in , ,

Ronaldo naye avuruga

Ronaldo naye avuruga

Nyota wa Ureno na Juventus, Cristiano Ronaldo ameingia matatani baada ya kukiuka maagizo ya kukaa ndani, akatoka na kwenda kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa Madeira, kwao Ureno.

Na sasa ameonywa, akiambiwa kuwa kwake nyota asichukulie kwamba ana kinga dhidi ya maelekezo yanayotolewa na serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO) juu ya jinsi ya kujingika na virusi hatari vya corona vinavyoua maelfu ya watu.

Watu wa Ureno, kama wa mataifa mengine mengi ya Ulaya na kwingineko, wametakiwa kubaki majumbani mwao, isipokuwa wale wenye shughuli maalumu kama za kuhudumia wagonjwa au kutoa huduma za lazima kama chakula, maji na dawa.

Nyota huyu wa zamani wa Real Madrid anayesifika kwa jinsi anavyofunga mabao mengi, alikwenda kwao Ureno wakati ugonjwa huo ukianza kushika kasi nchini Italia, akajitenga pamoja na familia yake, lakini pia akawa kwa ajili ya kumsaidia mama yake mzazi aliye mgonjwa.

Ronaldo alioneshwa kwenye klip akifanya mazoezi na wachezaji kadhaa, waliokuwa wakitumia mipira zaidi ya 10. Viongozi wa serikali wanasema kwamba mchezaji huyo aliyekuwa katika mazoezi ya ‘siri’ kwenye uwanja unaotumiwa na klabu ya CD Nacional, Funchal huko kisiwani, anatakiwa kuwa ndani kwake kama watu wengine ili kukwepa maambukizi.

“Ronaldo hawezi kuwa au kupewa upendeleo wowote katika hili. Hana kinga wala ruhusa ya kutoka kwenda kufanya mazoezi nje. Cristiano Ronaldo ana haki ya kufanya mazoezi ndani mwake ikiwa ataheshimu na kufuata kanuni kama wananchi wengine, hakuna cha upendeleo,” akamaka Mkuu wa Huduma za Afya wa Madeira, Pedro Ramos.

Licha ya wachezaji waliokuwa wakifanya naye mazoezi, zilionekana picha za watu wengine waliokuwa kando wakiwatazama, akiwamo mtoto.

Ramos anasema kwamba wananchi wanaweza kutoa nje ikiwa tu watafuata maelekezo ya kutokuwa kwenye mikusanyiko kwa kukaa umbali ulioelezwa. Akasema kwamba mchezaji nyota duniani kama Ronaldo anatakiwa kuonesha mfano kwa wengine, lakini amefanya tofauti kabisa, jambo linaloweza kuwa na athari mbaya kwa wengine, hasa watoto kuiga na kwenda kucheza nje.

Kitendo cha Ronaldo kinakuja baada ya kile cha Kocha wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho aliyekwenda naye kwenye mazoezi, akiwa na mchezaji wake ghali zaidi, Tanguy Ndombele na wenzake kama mlinzi Serge Aurier.

Baadaye alikiri kwamba alikosea kukiuka amri ya Serikali ya Uingereza ya kutaka watu wakae ndani, kwani ugonjwa wa homa ya mapafu umekuwa ukikumba wengi na kusababisha vifo hata jijini London anakokaa Mourinho.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson mwenyewe ameambukizwa na kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya St Thomas ya jijini hapa.alizidiwa hadi kupelekwa kwenye chumba cha uangalizi maalumu, na inaelezwa itachukua muda kurudi katika hali ya kawaida kama ni kupona. Kwa sasa nafasi yake inakaimiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Dominic Raab

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Machafuko Barcelona

Tanzania Sports

Harry Kane Madrid?