Nahodha wa England anasema penati aliyokosa dhidi ya Ufaransa ilimfanya kuwa mchezaji bora zaidi Kane aahidi kurejea kwa nguvu katika Kombe la Dunia 2026
Harry Kane amesema kuwa penati aliyokosa dhidi ya Ufaransa katika robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2022 ilimpa maumivu makubwa zaidi katika maisha yake ya soka, lakini pia ikamfanya kuwa mchezaji mwenye nguvu zaidi kiakili na kitaaluma. Nahodha huyo wa Uingereza sasa anasema amejifunza kutokana na kosa hilo na analenga kuongoza taifa lake kutwaa ubingwa wa dunia msimu ujao.
Katika mchezo huo uliochezwa Qatar, Kane alikosa penati dakika ya 84, England ikitolewa kwa kichapo cha mabao 2–1. Tukio hilo limebaki kuwa kumbukumbu mbaya zaidi kwake, hata kuliko kupoteza fainali tatu akiwa Tottenham Hotspur, ikiwemo ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019.
“Nadhani huo ulikuwa wakati mgumu zaidi katika maisha yangu,” alisema Kane. “Nilihisi kama jukumu lote lilikuwa mabegani mwangu. Nilikosa kitu ambacho nimefanikiwa mara nyingi maishani. Hilo ndilo lilikuwa gumu zaidi kulikubali.”
Baada ya tukio hilo, Kane alianza kuboresha mbinu zake za kupiga penati, akianzisha mtindo wa kusita kidogo kabla ya kupiga mpira ili kumsubiri kipa aonyeshe upande anaokwenda. Matokeo yake yamekuwa ya kuvutia.
Mshambuliaji huyo wa Bayern Munich alifunga penati 31 mfululizo kwa klabu na timu ya taifa baada ya tukio la Qatar. Mfululizo huo uliishia mwanzoni mwa msimu huu alipokosa penati katika Kombe la Ujerumani dhidi ya Wehen Wiesbaden, lakini tangu hapo amefunga tena penati sita mfululizo.
Penati yake ya hivi karibuni ilikuja katika ushindi wa 5–0 dhidi ya Latvia mjini Riga, ushindi uliowahakikishia England tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika Marekani, Kanada na Mexico.
“Kila wakati ninajaribu kujifunza kutokana na matukio kama hayo,” alisema Kane. “Baada ya ile penati, nilifunga 31 bila kukosa. Nilibadilisha mbinu yangu kidogo na nikajivunia maendeleo hayo. Ndiyo kumbukumbu yangu ya mwisho ya Kombe la Dunia, kwa hivyo ninatazamia nafasi nyingine kuweka mambo sawa – kufika mbali zaidi, kuinua kombe kama tunavyoota sote.”
Kane aliongeza kwamba tukio hilo lilimfanya kuimarika zaidi kama mchezaji na kama kiongozi.
“Njia nilivyojifunza kutokana na hilo na jinsi lilivyonipa motisha ya kuboresha si tu penati zangu, bali mchezo wangu kwa ujumla – ndilo lililonifanya kuwa mchezaji bora zaidi.”
Baada ya kufunga mara mbili dhidi ya Latvia, Kane amefikisha magoli 76 akiwa na timu ya taifa ya England. Hiyo inamfanya kuongoza kwa mbali katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa taifa hilo, rekodi ya Wayne Rooney ya mabao 53 ikiwa sasa historia.

Kane, mwenye umri wa miaka 32, amesema anahisi bado yuko kwenye kiwango cha juu zaidi na anaamini anaweza kufikisha magoli 100 kwa England kabla ya kustaafu.
“Namna ninavyojisikia sasa, sidhani kama ninapunguza kasi. Niko kwenye kiwango kizuri na nataka kuendelea kwa muda mrefu. Niko kwenye mabao 76 sasa, yanabaki 24. Tuna michezo kadhaa kabla ya Kombe la Dunia, kwa hivyo nitajaribu kuikaribia hiyo mia.”
Kane pia amekuwa na msimu mzuri akiwa Bayern Munich, ambapo amefunga mabao 18 kwa klabu hiyo na matatu kwa timu ya taifa.
“Nadhani niko katika kiwango bora zaidi maishani mwangu,” alisema. “Namba zinaonyesha hivyo. Namna ninavyojisikia uwanjani, jinsi ninavyoona mchezo, jinsi ninavyoshiriki bila mpira — najihisi niko kwenye kiwango cha juu zaidi msimu huu.”
Kocha wake wa Bayern, Thomas Tuchel, aliyemsajili kutoka Tottenham majira ya kiangazi mwaka 2023, alimpongeza kwa nidhamu na umakini wake mkubwa katika mazoezi na uchezaji.
“Kwangu, yeye ni mchezaji ambaye hakosi penati,” alisema Tuchel. “Alipokosa dhidi ya Wiesbaden hakufurahia, lakini nilihisi ni afadhali imetokea sasa. Nilifikiri, ‘Vizuri, sasa tunaanza mfululizo mpya.’ Yuko katika hali bora. Juhudi anazoweka katika mazoezi ya penati ni za kipekee – sijawahi kuona kitu kama hicho.”
Kwa Kane, safari ya kulipiza kisasi Qatar imeanza. Na kama alivyoonyesha kwa uthabiti wake ndani na nje ya uwanja, ni wazi anataka historia yake katika Kombe la Dunia ijandikwe upya mwaka 2026.


Comments
Loading…