matokeo hayo yaliwafanya Comoro kusogea pointi tisa huku wakisubiri mechi yao na timu ya taifa ya misri.
Kisiwa cha komoro hivi karibuni kiliushangaza ulimwengu wa soka baada ya timu yao ya taifa kuweza kufuzu kushiriki katika mashindano soka ya mataifa afrika ya mwaka 2021 ambayo yatafanyikia nchini Cameroon. Hii ni itakuwa mara ya kwanza kwa nchi hiyo kushiriki mashindano hayo toka yaanze. Tukio hilo lilitokea mnamo alhamisi ya tarehe machi 25 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na timu ya taifa ya Togo.
Kipenga cha mwisho kilipopulizwa katika uwanja wa stade said Mohammed Cheikh uliopo katika mji mkuu wa nchi hiyo unaofahamika kama Moroni. matokeo hayo yaliwafanya Comoro kusogea pointi tisa huku wakisubiri mechi yao na timu ya taifa ya misri. Wachezaji toka kisiwa hicho walibeba ndoto ya ya wananchi wa taifa hilo. Kundi lao halikuwa rahisi kwani walikuwa kundi moja likiwa na timu zenye wachezaji wenye uzoefu wa mashindano makubwa kama vile Togo, Misri, na majirani zetu Kenya.
Kikosi chao kina wachezaji ambao wengi wanacheza ulaya licha ya kwamba wanacheza katika timu ndogo. Wachezaji hao ni kama vile: Alli Ahmada ( bran Beggen- Denmark), m’dahoma Kassim(sc lyon-Ufaransa), Youssouf Bendjaloud( le mans fc- ufaransa),zahary Younn( pau fc- ufaransa), mogni ahmed( Annecy fc-ufaransa), faiz selemani( kv Kortrijk- ubelgiji), rafidine Abdullah( stade laisannem ouchy- uswisi), youssouf chongama( ac Ajaccio-ufaransa) nadjim abdou( fc martigues-ufaransa), fouad bachirou( Nottingham forest-uingereza), said bakari( RKC Waalwijk-uholanzi), ben nabouhane el fardou(crvena zvezda beograd- Croatia), faiz Mattoir( ac Ajaccio- ufaransa) na ibbroihim youssouf( fc Nouadhibou-mauritania)
Hakika ni jambo la kushangaza sana timu nzima ina wachezaji wa kimataifa tu yaani hakuna hata mchezaji mmoja ambaye anacheza katika ligi ya nyumbani na yaonekana hawa jamaa walijipanga muda mrefu sana kwani kuweza kupata timu nzima ambayo haina hata mchezaji mmoja anayecheza katika ligi ya ndani si jambo dogo. Nakumbuka jeuri hiyo walikuwa wanaweza kufanya wanaijerria tu peke yao kuwa na kikosi kizima kikiwa kinacheza katika ligi za ulaya na hakuna hata mmoja anayecheza katika ligi za ndani. Lakini hiyo ni naijeria ya nyakati za huko nyuma.
Ligi kuu ya soka ya nchi hiyo ni ndogo sana na hata ukiangalia uwanja wa taifa wa nchi hiyo una uwezo wa kuingiza mashabiki wachache tu yaani mashabiki 2000 tu. Nchi hiyo ina watu wasiozidi milioni 2. Ligi kuu yao ni ndogo sana na hushirikisha vilabu 10 tu na wala sio ligi yenye ushindani katika bara la afrika. Katika klabu bingwa afrika hakuna timu ya komorro ambayo huchachafya vilabu vingine wala kuvuma huku nyuma. Nchi hiyo kilijiunga na chama cha soka barani afrika CAF mnamo mwaka 2005 tu yaani juzi juzi tu.
Udogo wa nchi au uchache wa kazi inaonyesha sio kigezo katika mafanikio kisoka. Kwa hapa tunaona ili soka lisonge mbele lazima kuwe na mikakati ya mda mrefu. Kwanza kabisa suala la timu nzima kuwa wanacheza soka la kulipwa katika nje ya taifa hilo hili haliwezi kuwa lilikuja kirahisi bali ni matokeo ya mipango ya mda mrefu ya kuhakikisha wanawabidhaisha wachezaji wa nchi hiyo katika timu za ulaya. Na tunaona kwamba wametumia mahusiano mazuri waliyonayo na taifa la ufaransa kuwauza wachezaji wao katika vilabu vidogo katika nchi hiyo ili kucheza katika ligi hiyo.
Halikadhalika tukiangalia timu hiyo ya taifa ya komoro tutaona kwamba inafundishwa na kocha ambaye mwenye uraia wa nchi hiyo licha ya kwamba amezaliwa ughaibuni. Kocha huyo anayefahamika kwa jina la Amir Abdou ndiye kocha aliyeipeleka timu hiyo katika mashindano ya kombe la mataifa huru ya afrika. Na hana uzoefu mkubwa sana katika ukocha ila kaifikisha timu ya taifa hilo mbali.
Kwa muono wangu mimi ni muda muafaka sasa kuanza kuamini makocha wazawa wapewe mafunzo ya ziada ya ukocha na kisha wakabidhiwe timu zetu za taifa. Yawezekana tukaja kupata mafanikio makubwa tu na makocha wazawa kuliko makocha wa kutoka ughaibuni katika timu zetu za taifa.
Comments
Loading…