in

Dewji Hakujibu swali la Uwekezaji

Mohamed Dewji

Huenda ikawa habari nyingine ngumu kwa Wanasimba ila ni vizuri kufahamu ukweli juu ya uwekezaji wa timu ya Simba ambao tumeambiwa zinawekwa bilioni 20.

Katika mchakato wa hisa na ndio utaratibu uliotolewa na serikali kuwa Wanachama wanachukua hisa asilimia 51 wakati wawekezaji/muwekezaji atachukua asilimia 49.

Baada ya hayo kufanyika kwa ustadi mkubwa jambo ambalo sio haliwezekani ila limekuwa gumu kutolewa majibu juu ya kuingizwa katika benki ya Simbi kiasi cha shilingi bilioni 20 zilizosemwa.

Licha ya kulitolea ufafanuzi mara kwa mara lakini bado halijibiwi ili swali hili lisiulizwe tena.

Ukweli ni kwamba tajiri namba moja kwa vijana Afrika Mohamed Dewji hashindwi kuweka kiasi cha bilioni 20 katika akaunti ya Simba lakini kipi kinafanya asijibu moja kwa moja?

Leo katika mahojiano na kituo cha Wasafi Tv aliulizwa juu ya hizo bilioni 20 ameziweka kweli ndani ya akaunti ya Simba majibu yake yamekuwa rahisi mno.

Huenda watu wakachukia hasa wakiona mazuri mengi anayoyafanya kisha kuzungunza β€˜Negetive juu ya swala hili.

Majibu yake yalikuwa kama ifuatavyo:-

β€œKwa mwenye akili timamu Mo anashindwa kulipa bilioni 20,” alihoji.

β€œSiwezi kuiacha Simba, mfano nimenunua kiwanda nimewekeza Simba kwa mwenye akili timamu nashindwa kuweka milioni 20, niwatoe hofu Simba,”aliongeza

Kauli hii inaoneshaa dhahiri kuwa hajajibu swali la msingi, ni kweli hakuna asiyeamini uwezo wa kifedha wa Mohamed Dewji pesa anayo na anaisaidia sana Simba kama ameweka kwanini asiwe muwazi tu kuwa ameweka.

Aliongeza kuwa anatoa zaidi ya bilioni 3 kila mwaka juu ya kuisaidia Simba sasa anashindwaje kuingiza milioni 20.

Kwa kuichambua hiyo bilioni tatu au zaidi ni kwamba inatumika kutoa mishahara kwa wachezaji, usajili na mambo mengine ya timu.

Hapo kila kitu kinaenda sawa kikubwa ambacho wengi wanahitaji kujua na wawekwe sawa hata kama anasaidia vyote au aliwahi kusaidia kwanini asiweke hizo 20.

MIKAKATI MIPYA YA SIMBA

Timu hiyo ina mipango mingi ya kimaendeleo tena ya msingi zaidi katika mahojiano hayo ambayo yalihudhuliwa na Diamond Platnumz na Haji Manara Mohamed Dewji alisema kuwa timu inaenda katika mfumo wa kidigitali zaidi.

Juu ya kuwalinda na kuwathamini wachezaji kuokoa vipaji vyao timu itanunua kifaa maalumu kitakacho wajenga wao wenyewe kujua namna anavyotumika uwanjani.

Yaani inapotokea mechi  kila mchezaji atafahamika ametumia nguvu kiasi gani pamoja na kujituma.

Hajaishia hapo hiko kifaa kitasaidia hata kujua muda wa kupunzika kwa wachezaji je amelala kwa muda gani pindi wanapoachiwa kutoka mazoezini.

Haya ni maendeleo ambayo kila mmoja anatakiwa ayapigie makofi kwani huku ndiko ambako wengi tulitamani kufika.

Unaona kabisa malengo ya timu yanaelekea wapi na mwanga wa soka la kiweledi linaonekana.

Simba tayari inaeneo lake huko Bunju na wachezaji wanapata muda wa kufurahia eneo hilo huku wakicheza kwa kufuata utaratibu sahihi.

SIMBA DAY

Tayari tupo katika wiki ya Simba day ambapo kilele kitafanyika Agusti 22 uwanja wa Mkapa na Uhuru.

Mipango ya Simba mwaka huu imekuwa kivingine kabisa na kukusanya fedha zitakazoletwa na mashabiki kwa kuingia uwanjani.

Utaratibu waliouweka ni mzuri mno huku wakimuongeza Diamond Platnumz kunogesha sherehe hiyo kwani atatumbwiza jioni  mtanange.

Timu itakayo kuja ni Vital O ya Burundi ambako itamenyana na mabingwa Simba katika uwnaja wa Mkapa.

Leo hii imezindua wimbo mpya utakao iwakilisha Simba tena mtunzi akiwa Diamond.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
HERSI

Waliombeba Injinia Hersi watakuja kumshusha!

Tanzania Sports

Sevilla na rekodi ya Kombe la Europa