in , ,

EPL na mjadala wa wachezaji wa kigeni

Mbwana Samatta, Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Uingereza imejiondoa kwenye Umoja wa Ulaya (EU) rasmi na mjadala unaojengeka sasa ni juu ya idadi ya juu ya wachezaji wa kigeni wanaoweza kuwa katika kikosi cha klabu moja.
Baada ya kukamilika kujitoa huko, maarufu kama Brexit, sasa Chama cha Soka (FA) pengine na serikali huenda wakajielekeza katika kupunguza idadi ya wachezai wa kigeni wanaoweza ama kusajiliwa au kucheza kwenye mechi za Ligi Kuu ya England (EPL) – moja ya ligi maarufu zaidi Ulaya.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu, Richard Masters, anaonya kwamba kupunguza wachezaji kufikia chini ya 16 katika kikosi cha wachezaji 25 wa timu moja itakuwa na athari hasi kwa klabu za England kulinganisha na washindani wenzao wa Ulaya.

Mijadala inaendelea kati ya Ligi na FA juu ya jinsi ya kutengeneza vikosi, FA ikitaka kuona kwamba wanaondoa masharti magumu aliyopo sasa kwa wachezaji wanaotoka nje ya mataifa ya EU, ili mradi kwamba hakuna klabu inayosajili zaidi ya wachezaji 13 wa ng’ambo katika kikosi cha wachezaji 25.
Kwa sasa klabu zinaruhusiwa kusajili hadi wachezaji 17 kutoka ng’ambo huku bodi ya EPL ikitaka kubakia na idadi hiyo lakini kwa masharti kwamba ligi hiyo ichezeshe wachezaji Waingereza wenye vipaji na viwango vya juu vya soka sambamba na walio bora zaidi duniani.

“Ni suala la kusubiri kwamba suluhu ya mambo haya itakuwaje; bado hatujakaribia na kufikia makubaliano yoyote. Ingekuwa tuna mfumo na idadi hasa ya wachezaji tofauti na wengine Ulaya, basi klabu zetu kubwa hazitafaidika, maana nadhani kwamba wastani wa idadi yaw achezai wa kigeni wanaoweza kusajiliwa a ambao wanakuwa kwenye Ligi ya Mabingwa inaweza kuwa 16. Wakiwa pungufu si faida kwa klabu zetu,” anasema Masters.

Anaongeza kwamba maoni ya Bodi ya Ligi Kuu na klabu ni kwamba mfumo unafanya kazi na unatoa wachezaji wazuri wenye vipaji kutoka England kadhalika. Anasema hailaumu FA kwa nia yake ya kutaka uwazi zaidi na kuhakikisha hali hiyo inaendelezwa mbele.
“Kwa hayo tunakubaliana, lakini hatutaki kuingia kwenye hatari juu ya mfumo wa sasa. Hatutaki kuingia matatani na Ligi Kuu kwa sababu kimsingi sasa hivi kuna mafanikio,” ni maoni ya Masters.

Kuanzia Februari 7,wastani wa idadi ya wachezaji wanaofuzu kucheza England (EQPs) wanaoweza kuanza kwenye kikosi kwa msimu wa 2019/20 katika EPL ni asilimia 34.8, idadi ikiwa imeshuka kwa wastani wa 27.2 kwa klabu zile kubwa sita – Arsenal, Chelsea, Manchester City, Manchester United, Liverpool na Tottenham Hotspur. Hata hivyo, kwa ujumla idadi imeongezeka kwani msimu uliopita ilikuwa asilimia 30. Nyongeza hiyo imetokana zaidi na mchango wa Chelsea ambao umekuwa asilimia 20 hivi, ikitokana na kuwa kwenye zuio la kusajili hivyo kutumia chipukizi wake wa England.

Januari mwaka huu pia hawakusajili licha ya kuruhusiwa kufanya hivyo. Klabu mbili zilizopanda daraja – Aston Villa na Sheffield United nazo ziliongeza wastani kwa kuvuka asilimia 40.
Kocha wa Timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate, akichangia juu ya idadi ya wachezaji kwa masimu wa 2018/19 mnamo Mei mwaka jana, alisema kitu muhimu kinachotakiwa kufanywa ni kuhakikisha idadi ya Waingereza au waliokulia humu haishuki, kuhakikisha grafu haiendi chini zaidi.

“Hii ni kwa sababu si sahihi kudai kwamba hatujakuza wachezaji wazuri. Nadhani suala hili ni muhimu sana kwa hakika,” anasema Mwingereza huyo.
FA inaamini katika kutoa fursa kwa wachezaji wa kigeni kusajiliwa, lakini kuzuia ongezeko kubwa mno la idadi hiyo, kwani itakuwa kwa manufaa ya soka ya England. Klabu zitakuwa na dirisha moja zaidi la kusajili wachezaji chini ya mfumo wa sasa kabla ya kipindi cha mpito cha Brexit kumalizika Desemba 31 mwaka huu.

“Kimsingi suala hili lingetakiwa kupatiwa ufumbuzi kabla ya dirisha la usajili la kiangazi na hiyo itatoa fursa kwa klabu kujua kwa uhakika mfumo wa kanuni za Uhamiaji unakuwaje kwa ajili ya madirisha ya kuanzia Januari mwakani. Hiyo ingekuwa safi, lakini ilivyo si rahisi na itachukua muda zaidi na ni muhimu sana kuwa makini ili tusikosee; tuwe na muda maalumu,” anasema Masters.


Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Ole: Man United itawasha

Tanzania Sports

Dirisha la usajili kiangazi lasogezwa mbele