*Conservative wamejawa hofu, wanapingana
Hali ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, Covid-19 inayosababishwa na virusi vya corona imembadili Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson na kuwafanya pia wanachama wa chama tawala cha Conservative kujawa hofu.
Huyu ni waziri mkuu ambaye mwenyewe ameugua ugonjwa huo, na anajua kwamba hauwezi kutibiwa kwa namna tu ya kufikirika bila kuchukua hatua muhimu. Ikiwa Conservative wangejua mwaka jana kwamba janga hili lingetokea, je, wangefanya uchaguzi huu huu wa Johnson au ingekuwa tofauti?
Sifa za Jeremy Hunt, kama waziri wa zamani wa afya zingeweza kupewa uzito kuliko za huyu, japokuwa si sana. Yaani tuseme kama ingewezekana kurudi kwa wanachama hawa, maarufu kwa jina la Tories, mwaka jana kwenye mkutano ambao wagombea walikuwa wakijieleza kwa wapiga kura, uwaeleze kwamba kungetokea virusi vya Corona na kwmaba wangehitaji uwezo mkubwa wa waziri mkuu kuvidhibiti.
Wajumbe wale wangejawa na wasiwasi. “Mradi wa Hofu,: wangefoka. Wanataka tu kujua iwapo Boris Johnson atawafanyia vyema katika mradi wa kundoka Umoja wa Ulaya – Brexit na kushinda uchaguzi mkuu, jambo ambalo anafanya.
Tukirudi Mei 2020, tunakutana na wabunge wa Conservative wakinung’unika dhidi ya hatua zinazochukuliwa na serikali kukabili virusi vya Corona na ugonjwa viuletavyo. Hatua zake zinachanganya watu, kuna udhaifu fulani. Na hay ani mawimbi tu ya kutokukubaliana na Johnson ambapo ataendelea kukosea zaidi kabla ya chama kuchukizwa na kuaibika. Lakini kwa juu, mawimbi yanaonekana kwambna kuna matatizo makubwa zaidi.
Mvutano ni baina ya watu wa Conservative ambao wanakosa uvumilivu wa kuiondoa nchi katika kufungia watu ndani, wakieleza gharama za uchumi kuanguka kwa upande mmoja, lakini upande wa pili ni wale wanaoogopa kwamba kulegeza masharti ya ‘lockdown’ kutasababisha virusi kuibuka upya na kupata nguvu ya kuua tena.
Hiyo ni tofauti kati ya falsafa na tabia. Wasiotaka watu wafungiwe ndani zaidi hawaamini katika serikali hasa kwenye mambo yanayohusisha yenyewe kulipa watu mishahara au kuwaambia jinsi ya kujielekeza kimaisha wakati huu mgumu.
Hawapendi karantini kama ambavyo wasivyopenda utendaji wa wizara yenye dhamana ya afya au mambo ya Umoja wa Ulaya (EU). Wanaona kwamba kutoa fedha za kukwamua watu kiuchumi au kampuni na mashirika kutumia fursa ya kusogeza mbele muda wa kuwalipa wafanyakazi kisha serikali ibebe mzigo, ni sawa na kutembea huku wamelala kuelekea kwenye ujamaa.
Johnson hataki kuwaudhi wabunge wenye mtazamo huo, kwa sababu kwa kiasi fulani silika yake mwenyewe inampeleka uelekeo huo. Kadhalika, kutafuta ugombi na Tories wenye mrengo wa kulia ni jambo la hatari kwa shughuli za viongozi wa chama. Kuwakubalia katika hilo kwa sera za ajabu umekuwa ndio mbadala kwa kawaida.
Akiwa mwenyewe aliambukizwa virusi na kuonja machungu yake, Johnson anapata ushauri kutoka kwa wanasayansi wanaomwambia kwamba virusi hivyo vinasambaa kwa hiyo si sawa kuruhusu shughui zisizoratibiwa na kudhibitiwa ipasavyo.
