KIPIGO cha mabao 7-2 walichopata mabingwa watetezi wa EPL, Liverpool kimeshangaza wapenzi wa kandanda duniani. Mpaka dakika 38 ya mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Villa Park, mabingwa watetezi walikuwa wamechapwa mabao 4-1.
Liverpool walipata kipigo hicho saa chache baada ya mabingwa wa zamani Man United kuzabwa mabao 6-1. Vipigo hivyo vimekuja wiki moja baada ya mabingwa wa zamani Leicester City kuwazaba Man City kwa mabao 5-2 kwenye mfululizo wa Ligi Kuu England.
Takwimu zinaonesha kipigo cha Liverpool ni kikubwa kwa bingwa mtetezi tangu mwaka 1953. Kikosi cha Jurgen Klopp bila shaka hakikutegemea kukumbana na kipigo kikali cha namna hiyo, hasa kutoka timu iliyonusurika kushuka daraja msimu uliopita.
ATHARI ZA CORONA
Inawezekana ikawa jambo la haraka kushuhudia vipigo hivyo, lakini EPL imeanza msimu huu ikiwa katika mazingira ambayo hayakuzoeleka kama ilivyokuwa misimu mingine.
Timu zilikuwa na wiki za kujiandaa kwaajili ya msimu mpya kuliko vipindi vya nyuma. Dirisha la usajili limefungwa Oktoba 5 mwaka huu. Soko la mauzo na manunuzi ya wachezaji limeathiri msimu kwa ujumla wake kutokana na ugonjwa wa Corona.
Liverpool kama zilivyo timu zingine imeathiriwa kimapato. Lakini imefanikiwa kwuasajili Diogo Jota na Thiago Alcantara. Usajili wa nyota hao ulikuja baada ya mchezo wa kwanza wa Ligi dhidi ya
Leeds United. Kengele ya hatari ilishalia. Klopp alishasikia kengele hiyo ndiyo maana haraka alimsjaili nyota huyo wa Bayern Munich kama mbadala wa mbinu zinazoweza kutumia kwenye mechi mbalimbali na kuibuka na ushindi.
MIAKA 10 YA UJENZI
Baada ya miaka 10 ya kujenga upya klabu ya Liverpool, imevunja mwiko uliodumu kwa miaka 30 ya kuishi bila kutwaa ubingwa wa EPL. Makocha mbalimbali wamepita klabu hapo hapo, akina Kenny Dalglish, Graham Souness, Brendan Rogers, Rafael Benitez na wengineo. Lakini ni Jurgen Klopp pekee amefanikiwa kuandika rekodi ya kipekee baada ya kutwaa mataji mawili ya EPL na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Chini ya umiliki wa John Henry, Liverpool imekuwa ikijaribu kujitutumua, mara nyingi ilikosa ubingwa katika mazingira ya kustajabisha. Klopp pekee amebdili masiaha ya mashabiki na viongozi wa Liverpool na kuwafanya waamini inawezekana. Ndoto za John Hnery zimekuja kutimia zaidi katika kipindi cha ukocha wa Jurgen Klopp kwa sababu ndiye alileta soka la aina yake, maarufu kama Gegen Pressing. Mjerumani huyo ametumia miaka minne kujenga kikosi imara Liverpool na kuwaibua nyota wakali wanaotisha katika soka la Ulaya, Mohammed Salah, Sadio Mane, Roberto Firmino na nyota wengine kama Van Diyk, Fabinho, Trent Alexander Arnold. Kwahiyo miaka 6 ya kukosa ubingwa kwa mmiliki John Henry, na kumpa miaka minne Jurgen Klopp kujenga Liverpool tishio si England pekee bali barani Ulaya ni matunda ya kazi nzuri na uvumilivu wa hali ya juu. Si jambo rahisi kwa wamiliki kukaa miaka 10 bila ubingwa au miaka minne kumvumilia kocha mmoja.
