in , , ,

Chelsea wavunjiwa daraja lao

*Man U washinda Stamford Bridge baada ya miaka 10

*Liverpool nusura wawatoe nishai Everton kwao

Ilikuwa Jumapili ya kukamiana, iliyoshuhudia wageni wakiwapeleka puta wenyeji katika dakika za mwanzo za mechi kwa mabao 2-0.
Manchester United waliokuwa Stamford Bridge walianza kwa kasi na kuwakokota Chelsea, kama Liverpool waliokuwa Goodison Park walivyowakimbiza Everton mchakamchaka na kutangulia kwa mabao 2-0 pia.
Matokeo yangeweza kuwa sawa ya ushindi wa mabao 3-2 kama bao la tatu la Luis Suarez katika dakika za majeruhi halingekataliwa kwa madai ya kuotea.
Manchester United walifanikiwa kuwafunga Chelsea Stamford Bridge kwenye Ligi Kuu kwa mara ya kwanza katika miaka 10.
Hata hivyo, United hawakuwa na kazi rahisi, na  baada ya Chelsea kuchomoa mabao hayo mawili na kuwa sare, walifanikiwa kupata bao baada ya wachezaji wawili wa Chelsea kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Beki Branislav Ivanovic alitolewa kwa mchezo wa rafu akijaribu kupunguza shinikizo la Man U, wakati Fernando Torres alipewa kadi ya pili ya njano kwa madai ya kujirusha baada ya kuguswa na beki Johnny Evans.
Pamoja na kuwa ushindi wa kwanza Stamford Bridge katika miaka 10, ulikuwa mchezo wa kwanza msimu huu Chelsea kupoteza, na waliondoka uwanjani wakiwa wamekasirika.
Ilibidi makocha Roberto Di Matteo wa Chelsea na Sir Alex Ferguson watenganishwe, baada ya Mtaliano huyo kuona kwamba wanaonewa.
Licha ya kadi mbili nyekundu, Chelsea wanaona kwamba mfungaji wa bao la tatu, Javier Hernandez ‘Chicharito’ alikuwa ameotea.
Lakini uamuzi wa mwisho ni wa refa, na Jumapili hii alikuwa Mark Clattenburg, ambaye msimu huu ameshatoa robo ya kadi zote nyekundu walizotoa waamuzi kwenye mechi za Ligi Kuu ya Uingereza.
Bahati ya Chelsea ya tangu kuingia Di Matteo iligeuka balaa, baada ya David Luiz kujifunga kabla ya Robin Van Persie kupachika bao la pili mapema kipindi cha kwanza.
Alikuwa Juan Mata ambaye nyota yake imekuwa iking’aa siku za karibuni, aliyefunga bao la kwanza la Chelsea na nusura afunge la kusawazisha kabla ya mapumziko. Ramires alilifunga kipindi cha pili kabla balaa mambo hayajaanza kwenda kombo.
Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich alionekana amejikunyata kimya muda mwingi wa mchezo, huku Ferguson akisema kadi nyekundu zilikuwa stahili ya wachezaji wa Chelsea, na watatakiwa kujilaumu wenyewe.
Kwa ushindi huo, Manchester United wamepunguza pengo kubwa kati yake na Chelsea na kuacha pointi moja, wakishika nafasi ya pili, kwa kuwashusha Manchester City hadi ya tatu.
Ama katika dimba la Goodison Park, Everton walionekana kuwa na bahati kubakishiwa walau pointi moja, kwani licha ya kulala bao 2-0 mapema na kuja kusawazisha baadaye, bao la tatu la Liverpool lilikataliwa.
Suarez ambaye angeondoka na ‘hat trick’ na pointi ambazo zingeibeba sana Liverpool kwenye msimamo wa ligi, alishangilia bao la kwanza kwa kujirusha mbele ya kocha wa Everton, David Moyes.
Kocha huyo alikuwa amesema kabla ya mchezo kuwa Suarez ana tabia ya kujirusha au kuanguka hovyo. Moyes hakuwa na la kufanya, na muda mfupi baadaye akashuhudia Suarez akitikisa tena nyavu za Everton.
Ilikuwa mechi ya 219 ya watani hao wa jadi, ambapo Everton walipambana vilivyo na kufanikiwa kukomboa mabao kupitia Leon Osman na Steven Naismith.
Kwa matokeo hayo, Everton wanashika nafasi ya tano, lakini pia Liverpool inazidi kujiimarisha, kwani hii ni mechi ya tano pasipo kufungwa, baada ya kuanza msimu vibaya.
Tottenham imefanikiwa kukwea hadi nafasi ya nne, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya vibonde wa ligi, Southampton.
Vijana hao wa Andre Villas-Boas nusura wakose ushindi, kutokana na jinsi Southampton walivyogangamala kutaka kusawazisha na pengine kuondoka na ushindi.
Magoli ya Spurs yalifungwa na Gareth Bale na Mmarekani aliyesajiliwa kutoka Fulham msimu huu,
Clint Dempsey. Southampton walisawazisha katika kipindi cha pili kupitia kwa Jay Rodriguez.
Newcastle United walibahatika kushinda kwa goli la dakika za majeruhi dhidi ya West Bromwich Albion, hivyo mchezo kumalizika kwa mabao 2-1.
Ilikuwa kiki ya Sammy Amoebi iliyomgonga mchezaji machachari, Papiss Cisse na kwenda wavuni moja kwa moja, kuwaandikia Newcastle bao la pili, baada ya lile la Demba Ba dakika ya 35.
Mchezaji aliye West Brom kwa mkopo kutoka Chelsea, Romelu Lukaku aliwasawazishia wageni dakika ya 55, na wengi walishachukulia kwamba mpira ungemalizika kwa sare hiyo, japokuwa Cisse hakutulia muda wote, akitafuta bao la ushindi kwa udi na uvumba.
Hadi sasa West Brom hawajashinda ugenini na wamebaki nafasi ya nane, wakati Newcastle ni wa 10.
Funga wiki hii inawaacha Fulham katika nafasi ya saba, West Ham wa tisa, Swansea wakiwa nafasi ya 11 wakifuatiwa na Liverpool, Stoke City na Sunderland.
Wigan wanashika nafasi ya 15 wakifuatiwa na Norwich wakati Aston Villa wakiwa katika nafasi ya 17, Reading ni wa 18, Southampton wa 19 na pazia linafungwa na Queen Park Rangers (QPR) katika nafasi ya 20.
Mabingwa wa England, Manchester City, ndio wamebaki timu pekee bila kufungwa mchezo wowote msimu huu hadi sasa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

TOC kukutana Zanzibar kujadili mkutano

Nani zaidi: Clattenburg au Chelsea?