Kuna hali ya mkorogano kati ya kauli mpya ya serikali siku hizi isiyokuwa bayana ya ‘kaeni macho’ iliyotokana na mgogorokati ya masuala anuai ya kliniki kwa upande mmoja na matakwa ya kisiasa ya juu ya maelezo mapya tofauti na hayo ya kitabibu, kwa sababu wanaona kwamba katika baadhi ya mijadala, hayo ya awali hayafai.
Na hapo ndipo tunaona watu wakikunjiana ndita hapa England – na ni England pekee – wakibadili kanuni, huku wakiacha mambo kama vile vile. Johnson anataka kuondoka kwenye karantini, lakini hapo hapo miguu yake ikiwa imegandamizwa kweye eneo lililotengwa.
Baadhi ya Tories ambao wangetaka kiongozi wao akimwagiwa zigo la lawama baada ya kuwa ametoka kwenye chumba kile cha uangalizi maalumu – ICU. Kuna wanaohisi kwamba waziri mkuu huyu mwenye hadhari, akitoka kwenye karantini tofauti na matakwa ya madaktari, siye yule waliyemwajiri mwaka jana; sasa wananong’onezana kwamba amepoteza ujasiri wake na kuonesha woga.
Ni kweli kwamba mwenendo wa Johnson umebadilika na ugonjwa huu mbaya huwa una kawaida ya kuacha makovu ya kisaikolojia. Hata hivyo, kuna ikwesheni rahisi la kisiasa ambalo jamaa wa Downing Street wanalijifunza.
Katika hatua za awali, hadhi ya Johnson ililindwa mbele ya umma na watu walioonesha heshima na huruma, na kwamba walitambua kuwa ugonjwa ndio ulitakiwa kulaumiwa kwa kuua watu, na siw anasiasa waliokuwa wakijaribu kuuzuia. Lakini katika hatua ya pili, mambo yanaweza kumgekia – kwamba maambukizi yamerudi na yataunganishwa na uamuzi wake wa kulegeza masharti ya karantini au kujitenga.
Ama wengi katika Westminster wanajielekeza kwenye siasa za siku hadi siku japokuwa wanamikakati wa Tories hawajasahau juu ya uchaguzi wa bunge wa mwakani huko Uskochi sambamba na wimbi la kutaka uhuru linalosogezwa hapo Downing Street.
Chochote kitakachochukuliwa kwake kama kiburi au kutojali ni sumu kwa Johnson. Wabunge wa upinzani wanachukua hadhari sana, lakini pia Tories kwenye baadhi ya majimbo kama ya kati, kaskazini mwa England na Wales – ilikokuwa ngome ya Labour hadi Desemba mwaka jana.
Johnson hangekuwa madarakani bila viti hivyo, ambapo alifanya kazi kubwa sana ya kushawishi, akichanganya karisma yake na mpango wa Brexit kuvunja ngome iliyokuwa na utamaduni tofauti kabisa na wa Tories. Hata hivyo, hili la Covid-19 linaweza kuwasaidia Labour kupindua meza. Alipigiwa kura na hata watu wasiokuwa Tories, akicheza atapoteza.
Waziri Mkuu amejifungia kwenye fundo, akijaribu kwa mkono mmoja kufanya imla kutoka kwenye siasa, wakati kwa huo mkono mwingine kumlisha dubu mwenye uchu itikadi ambayo ataimeza bila kuitafakari wala kutaka ushahidi. Utata umekuwa kana kwamba ni kitu muhimu kwenye mradi wote
Walisema ima faima, angepigiwa kura na hata wanaomchukia ndani ya chama chao na hakika mvutano uliokuwa mkubwa wakati ule uliikwa na matokeo ya uchaguzi pamoja na Brexit, lakini sasa janga la Covid-19 linauibua tena. Kushughulikia janga hili ni ghali, kunachanganya na ni kazi kubwa ya serikali. Kuchanganyikiwa kwao kutaongezeka; atajaribu kuwaridhisha pasipo kufanya kila wanachotaka, formula ambayo ni dhahiri itasababisha mgawanyiko kwenye chama, ufanisi hafifu serikalini na kushindwa katika hatua muhimu za janga la Covid-19.