in

FAIDA NA HASARA KAMA TIMU YA YANGA IKISHUSHWA DARAJA

Yanga

Aidha ndugu Mwakalebela akasema kwamba klabu yake inatishia kujitoa kwenye ligi kuu ya Tanzania bara.

Hivi karibuni kulisambaa clip za video za mwenyekiti wa Yanga ndugu Fredrick Mwakalebela akizungumzana wanahabari huku akitoa malalamiko yake dhidi ya shirikisho la mchezo wa soka Tanzania (TFF), bodi ya ligi kuu, kamati ya waamuzi wa ligi kuu Tanzania na kamati ya waamuzi, kamati ya saa 72. Hii ilikuwa ni baada ya kutoka sare mfululizo katika mechi za ligi kuu Tanzania. Sare ya kwanza ilikuwa ni na timu ya Mbeya City ambayo ilikuwa ni ya kufungana bao moja kwa moja na sare ya pili ilikuwa ni baada ya kufungana mabao matatu kwa matatu na timu ya Kagera Sugar. Katika madai yake alidai kwamba katika mchezo wa Mbeya city walikoseshwa kupewa penati mbili za wazi. Aidha ndugu Mwakalebela akasema kwamba klabu yake inatishia kujitoa kwenye ligi kuu ya Tanzania bara. Kwa kauli hiyo kama wataitekeleza basi ina maana timu ya yanga itashuka daraja na kutoka kwenye ligi kuu na kasha kwenda madaraja ya chini.

Watu wengi wanadai hilo litakuwa tukio la ajabu katika soka kuliko lote mi nasema kwamba sio la ajabu ngoja nitoe mifano ya baadhi ya matukio ya ajabu yaliyowahi kutokea:

Tukio la kwanza ninalolikumbuka lilikuwa mnamo mwaka 1990 katika kombe la dunia timu ya taifa ya Cameroon ilishangaza ulimwengu kwa kuifunga timu ya taifa ya Argentina. Katika mechi hiyo timu ya taifa ya Argentina ilikuwa na wababe wa soka kama vile Diego Maradona, Claudio Caniggia na wengineo wengi ila ilishangazwa na kufungwa na timu ndogo ambayo haikuwa na hata staa mmoja.

Tukio la pili lilikuwa mnamo Mwaka 2004 timu ya taifa ya Ureno ilishangaza dunia kwa kufungwa na timu ndogo ya Ugiriki katika michuano ya Euro timu hiyo ya Ureno ilikuwa imesheheni vipaji lukuki kama vile Luis FIgo, Christiano Ronaldo, Ricardo Quaresma na wegineo ilijikuta inatolewa katika mashindano hayo na timu ndogo ambayo haikuwa na mastaa hata kidogo.

Na je kama kushushwa kwao daraja kutakuwa ni jambo geni  katika ulimwengu wa sasa. La hasha! Haitakuwa ni jambo geni katika ulimwengu wa soka la kisasa. Mfano mzuri ni Katika msimu wa mwaka 2006- 2007 timu ya Juventus ya Italia ilishushwa daraja na chama cha soka cha Italia baada ya kubainika kukutwa na kashfa ya kupanga matokeo na kwenda kwenye daraja la Serie B katika ligi kuu ya Italia. Juventus ilijipanga upya katika daraja la chini na msimu uliofuata ilifanikiwa kurudi katika daraja lake la Seria A na tokeo iliporudi imekuwa na mafanikio makubwa sana.

Tukirudi katika msingi wa mada tuangalie baadhi ya hasara ambazo zitakozokosekana kwa mda baada ya yanga kujitoa kwenye ligi kuu

Mosi, ushindani utapungua kwa mda katika ligi kuu ya Tanzania. Hakuna ubishi kwamba vilabu vya samba na yanga ushindani wao kwa miaka mingi katika ligi kuu ya Tanzania umekuwa ni chachu kubwa ya ufuatiliaji wa maendeleo ya ligi kuu Tanzania. Mechi za timu hizi zimekuwa zinagusa hisia kubwa za timu nyingi na kama yanga itatoka basi ushindani utapungua kwa kiasi

Pili, mapato yatapungua kwa kiasi Fulani katika ligi kuu ya Tanzania. Halina shaka timu ya yanga uwepo wake katika ligi kuu unachangia kwa kiwango Fulani kwa mapato kwa timu ambazo huwa inakutana nazo na kama itashuka daraja basi itaathiri mapato kwa kiasi Fulani.

Tuangalie kwa namna Fulani faida ambazo zitapatikana kwa timu ya yanga kushuka daraj

Mosi kushuka kwao daraja kutachangia kuinua soka la chini hususani kwenye madaraja ya chini. Madaraja ya chini kwa mda mrefu ligi zake hazijakuwa na msisimko mkubwa na inatokana kwamba zimekosa uwepo wa timu kubwa kwenye madaraja hayo na imepelekea zimekosa washabiki wafuatiliaji wa ligi hizo kwa kiwango Fulani.

Pili kushuka kwao daraja kutachangia mapato kwa vilabu ambavyo vinashiriki ligi daraja za chini. Sio jambo la kushangaza kusema kwamba timu ambazo zipo katika madaraja ya chini hazina udhamini wa kutosha na kama timu ya yanga itashuka daraja basi hata wadhamini kwa ajili ya ligi ya madaraja ya chini watapatikana tu na watatoa udhamini wao.

Tatu itachochea ushindani katika ligi ya madaraja ya chini. Haina shaka kwamba kama timu za daraja la chini kwa kuwa timu ambazo zitatakiwa kupambana nazo zitajiandaa kwa nguvu kwa ajili ya kushindana na yanga. 

Kwa baadhi kushuka kwa yanga kutakuwa ni faida na kwa baadhi kutakuwa ni hasara ila kwa ujumla kutakuwa ni mabadiliko makubwa katika soka la Tanzania.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
man city

Ni ipi siri ya mafanikio ya Manchester City?

SIMBA SC

Simba wanatangaza β€˜utamu’ wa Ligi Kuu Tanzania