in

Kati ya Bumbuli na Nugaz mmoja atoke Yanga

Kuna tatizo kubwa sana kwenye idara ya mawasiliano katika klabu ya Yanga. Idara hii ni muhimu sana kwenye taasisi yoyote ile kwa sababu ndiyo idara ambayo hutoa picha halisi ya taasisi husika.

Taasisi inaweza kuonekana bora au dhaifu kwa watu kama idara ya mawasiliano ya taasisi husika itakuwa imara au bora. Idara ya mawasiliano ya taasisi yoyote inaweza ikaficha hata madhaifu ya taasisi husika.

Idara ya mawasiliano  pia inaweza ikatangaza mazuri ya taasisi husika na taasisi kuonekana katika picha ambayo inavutia kibiashara nje ya taasisi.

Kumekuwa na utata mkubwa katika utoaji wa habari mbalimbali katika taasisi ya Yanga. Utata ambao unaonesha madhaifu makubwa ndani ya taasisi ya Yanga.

Madhaifu ambayo yanaifanya Yanga ionekane na picha ambayo haivutii nje ya taasisi katika jicho la kibiashara.

Ushirikiano wao kikazi una maswali mengi
Ushirikiano wao kikazi una maswali mengi

Madhaifu ambayo yanaifanya Yanga ionekane taasisi isiyoendeshwa kwa utaratibu ambao ni maalumu na wenye kuvutia.

Kuna nyakati unaweza ukakosa ni yupi msemaji wa taasisi ya Yanga. Kuna wakati unaweza ukamsikia mwenyekiti wa klabu akitoa taarifa ambayo inakinzana na GSM ambao ni wadhamini wa klabu hiyo.

Kuna wakati GSM hutoa taarifa ambazo zinakinzana na mwenyekiti wa klabu hiyo. Kuna wakati mwenyekiti msaidizi wa klabu ya Yanga anaweza kutoa taarifa ambayo inakinzana na mwenyekiti wa klabu.

Kuna wakati mwenyekiti msaidizi anaweza kutoka nje ya klabu na kusema anafanyiwa figisu figisu ndani ya klabu ya Yanga na viongozi wenzake.

Kitu ambacho kingeweza kumalizwa na vikao vya ndani vya viongozi wa klabu ya Yanga na siyo kuyatoa nje ya Yanga. Hapa picha inayochafuliwa ni ya Yanga na kiongozi husika.

Kiongozi huyu anajishushia thamani bila yeye kujua . Inawezekana anaweza akawa anasema anaonewa na viongozi wenzake kwa minajili ya kupata huruma kwa mashabiki.

Lakini mwisho wa siku picha yake inachafuka, anaonekana hana weledi. Haishii kuichafua picha yake peke yake tu ila picha ya taasisi ya Yanga inachafuka kwa sababu anatoa madhaifu ya taasisi.

Kwenye dunia hii ya ushindani wa kibiashara kulinda picha ya taasisi ni kitu cha muhimu sana. Picha ya taasisi husika ndiyo hujenga mahusiano mazuri ya kibiashara nje ya taasisi.

Ndiyo maana taasisi nyingi huajiri  watu wa mahusiano ya jamii. Kwenye klabu ya Yanga watu wa mahusiano ya jamii ni Antonio Nugaz na Hassan Bumbuli.

Hawa ndiyo wanaotakiwa kuifanya picha ya Yanga iwe inatazamika vyema kwenye jamii. Hawa ndiyo wanaotakiwa kuiunganisha picha ya Yanga kwa jamii.

Hawa walitakiwa kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha wanaijenga picha ya Yanga ionekane vyema. Picha ya Yanga ni Chapa ya Yanga.

Moja ya njia nzuri ya kujenga Chapa bora ni ya taasisi ni taasisi husika kutoa taarifa ambazo ni nzuri nje ya taasisi. Kuwe na mfumo sahihi za utoaji wa taarifa.

Hili kwa Yanga halipo. Kwa Yanga kila kiongozi ni mtoaji wa taarifa na taarifa zenyewe huwa zinakinzana kwa viongozi husika.

Mfano,  Hassan Bumbuli alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa mashabiki wa Yanga wanatakiwa kwenda uwanja wa ndege kumpokea Yacoub Sogne lakini Antonio Nugaz akakanusha kuwa hiyo siyo taarifa ya klabu.

Katika ujengaji imara wa Chapa utoaji wa taarifa ni kitu cha muhimu. Hawa wawili ndiyo wamepewa jukumu la kutengeneza picha nzuri ya Chapa ya Yanga kwa jamii. Kama wakishindwa inatakiwa mmoja wao atoke.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Kocha wa YANGA kaja kuifunga Simba

Arsenal

Arsenal wameanza kama walivyomaliza msimu