NDOTO ZA KUWASHIKA MAN UNITED
Kwenye kipindi cha miaka minne ya Jurgen Klopp ametwaa taji moja la Ulaya na Ligi Kuu moja. Mataji mengine ni kama lile la dunia pamoja na Super Cup.
Kihistoria Man United wametwaa mataji 20 ya Ligi Kuu England ikiwa ni moja mbele zaidi ya Liverpool. Kwa kipindi cha miaka 30 ambayo Liverpool walikuwa wamedorora, Man United walitawala EPL.
Nje ya hapo walimenyana na Chelsea na Arsenal kupigania ubingwa wa EPL. Wakati Liverpool wana ndoto ya kutwaa taji la 20 la EPL, wenzao Man United wanahangaika ili kurudisha makali yao, huku kocha wao Ole Gunnar Solskjaer akiwa anaungwa mkono licha ya matokeo mbaya.
Hapo ndipo ilipo changamoto ya Liverpool kama kweli wataweza kukimbia mbio ndefu ya Ligi Kuu na kuweza kutwaa taji la 20, ikiwa watakwepa vipigo kama walichokipata Villa Park.
Majukumu hayo mawili ya kuwawafikia Man United ambao ndio wapinzani wao wa jadi, pamoja na kutetea ubingwa ni mambo ambao yanawapa uzito mkubwa. Wanahitaji utulivu ambao utakifaya kikosi kifanye kazi yake kwa ufanisi zaidi.
KILICHOTOKEA VILLA PARK
Mchezo wa wikiendi kati ya Aston Volla na Liverpool umefungua zaidi tatizo alilioona kocha wa Leeds United, Marcelo Bielsa maarufu kama El Locco na mpira wake wa Bielsa Ball. Kwenye mchezo wa ufunguzi Liverpool walisubiri hadi dakika za lala salama kuhakikisha wanaibuka na ushindi. Lakini namna timu yao inavyocheza na mbinu mpya ya Klopp kutaka kucheza na viungo zaidi bila mabeki wote wa kati ni jambo lingine linalodhoofisha timu hiyo.
Kwenye mchezo dhidi ya Astn Villa, Klopp alibanwa eneo la kiungo. Kwenye mstari wa katikati ya uwanja palikuwa na viungo watatu wa Astrin Villa ambao kazi yao ilikuw akupokonya mipira na kucheza mashambulizi ya kushtukiza.
Kwa vile kiungi wa ulinzialikuwa mmmoja, Fabinho ilikuwa rahisi kumkwepa Nabil Keita na kumfanya Fabinho arudi nyuma zaidi. hali ambayo ililazimu beki nambari nne Joe Gomez apande kumsaidia Fabinho na kutengeneza pengo katio ya ulinzi na kiungo.
Villa walisambaratisha eneo la katikati ya Liverpool. Villa hawakuwa na mpango wa kuwadhibiti mabeki wa Liverpool wa pembeni ambao ni hatari, badala yake Ross Barkley na Grealish walikuwa silaha ya kucheza mashambulizi ya kushtukiza.
Hii ina maana Klopp ni lazima abadili mbinu kwa kuhakikisha ene la kiungo wa ulinzi linakuwa na viungo wenye jukumu hilo endapo anamkosa nyota mmoja wapo kati ya Mane,Firmino na Salah.
Villa hawakuwa na maajabu zaidi ya Counter Attacks. Hawakuwa na skills za kuwayumbisha Liverpool isipokuwa ‘game plan’ ilikuwa kuwavuruga Liverpool kwa makosa yao ya kimbinu ndio maana mabao mengi yamefungwa kutokana na makosa ya mabeki ambao mara nyingi waligongwa mipira kabla ya kutua kimyani. Je, bila kubaidli mbinu, Liveerpool wataweza kutetea ubingwa wao? Hilo ndilo swali.
Muda utaongea.
Comments
Loading…