in , , ,

Ivo Mapunda aivua ubingwa Uganda….

Ivo Mapunda ameivua ubingwa Uganda na kuiingiza Stars nusu fainali ya kombe la chalenji ambapo sasa itacheza na Kenya.

Kenya walishinda katika robo fainali nyingine dhidi Rwanda iliyochezwa leo jioni kwenye Uwanja huohuo wa Manispaa unaobeba mashabiki 15000,  kwa kuwafunga Rwanda goli 1:0. Uganda iliutwaa ubingwa huo mwaka jana mjini Kampala ikiwa haijafungwa bao hata moja kwenye mechi zake zote, Uganda ilikuwa inaelekea kutimiza rekodi hiyo lakini jana Stars ikatibua mambo. Awali kwenye mechi za makundi Uganda ilikuwa haijaruhusu bao lolote.

Mapunda anayeichezea Gor mahia ya Kenya alipangua penalti tatu za Uganda ambayo kocha wake, Sredejovic Milutin ‘Micho’ alijitetea kwamba penalti hazina ufundi na wala Stars haijafanya cha ajabu.; “Hakuna cha ajabu kwenye penalti hakuna fundi.”

Licha ya mwamuzi kutoka Somalia , Wish Wabarow kuonekana kuzidiwa na mchezo, mechi hiyo ilimalizika kipindi cha kwanza Stars ikiongoza mabao 2-1 huku ikishangiliwa na Uwanja mzima uliokuwa umetawaliwa na wakenya na Watanzania walioingia kupitia Lungalunga, Tanga.

Mshambuliaji wa Uganda, Danny Serunkuma ndiye aliyefunga bao la kwanza dakika ya 16 akipiga shuti kali katikati ya mabeki wa Stars lakini dakika mbili baadae Mrisho Ngassa alisawazisha kwa shuti kali kutoka nje kidogo ya mstatili, likamshinda kipa Benjamin Ochan.

Ngassa huyo huyo akapiga bao la pili kwenye eneo pacha dakika ya 38. Mchezo huo uligubikwa na aibu ya aina yake kutokana na kutokuwepo kwa wasaidizi wa msalaba mwekundu kwa kile kilichodaiwa kwamba hawajalipwa chao na Cecafa.

Timu hizo zilishambuliana kwa kasi kipindi cha kwanza ambapo mastraika Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu waliipa shida Uganda ambayo kwa siku ya jana straika wake, Danny Serunkuma ndiye aliyeisumbua zaidi Stars.

Kipindi cha pili dakika 52 Aboubakar Salum ‘Sure boy’ ambaye alikuwa akichezesha timu, alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga beki wa kushoto wa Uganda, Godfrey Walusimbi.

Ulimwengu na Samatta walipiga mashuti kadhaa langoni mwa Uganda ingawa jana haikuwa bahati yao, lakini katika hali ya kujiamini Ulimwengu alisogea kwenye mstari wa pembeni na kuliambia benchi la ufundi lisifanya mabadiliko ya haraka licha ya kwamba Stars walikuwa pungufu.

Dakika ya 75 beki mrefu wa Uganda alifunga bao laini baada ya Ivo kuutema mpira wa krosi ya Wakiro Wadada. Kim Poulsen alimuingiza Athuman Idd kumiliki kiungo huku akimtoa Mrisho Ngassa ambaye katika mechi dhidi ya Burundi alitoa krosi ya goli kwa Samatta.

Baada ya kumalizika kwa dakika 90 zilipigwa penalti ambapo Uganda ilikosa tatu na Stars ikakosa mbili. Penalti za Stars zilipigwa na Erasto Nyoni na Mbwana Samatta(walikosa), Amri Kiemba, Athuman Idd na Kelvin Yondani. Uganda walipiga Danny Walusimbi(alikosa),Emanuel Okwi, Aucho Khalid (alikosa),Hamis Kiiza na Serunkuma aliyekosa penati ya mwisho na kuivusha Stars.

Ivo Mapunda ambaye alikuwa akishangiliwa na mashabiki wengi wa Kenya alisema; “Siamini kwamba tumeshinda, ni mungu tu. Mpira ulikuwa mgumu sana na tulicheza na timu ngumu ambayo tumeitoa kwa juhudi binafsi za wachezaji.”

Stars ilipangwa hivi; Mapunda,Michael Aidani, Erasto Nyoni, Said Morad, Kelvin Yondani, Sure Boy,Mrisho Ngassa/Athuman Idd, Frank Domayo,Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba.

Uganda; Benjamin Ochan, Wakiro Wadada, Walusimbi, Kasaga Richard, Martin Mpuga, Aucho Khalid, Hamis Kiiza, Mpande Joseph, Kizito Godfrey, Okwi na Serumkuma.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Makundi Kombe la Dunia hadharani

Man United gonjwa?