita 91.9 sawa na futi 301  na inchi sita, umbali ambao hakuna mchezaji aliyefanikiwa kufunga.

Baada ya mpira huo kufika langoni mwa Saints, ulimgonga kipa wao, Arthur Boruc na kuzama nyavuni kwenye mechi iliyochezwa Britannia Stadium.

“Nafurahishwa sana kupewa heshima jinsi hii na kama kipa sikutarajia kitu kama hiki kutokea, hasa kwa kuweka rekodi ya pekee, naipokea kwa furaha.

“Kwa kweli nashukuru kwa tuzo hii pamoja na cheti nilichopewa ambacho ni wazi vinanipa fahari kubwa na nitavitafutia sehemu nzuri ukutani nyumbani kwangu.

“Shukurani zangu nazitoa kwa kila mmoja huko kwenye Rekodi za Dunia za Guinness kwa kunikabidhi tuzo hii ya aina yake,” anasema.

Wachezaji wengine wanaoingia kwenye toleo hilo la rekodi ni mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo; bondia Floyd ‘Money’ Mayweather Jr; mfukuza upepo wa Jamaica, Usain Bolt; mcheza tenisi Roger Federer; Rory McIlroy na Tony McCoy.
 
Ronaldo ameingia huko kwa kufunga idadi kubwa zaidi ya mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwani alicheka na nyavu mara 15 msimu uliopita.

Kadhalika ametamba kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi kwenye ukurasa wake wa Twitter, wakizidi watu milioni 25.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

England wawafunga Norway kwa tabu

Van Persie amwonya Falcao