in , , ,

Chelsea nje Ulaya

*Liver wawapiga Man U Europa*

Wakati Manchester United wamelala mbele ya Liverpool katika mchezo wa

Ligi ya Europa, vigogo wengine wa England, Chelsea wametolewa katika

Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).
Ndoto za Chelsea na kocha wa wa mpito, Guus Hiddink kusonga mbele na

labda kutwaa ubingwa wa Ulaya zilikatishwa kikatili katika hatua ya 16

bora na Paris Saint-Germain (PSG) wakiongozwa na Zlatan Ibrahimovic.
Japokuwa Chelsea walikuwa wakicheza nyumbani Stamford Bridge,

walishindwa kufurukuta huku wageni wakiingia wakiwa kifua mbele

wakijivunia kuwa na utangulizi wa mabao 2-1 kwenye mechi ya mkondo wa

kwanza.
Ibrahimovic alitoa pasi maridhawa kwa Adrien Rabiot aliyecheka na

nyavu karbu kabisa na lango katika dakika ya 16 tu.
Diego Costa alifanya vyema kuwafanya Chelsea kuwa sare huku

wakitarajia kupata mabao zaidi lakini alipotoka uwanjani kutokana na

majeraha na Ibrahimovic kufunga bao la pili, ilikuwa msumari wa mwisho

kwenye jeneza la Chelsea.
Alikuwa mchezaji wa zamani wa Manchester United, Angel di Maria

aliyempa pasi nzuri Ibrahimovic na kuwafanya PSG kutinga robo fainali

ya michuano hiyo.
Chelsea wanaoshika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England

wanaweza wasishiriki michuano yoyote ya Ulaya msimu ujao, tena Costa

na Eden Hazard wakiumia kabla ya mechi ya robo fainali ya Kombe la FA

dhidi ya everton Jumamosi hii.
LIVERPOOL WAWAPIGA MAN U EUROPA

Man Utd Hoi..
Man Utd Hoi..

Manchester United wamepoteza moto wao kwenye Ligi ya Europa baada ya

kukubali kichapo cha 2-0 kutoka kwa Liverpool.
Kiungo wa zamani wa United, Paul Scholes amesema kwamba Mashetani

Wekundu walikuwa hovyo sana kwenye mechi hiyo, akiendeleza

mashambulizi yake dhidi ya kocha Louis van Gaal.
Ilikuwa United wapokee kichapo zaidi kama si kipa wao, David de Gea

kujitahidi kuzuia mabao mengine, lakini akashindwa yale ya Daniel

Sturridge na Roberto Firmino.
Hiyo ilikuwa mechi ya mkondo wa kwanza na United watajua hatima yao

watakapowakaribisha Liverpool Old Trafford kwa mechi ya mkondo wa pili

Alhamisi ijayo.
Scholes alieleza mshangao wake kwa klabu yake hiyo ya zamani kupigwa

hovyo, akisema wana kiwango chao cha juu wanachotakiwa kukihakikisha

na kwamba wanatakiwa kuwania ubngwa wa England na wa Ulaya.
Walitupwa kwenye Ligi ya Europa, ligi ndogo tu, baada ya kumaliza

wakiwa wa tatu kwenye kundi lao la UCL, na wenzao waliobimbirika nao

kutoka huko juu ni Wolfsburg, PSV Eindhoven na CSKA Moscow.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

SIMBA YAWAADHIBU NDANDA, YAREJEA TENA KILELENI

Tanzania Sports

Ulivyo uwezekano wa Leicester ama Tottenham kutwaa taji la EPL