in , , , ,

Fadlu apasua Kichwa kwa Yanga

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids anasuka mipango ya kukabiliana na mahasimu wao – Yanga kwenye mechi ya Ngao ya Jamii itakayochezwa Jumanne hii.

Raia huyo wa Afrika Kusini amesema kwamba kikosi chake tayari kimeanza maandalizi kuiendea mechi hiyo ya kufungua msimu wa soka 2025/26 na hakusita kuweka wazi msimamo wake kuendea Dabi ya Dar es Salaam.

Simba ambao wametoka kumaliza ‘Simba Day’ wiki iliyopita watapenda kulipa kisasi kwa Yanga ambao kwa miaka ya karibuni wamekuwa wakiwafunga Simba, lakini anasema kuwa lazima sasa ifike mwisho.

Msakata kabumbu huyo mstaafu alibainisha kwamba walipumzika Ijumaa na sasa wanaanza kujiandaa na mechi aliyosema ni mtuhani usiokuwa wa kawaida, akifananisha mchezo huo na fainali, na zaidi sana ni mechi ya kurudisha heshima nyumbani Msimbazi.

“Tumemaliza mapunziko na leo (Jumamosi tunaanza maandalizi ya mechi dhidi ya Yanga. Huo ni mtihani mkubwa, ni fainali, ni mechi ya heshima,” alisema Fadlu aliyeonekana kujiamini.

 Baada ya hapo tutaelekeza nguvu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Tutafanya uchambuzi, mikutano binafsi na ya pamoja, ili kuweka mambo sawa,” alisema kocha.

Ratiba ya Simba imebana kwani ndani ya wiki hiyo hiyo watatakiwa kusafiri hadi Botswana watakakokaribishwa kwenye mechi dhidi ya Gaborone United.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa mashabiki kuendelea kutoa sapoti kubwa, akibainisha matarajio ya timu kupata kibali cha kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi za nyumbani ili mashabiki wengi waweze kushuhudia michezo yao.

Fadlu alielezea utimamu wa wachezaji wake na akataka washabiki wao pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wawaunge mkono, kwani wanaliwakilisha taifa, hivyo wanahitaji msaada pia wa kuruhusiwa kutumia dimba la Mkapa ili washabiki wao ambao ni weng wapate kuingia uwanjani, kuwaona na kuwashangilia.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Iko wapi nguzo ya kikosi cha Taifa Stars?

Tanzania Sports

Mwelekeo mpya wa Simba utimize hasira hizi