in , ,

Hatimaye Tanzania yaweka rekodi mpya Yalinyakua Kombe la Dunia Kwa Watoto wa Mitaani 2014 Rio de Janeiro

Timu ya Taifa Ya Tanzania kwa Watoto wa Mitaani hatimaye Yanyakua Kombe la Dunia Kwa Watoto wa Mitaani, (Street Child World Cup 2014) Rio de Janeiro, Brazil

Ikitinga fainali za Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani kwa mara ya pili mfululizo, hatimaye Tanzania imeweza kutwaa Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani kama linavyojulikana Street Child World Cup hapa Rio de Janeiro.

Tanzania leo imeweza kuchachanya Burundi iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kulinyakua Kombe hili kwa Kuinyuka magoli 3 kwa moja huku mchezaji kiungo mshambuliaji wa Tanzania Frank William akipiga magoli matatu na kuwa nyota wa mchezo, Tanzania iliweza kufunga magoli mawili kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuongeza goli latatu kipindi cha pili. Burundi iliweza kufunga goli lake la pekee zikiwa zimebaki daika nne mpira kuisha.

Tanzania imeweza kufika fainali baadaya kuonyesha kiwango cha juu hata kuzishinda timu ngumu kama Burundi, Marekani, Indonesia, Nicarague, Ufilipino na Argentina.

Golikipa wa Tanzania Emmanuel ameweza kuchaguliwa kuwa golikipa bowa wa michuano hii ya kombe la dunia. Ikumbukwe kuwa fainali zilizopita za michuano hii Kule Durban Afrika Kusini Tanzania ilifika fainali na kufungwa na India.

Timu ya Tanzania itaondoka Brazil kesho Jioni ikipitia Dubai na kuwasili Dar es salaam siku ya tarehe 10 kwa Shirika la Ndege la Emirates.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Yanga wawasha moto

Kocha pekee mweusi EPL afukuzwa