in , , ,

HIKI NDICHO KINACHOISIBU MANCHESTER UNITED.

Jana Manchester United walitoa sare katika uwanja wake wa nyumbani ,
ikiwa ni mwendelezo wa matokeo mabaya katika mechi tatu zilizopita.

Kipi ambacho kinaisibu Manchester United kipindi hiki ?

1: Wachezaji wa kuipa ushindi timu katika mazingira magumu ( match winner).

Kuna wakati Paul Pogba alikosekana katika mechi kadhaa timu ilikosa
ubunifu wa kutengeneza nafasi nyingi za magoli kule mbele.

Paul Pogba karudi tena, timu inatengeneza nafasi nyingi, ila kitu
ambacho kinakosekana ni mtu ambaye ana uwezo wa kuibeba timu katika
mazingira magumu.

Kutengeneza nafasi nyingi peke yake hakutoshi, kunahitajika mtu ambaye
anauwezo mkubwa wa kuzibadilisha hizo nafasi kuwa magoli.

Kunahitajika mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa kuibeba timu kwenye
kipindi ambacho timu ikiwa na mazingira magumu. Mfano mtu kama
Antoinne Grienzmann.

2: Jose Mourinho anahitaji beki mpya wa kati.

Ni kweli timu ni ngumu, inajilinda vizuri na ina ukuta unaotia
matumaini sana, lakini huwezi kushinda taji lolote kama mabeki wako wa
kati wa kikosi cha kwanza wakiwa wanakabiriwa na majeraha ya kila
mara.

Phil Jones na Eric Baily wamekuwa wakikabiliwa majeraha kila mara huku
wakiwa ndiyo mabeki tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho.

Victor, Smalling, Rojo wamekuwa wakitumika kama mbadala wa kina Baily
na Jones lakini siyo imara ukilinganisha nao.

3: Manchester United inakosa viongozi wengi kwenye timu.

Mechi dhidi ya Bristol City , Jose Mourinho alilalamika kuwa wachezaji
wake wamejaa utoto ndiyo kisa cha wao kukosa ushindi.

Nafasi nyingi za wazi kina Lingard, Martial na Rashford walizikosa.

Hili linasababishwa na nini ?

Hapa jibu ni jepesi tu, hakuna kiongozi wengi wa kuwaongoza hawa
kufikia hatua ya ukomavu.

Hakuna wa kuwafanya wajione wakomavu uwanjani na kuwakemea kipindi
ambacho wanapofanya makosa ya kitoto.

4: Beki namba tatu
Ashley Young ndiyo beki anayetegemewa kwa sasa kwenye kikosi cha
kwanza kama beki namba tatu.

Umri umesonga, miaka 32 kwa sasa hali ambayo inatia ugumu kwake yeye
kutimiza majukumu yote katika ufanisi mkubwa.

Luke Shaw ambaye ni kijana mwenye miaka 22, majeraha yanamwandama kila
siku na kila akitoka katika majeraha amekuwa akichukua muda mrefu
kurudi kwenye kiwango chake.

Hakuna mbadala sahihi wa Ashley Young, na hakuna mtu sahihi katika
upande wa kushoto ambaye anaweza kukidhi mahitaji ya beki namba tatu.

Ni wakati sahihi kwa Jose Mourinho kuingia sokoni na kuanza
kuwapigania kina Danny Rose au Alex Sandro wa Juventus

5: Mchezaji mchezeshaji ( playmaker).

Henrink Mickhtaryian amekuwa na kiwango cha kupanda na kushuka, hana
mwendelezo mzuri wa kiwango chake.

Kwa hiyo nani wa kumsaidia pindi ambapo kiwango chake kitakapokuwa kimeporomoka?

Juan Mata? Inaweza ikawa chaguo sahihi lakini likawa chaguo ambalo
siyo bora kwa sababu na yeye pia ana matatizo kama ya Henrink .

Hivo kuna hitajika kiungo mchezeshaji ambaye anauwezo wa kulinda
mwendelezo wa kiwango chake kwa asilimia kubwa.

6: Mbadilishano wa majukumu.

Kuna kitu ambacho Jose Mourinho naamini anajifunza kwa Pep Guardiola.

Manchester City imekuwa timu ambayo wachezaji wake wamekuwa
wakisaidizana majukumu kitimu.

Pamoja na kwamba hakuna mchezaji wa Manchester City anayeongoza
ufungaji wa magoli mengi lakini timu ina idadi kubwa ya magoli.

Timu imefunga magoli mengi, magoli ambayo yametokana na idadi kubwa ya
wachezaji wa Manchester City kufunga.

Hiki kitu hakipo kwa Jose Mourinho.

Pep amekuwa akiwabadilisha vizuri Gabriel Jesus na Kun Aguero. Na kila
anapowabadilisha wamekuwa wakifanya vizuri.

Manchester United ina Zlatan na Lukaku.

Watu ambao kama ukiamua kuwafanyia mabadilishano mazuri wanaweza
wakaisaidia timu kwa kiasi kikubwa kuliko kuwachezesha pamoja.

7: Jose Mourinho anatakiwa awe mpya.

Anavyocheza na timu kubwa, Jose ni yule yule wa mwaka 2004,
hajabadirika , timu inacheza kwa kujihami sana hata kipindi ambacho
timu haiitaji kujihami.

Kuwa bingwa huitaji kujihami zaidi kwa asilimia kubwa kuliko kushambulia.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

UCHAMBUZI WA MECHI MBALIMBALI WEEKEND HII

Tanzania Sports

JINSI AMBAVYO LIVERPOOL WATANUFAIKA NA: Virgil van Dijk