inawezekana kwa kiasi kikubwa Diego Costa ameoneshwa mlango wa kutokea
mara baada ya jana Chelsea na Real Madrid kukubaliana dau la uhamisho
wa Morata kwenda Chelsea.
Awali kulikuwa na mahitaji mawili, la kwanza lilikuwa la Morata na la
pili lilikuwa la Belloti.
Kumchukua Morata mbele ya Belloti hii inafaida kubwa sana kwa Chelsea.
Pamoja na kwamba Morata ana wastani wa ufungaji wa magoli kwa dakika
alizocheza ni mzuri kuliko wa Belloti pia Morata amekuwa mchezaji
ambaye ameshirika mara nyingi UEFA na kuwa na medali ya ushindi na
ushindi wa pili, kombe ambalo Chelsea atakuwa anashiriki msimu ujao
Kwa hiyo kumwingiza Morata katika kikosi cha Chelsea itakuwa na faida
kubwa katika michuano ya ulaya kwa sababu ni mchezaji ambaye amezoea
hayo mashindano.
Morata mpaka sasa amecheza katika ligi mbili tofauti, hii ligi ya
Uingereza inaenda kuwa ya tatu. Kucheza kwake Seria A na La Liga
inaonesha ni mchezaji ambaye amekomaa kucheza katika ligi yoyote na
hii inakuwa faida sana kwenye kikosi cha Antonio Conte.
Antonio Conte msimu uliopita katumia mfumo wa 3-4-3 , ambapo mbele
ilikuwa inamwezesha kuwachezesha Hazard, Pedro/ Willian na Costa.
Kwenye mfumo huu pia Morata anaweza akacheza kwenye nafasi ya Costa.
Lakini kama Conte ataamua kumtumia Morata na Costa kwa wakati mmoja
itabida abadili muundo wa mfumo kidogo. Itamlazimu atumie mfumo wa
3-5-2 ambapo mbele Morata atcheza nyuma ya Costa. Ambapo Hazard
itambidi atokee chini kidogo.