in , , ,

FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA


Ushindani wa makundi unanoga

TIMU ya Taifa ya England ni moja ya waliofanya vyema hadi sasa kwenye fainali za Kombe la Dunia, hatua ya makundi na wameshafuzu kuingia 16 bora.

Walianza kwa ushindi mwembamba dhidi ya Tunisia kabla ya kuwakung’uta Panama 6-1 Jumapili hii, wakiwa chini ya kocha Gareth Southgate.

Huyu anataka kuwa tofauti na watangulizi wake, Sam Allardyce na Roy Hodgson na lengo ni kurejesha heshima ya England iliyopotea muda mrefu uliopita, ambapo wakivuka sana kwenye mashindano makubwa wamekuwa wakiishia hatua ya robo fainali.

Euro 2016 nchini Ufaransa ilikuwa aibu kwao, wakitolewa mapema na Iceland, ndipo Hodgson akaachia ngazi na kupewa Allardyce aliyeondoka baada ya kashfa ya kwenda kinyume na maadili ya uongozi.

Southgate ni chaguo ambalo halikutarajiwa, lakini FA wamekuwa wanataka sasa kuwa na kocha mzawa, wakiamini wanao wa kutosha na ni heshima pia kwa taifa hili kubwa kisoka. Bado ni vigumu kuona iwapo England watafika mbali, kwani timu walizocheza nazo hadi sasa si kali, japo kidogo Tunisia waliwatisha.

Panama ndiyo mara ya kwanza wanaingia na kwa hakika si ajabu kusema wanaweza kufungwa na timu yoyote ile. Pengine kipimo kizuri kingekuwa dhidi ya Ubelgiji, hasa kabla ya kufuzu kwao, maana wanapochea kukamilisha ratiba inawezekana wasikamiane sana, japokuwa kila mmoja angetaka kuwa wa kwanza kwenye kundi lake, ili akabiliane na wa pili kwenye jingine.

Wanao wachezaji wazuri na safari hii kiongozi wao kama nahodha na pia kwenye upachikaji mabao ni Harry Kane wa Tottenham Hotspur. Kutakuwapo msisimko wa kujua watakabiliana na nani kwenye hatua ijayo, na zaidi sana kushuhudia mechi yenyewe wakati huu ambapo vigogo wametikiswa, wakiwamo Ujerumani na Argentina.

Katika kundi A tayari Urusi na Uruguay wamefuzu, wakiwatupa mbali Misri na Saudi Arabia. Kundi B wanachuana Hispania na Ureno wenye alama nnne kila mmoja na Iran wenye tatu huku Morocco wakiwa wameondoshwa.

Kundi C Ufaransa wamevuka wakishinda mechi zao mbili, Denmark wana alama nne wakati Australia wakiwa na moja na Peru hawana chochote na wametoka. Kundi D Croatia wamejihakikishia, Nigeria wakiwa na alama tatu huku Iceland na Argentina wakiwa na alama moja kila mmoja. Kundi E kuna mvutano, Brazil na Uswisi wakiwa na alama nne nne huku Serbia wakitafuta bado wakiwa nazo tatu na Costa Rica wameshatolewa wakibaki bila alama.

Katika Kundi F, Mexico wamevuka kwa ushindi wa mara mbili, Ujertumani na Sweden wanahangaika wakiwa na alama tatu kila mmoja wakati Korea Kusini wamefurushwa.

Kundi G ndilo la England waliovuka na Ubelgiji huku Tunisia na Panama wakitumwa nyumbani. Kundi la mwisho la H ni kwamba kuna mvutano wa timu tatu – Japan na Senegal wenye alama nne kila mmoja huku Colombia wakiwa nazo tatu na Poland wameaga. Mechi za mwisho zitapendekeza kutazama.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

LINI MPIRA UTAWATENDEA HAKI KINA MODRIC NA KROOS

Tanzania Sports

‘Messi ana msongo wa mawazo’