in , , ,

Di Maria aelekea PSG

*Man United wamsubiri Pedro

*Chicharito kuondoka United

 

Kiungo aliyevunja rekodi ya Uingereza kwa kusajiliwa na Manchester United kwa pauni milioni 59.7 msimu uliopita, Angel Di Maria anakamilisha hatua za kujiunga rasmi na Paris Saint-Germain (PSG).

 

Raia huyu wa Argentina amesema kwamba ana furaha kubwa kuondoka Old Trafford na kuingia PSG ambako alifanyiwa vipimo vya afya Jumanne hii baada ya klabu kulipa pauni milioni 44.3.

 

“Ninayo furaha kubwa kujiunga na Paris St-Germain. Ni klabu muhimu sana; walifika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita tofauti na ilivyokuwa nyuma. Nitajitahidi kufanya vyema kabisa kuwasaidia kwenye malengo yao na kufika fainali msimu huu,” akasema.

 

Di Maria, 27, alifanyiwa vipimo vya afya Doha, Qatar baada ya msimu uliokuwa si mzuri na United, ambapo alifunga mabao manne katika mechi 32, tofauti na msimu uliotanguliwa ambapo alikuwa tegemeo kwa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Argentina.

 

Kocha Louis van Gaal alimbadilisha namba, akimpanga sita tofauti ikiwa ni pamoja na kiungo cha kati na ushambuliaji lakini hakuweza kufanya vyema, ikiwa ni pamoja na kukumbwa na nyakati za majeraha kama mwezi mzima wa Desemba.

 

Zipo habari kwamba alikuwa na matatizo ya kisaikolojia kutokana na wezi kuvunja nyumba yake akiwa na familia, japokuwa walikimbia baada ya Di Maria kubonyeza king’ora. Alihamia hotelini baada ya tukio hilo.

 

Van Gaal  aliwalazimisha PSG kulipa pauni milioni tatu zaidi, baada ya mchezaji huyo kutundika picha kwenye mtandao akiwa na mmiliki wa klabu hiyo, Nasser Al-Khelaifi nchini Qatar.

 

Ili kuziba pengo lake, United wnaatarajia kumsajili mshambuliaji wa Barcelona, Pedro, 28. Van Gaal amemuahidi Pedro kwamba atacheza pamoja na Wayne Rooney na Memphis Depay kwenye eneo la ushambuliaji, ikiwa ni njia ya kumshawishi kukubali ofa.

 

Pedro angependa kuondoka Barca kwa sababu hapati nafasi ya kucheza, kwani wapo vyema wakiwa na Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez hivyo yeye kubaki benchi mara nyingi.

 

Wolfsburg wapo tayari kumuuza Kevin De Bruyne, 24, kwa Manchester City, lakini kwa masharti kwamba ada isiwe chini ya pauni milioni 50. West Ham wanatarajia kuongeza dau kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez ‘Chicharito’.

Zipo habari kwamba Chicharito binafsi anataka kuwaomba United kushusha bei wanayotaka kumuuzia ya pauni milioni 12 ili aondoke.

 

Tottenham Hotspur pia wanamtaka. Angependa kuondoka kwa sababu hana uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza na msimu uliopita alicheza Real Madrid.

 

Everton wana hofu ya kumpoteza mlinzi wao Mwingereza, John Stones, 21, kwa sababu Chelsea wanaendelea na shinikizo, huku wakisema wanakwenda na dau jipya la pauni milioni 30 baada ya lile la awali kukataliwa na Everton kusema hawamuuzi mchezaji huyo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

English Premier League 2015-2016 Kuanza

Usajili EPL wafikia £500m