in , , ,

LINI MPIRA UTAWATENDEA HAKI KINA MODRIC NA KROOS

Miaka kumi (10) imepita, miaka ambayo imekuwa na ushindani wa watu wawili tu katika dunia hii ya mpira wa miguu.

Dunia ambayo haikutenda haki kwa Andres Iniesta. Kiungo ambaye aliweza kutuonesha mpira unahitaji akili nyingi kuliko nguvu, kiungo ambaye alipata mashabiki wengi hata wale ambao walikuwa wakimkaba ndani ya uwanja.

Kiungo ambaye alikuwa na uwezo wa kushinda Ballon D’or katika miaka yake yote ambayo aliwahi kucheza, lakini historia yake inaenda kumalizika na neno la kuhuzunisha kuwa hajawahi kushinda ballon d’or.

Mwisho wa hadithi yake unatia huruma, unatia simanzi na unaonesha uonevu mkubwa juu ya kipaji hiki ambacho kiliwahi kuufanya mpira uonekane kama unasikiliza gitaa la Carlos Santana.

Burudani ilikuwa katika miguu ya Andres Iniesta, hakuchosha kumwangalia na kila muda jicho lilitamani kumuona.

Alinoga zaidi kipindi ambacho alikuwa anacheza na pacha wake kutoka baba na mama tofauti ( Xavi). Mchezaji mwingine anayeichukia haki duniani kwa sababu haikuwahi kutumika kipindi ambacho aliwahi kuutumikia mpira.

Alistahili kustaafu na tunzo ya ballon d’or lakini haki haikutumika katika maisha yake ya soka na hii ni kwa sababu alicheza mpira kipindi ambacho Cristiano Ronaldo na Lionel Messi walikuwa wameshaanza kucheza mpira.

Hapa ndipo ugumu wa yeye kupata tunzo hii ulipoanzia, ndipo ugumu wa Frank Ribery pia kupata tunzo hii ulipozaliwa. Kipindi ambacho alionekana kustahili kupata tunzo hii ndicho kipindi ambacho Cristiano Ronaldo na Lionel Messi walikuwepo katika uso wa dunia.

Walichukiza kwa sababu kuna wakati walikuwa wanapewa heshima ambayo wengine walionekana wanastahili, heshima ambayo Wesley Sneijder alionekana kustahili mwaka 2010 lakini ikapokwa.

Dunia ililalama sana, ikaumia na upande mwingine wa dunia ulilia sana lakini hakukuwepo na kitu kingine cha kufanya kwa sababu karatasi zilikuwa zimeshamwandika Wesley Sneijder kama mtu ambaye aliyeshindwa.

Hii ni kwa sababu mbele yake alikuwepo Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Wachezaji ambao wameigawa dunia katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza inaitwa Cristiano Ronaldo na dunia ya pili inaitwa Lionel Messi. Dunia ambazo zimetawala sayari hii ya mpira.

Wamegawana tunzo za ballon d’or katikati ndani ya miaka kumi iliyopita. Miaka kumi ambayo ilikuwa michungu kwa wachezaji wengine ambao walionekana wanastahili kubeba ballon d’or.

Tuliumia kwa kina Andres Iniesta, Xavi, Wesley Sneijder na Frank Ribery walipokosa ballon d’or kisa uwepo wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Nyakati hizi tunatakiwa tujiandae na maumivu ya kushuhudia Luka Modric na Toni Kroos wakikosa ballon d’or katika maisha yao ya soka.

Wachezaji ambao ni mhimili mkubwa katika timu zao wanazocheza lakini cha kuumizwa ni kuwa wanacheza kipindi ambacho Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wako hai na kibaya zaidi bado wapo wanavaa jezi kuzitumikia timu zao.

Kipindi hiki ni kipindi ambacho Luka Modric na Toni Kroos wanatakiwa kupewa heshima kutokana na kitu ambacho wanakitumikia kwa kiwango kikubwa.

Modric

Kabla ya kumsifia Cristiano Ronaldo unatakiwa uangalie ni kina nani ambao ni muhimili wa timu ya Real Madrid.

Wao ndiyo roho ya timu, hawafungi sana magoli ila wanaifanya timu ya Real Madrid ifunge sana.

Wao ndiyo wanaoamua ni namna gani ambavyo timu inatakiwa icheze. Ni namna gani ambavyo timu inatakiwa kushambulia kupitia maeneo gani.

Wao ndiyo wanafungua ya mashambulizi ya timu ya RealMadrid hata kwenye timu zao za taiga wao ndiyo roho ya timu zao.

Hakuna kitu kibaya kinachotumika kwenye ballon d’or kama kumwangalia mtu ambaye anafunga sana na kuwasahau watu kama hawa ambao ni roho kubwa ya timu wanazocheza.

Huu ni wakati sahihi kwa mpira wa miguu kutoa heshima kwa watu aina ya Luka Modric na Toni Kroos.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

CHOZI LA MARADONA NI DENI KUBWA KWA MESSI

Tanzania Sports

FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA