in , , ,

Jurgen  Klopp na ukocha wa makocha

Jurgen Klopp

WAKATI anaacha kazi katika klabu ya Liverpool aliwaambia wanachama na washabiki kuwa ameihsiwa maarifa na mawazo mapya ya kuipaisha timu yao. Kama kuna wakati ambao Liverpool walianza kupoteza matumaini au kutengeneza njia ya kushindwa kupambania ubingwa wa England basi ni kipindi hiki. 

Matokeo ya Jurgen Klopp kutangaza angeondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu lilikuwa tangazo la kurudisha nyuma mapambano ya ubingwa. Pengine zinaweza kuwa hisia tu lakini ukweli unabaki Liverpool haikuwa ile iliyokuwa inaendeleza cheche iwe kubwa ama ndogo lakini kulikuwa na kila dalili kuitishia Man City kwenye vita vyua ubingwa.

Hata hivyo Jurgen Klopp alipoondoka alielekea jijini Mallorca kuanza maisha yake mapya na familia yake. Klopp ni mwalimu mzuri, mpambanaji na mwenye falsafa inayoeleweka katika kandanda. Ni watu wachache wanaofahamu juu ya falsafa yake ya Gegenpressing katika kandanda. Klopp ameshinda kila taji ambalo mwalimu wa kandanda barani Ulaya angependa kunyakua. Ameshinda Ligi ya Mabingwa na taji la EPL kama ilivyokuwa kwa Ujerumani. 

Lakini Jjina la Jurgen Klopp limerudia kwenye vichwa vya habari kwa kasi kwa namna mbili; namna ya kwanza ani ajira mpya aliyopata katika kampuni ya Red bull ambayo inamiliki timu kadhaa za kandanda, na pili jina lake limerudi na hasira za mashabiki wa Borussia Dortmund ambao wanapiga kelele huko Ujerumani kulalamikia kile wanachokiita usaliti kutoka kwa mtu wao wanayemwamini. Jurgen Klopp alikuwa kocha wa Borussia Dortmund kw amuda mrefu, aliwageuza wachezaji chipukizi kuwa miamba ya sokia Bundesliga. Alipambana na utawala wa Bayern Munich na kutamba kwenye Ligi ya Mabingwa. 

Kwa sasa Jurgen Klopp anakuwa kocha mkuu wa vilabu vinavyomilikiwa na Red bull. Hatuwezi kusema Klopp atakuwa akionekana mara kwa mara kwenye viwanja vya soka akiongoza timu, hapana. Lakini Jurgen Klopp ndiye kocha wa makocha wa vilabu vya Redbull vya nchi za Ujerumani, Marekani na Austria. Timu hizo ni Red bull Salzburg, RB Leipzig, na New York Red bull. Klopp ataanza kazi ya ukocha wa makocha ifikapo Januari mosi mwaka 2025. Ajira yake itanaanza rasmi na atakuwa na majukumu ya kuwawezesha mabenchi ya ufundi na kurugenzi za michezo katika klabu hizo hapo juu. 

Kwa mujibu wa taarifa iuliyotolewa na Redbull inaeleza kuwa Jurgen Klopp atakuwa na majukumu ya kutoa ushauri kwa makocha wa vilavy vya Leipzig, Salzburg na New York Rebull. Majukumu hayo yataambanishwa katika maeneo yafuatayo; kuwashauri viongozi na benchi la ufundi kuhusu falsafa ya timu katika uchezaji,kukuza na kuendeleza vipaji,namna ya kusajili wachezaji wazuri wenye kuendana na falsafa ya timu yao, kuendeleza na kuibua wachezaji pamoja na makocha. Kimsingi kutakuwa na mashauriano kati ya Jurgen Klopp na makocha wa timu hizo hapo juu. 

Akizungumza na vyombo vya habari Jurgen Klopp alisema, “kwa miaka takribani 25 nilikuwa nasimama kwneye benchi la ufundi kutoa maelekezo kwa wachezaji, kusimama katika eneo la kocha uwanjani ni tofauti na jukumu la sasa. Nina hamu kubwa ya kutumikia nafasi mpya na kuona namna gani nitashiriki kuleta matokeo chanya katika mradi huu wa sasa. Jukumu langu huenda limebadilika lakini ari na hamasa yangu bado ipo palepale kwa mchezo wa soka pamoja na watu wanaojihusisha na mchezo huo. Kwa kujiunga na Redbull katika nafasi ya ukuu wa makocha kimataifa, nataka kuwaendeleza,kukuza na kuunga mkono juhudi za kuufanya mcehzo wa soka uwe wenye vipaji vingi na kwamba nitatoa mchango wangu kwa asilimia zote. Zipo namna nyingi za kucheza soka ambazo zinaweza kutumika na kuleta matokeo ya kiwnago cha juu, kuanzia elimu,uzoefu na nafasi muhimu zinazopatikana kwa timu za Redbull. Kwahiyo pande zote tunakwedna kujifunza namna bora na kuendeleza mchezo huo unaopendwa duniani.”

Huu n impango mpya ambao haujawahi kufanyika, kwa kocha kuajiriwa kutoa mafunzo au mashuariano na makocha wakuu wa vilabu. Tangu alipoondoka Liverpool ilihisiwa angerudi viwanjani siku moja lakini hakuna aliyetarajia kama angekuja namna hii. Kwamba mchezo wa soka unazidi kutanua mbawa zake na kuonesha nguvu ya uchumi dhidi ya michezo mingine, hivyo wawekezaji wapo tayari kuajiri makocha kama Jurgen Klopp. Hii ni pensheni ambayo inampa nafasi ya kutengeneza falsafa ya kucheza kandanda katika kiwango bora kwa miaka mingine ijayo kupitia vilabu hivyo. Ingawa mashabiki wa Dortmund wamekasirika lakini ukweli ni kwamba Klopp bado anahitajika katika ulimwengu wa soka, si mtu kusema amepitwa na wakati.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

10 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

MSHERY ATAPOTEA KAMA KABWILI?