Miaka sitini na mbili iliyopita alizaliwa shujaa wa kufukuza upepo tena chini ya mlima Hanang huko Katesh mkoani Manyara, makubwa aliyowahi kuyafanya ndio sababu tosha kabisa tovuti hii imefunga safari kupata historia yake.
Gidamis Shahanga moja ya jina kubwa sana hapa Tanzania tena ukizungunzia riadha huwezi kuacha kutaja jina lake, kwa ubora na uwezo wake kwa wakati huo.
Ni mshindi pekee wa medali ya mbili kutoka katika mashindano ya ‘Commonwealth games’ yaani mwaka 1978 marathoni na 1982 Mita 10,000.
Hii hapa historia yake kwa ufupi alipozaliwa na maisha mengine na ameupataje umaarufu kupitia riadha.
Shahanga amezaliwa September, 1957 huko Hanang, Kateshi Tanzania ikiwa yeye na mdogo wake Humphrey Shahanga ndio wanariadhaa pekee katika familia yao huku kukiwa na ongezeko la mtoto wa dada yake anayeitwa Emanuel Geniki.
Ana elimu ya juu kabisa ambapo shule ya msingi amesoma huko Katesh na sekondari alifanikiwa kusoma Mazengo huko Dodoma, historia ya riadha imeanzia akiwa shule ya sekondari ndipo alipojumuishwa katika timu ya taifa ya riadha ambapo shindano lake la kwanza alikuwa mtu wasaba.
Katika elimu hakuwa nyuma kwani chuo alisoma huko Marekani alichukua degree japo kazi kubwa alitumia miguu yake kuweza kutengeneza maisha yake sio elimu aliyoipata. Hii inamaanisha kuwa unaweza kusoma ila maisha yako yapo upande mwingine.
Juan Mata wa Manchester United ni mwandishi wa habari aliye na bachela yake lakini mpira ni sehemu yake inayompa ajira.
Hakuweza kutaja watoto idadi ya watoto lakini alisema kuwa hakuna aliyefuata nyayo zake za kufukuza upepo, ndani ya riadha alikuwa anakimbia mita 10,000 ambazo zimempa umaarufu huko chini tutakupatia idadi zake za ushindi.
Katika miaka yote hiyo tangu aingie katika mchezo wa riadha jina lake limeanza kupaa katika masikio ya Watanzania na dunia kumsikia kijana mwenye miaka 21 akishinda mbio mbio ndefu za riadha mwaka 1978 huko Edmonton, Canada alikimbia kwa saa 2:15:40.
Baada ya ushindi huu alipata kupokelewa kwa shangwe sana huko shuleni kwake Mazengo mkoani Dodoma, shule za msingi na sekondari waliruhusu kumpokea kwa mayowe ya furaha.
Shahanga alikuwa mwanariadha aliyekimbia kwa wastani mzuri tena kwa mita 10,000 na mbio za kawaida.
Mwaka 1982 katika mashindano ya jumuiya madola ‘Commonwealth Games’ aliibuka mshindi wa kwanza huko Brisbane, Australia mita 10,000 kwa kutumia dakika 28:10:15.
Wakati historia zinaendelea mwaka 1984 aliibuka tena mshindi wa kwanza Los Angeles Marathon alitumia saa 2:10:19, Marekani na Rotterdam Marathon, Uholanzi 2:11:12.
Ilipofika mwaka 1990 alienda tena kufanya maajabu huko Vienna, Austria kwa kushinda tena namba moja alitumia muda wa saa 2:09:28.
Mwak 1990 huko Munich, Ujerumani aliibuka na ushindi katika mbio ndefu alitumia muda wa saa 2:14:28.
Ushindi wake wa mwisho ilikuwa mwaka 1993 huko Munich, Ujerumani kwa kutumia saa 2:17:27.
Nilipo muuliza ugumu gani alioupata wakati anakimbia riadha alisema kuwa baridi sana au joto sana wakati anakimbia lilimpa wakati mgumu katika kufanikiwa, alisema ili ufanikiwe lazima uwe na njaa ya kuhitaji kitu.
Amesema kuwa njia pekee iliyompaa nguvu kuwa na nidhamu katika mchezo huo na aliokuwa akikimbia anapunzika kidogo kisha anaenda katika mbio nyingine.
“Nilikuwa nikimbia marathon moja narudi nyuma nabadilisha nyingine kisha narudia tena,”alisema.
Nilikuwa Napata mualiko mara kwa mara ila nilikuwa nachagua maana huwezi kukimbia mara kwa mara na hiyo ndio imenipa ubora,”alsiema.
Tulipo muuliza juua ya waliofuata nyanyo amesema mtoto wa dada yake Emanuel Geniki ni moja ya familia yake.
Tatizo kubwa la kutofanya vizuri kwa upande wake amesema kuwa huenda wanariadha wanaojitokeza hawana ubora unaohitajika kwakuwa wanaona kuna fursa wanajipenyeza na kuingia katika mchezo, hivyo ameeleza kuwa kwa maelezo zaidi tuwatafute wanaosimamia mchezo huo.
“Huenda wanariadha wanaojitokeza hawana ubora unaohitaika, wanajitokeza kwakuwa huku kuna fursa, hivyo inatakiwa wapatikane watu sahihi ili wawakilishe mchezo huu,”alisema.
Rekodi hii nimeitoa ile aliyowahi kushika nafasi ya kwanza bado kuna nyingine alikuwa nafasi ya pili hadi ya tatu, sio wastani mbaya ila mimi nimechagua alizoshinda nafasi ya awali.
Hii hapa orodha ya ushindi wake kwa pamoja:-
1. Mwaka 1978- Commonwealth games huko Edmonton, Canada saa 2:15:40. Brisbane, Australia.
2. 1982- mashindano hayo hayo ila sasa yalifanyika Brisbane, Australia alitumia saa 28:10:15 ilikuwa mita elfu kumi, ni medali pekee kutoka katika mashindano hayo alipata Mtanzania huyo.
3. 1984- Huko Los Angeles Marekani alitumia saa 2:10:19.
4- Mwaka 1990 aliibuka tena mshindi mara mbili na mwisho kabisa ilikuwa mwaka 1993 huko Munich, Ujerumani.
Comments
Loading…