in , , ,

Chelsea mbendembende

*Wamecharazwa 3-1 na Liverpool

*Arsenal na Manchester City safi

Hali imezidi kuwa mbaya kwa Chelsea ya Jose Mourinho, baada ya kupoteza mechi ya sita 

Jumamosi hii.

Chelsea walifungwa 3-1 na Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England (EPL) na kuongeza machungu na shinikizo kwa Mourinho.

Chelsea walianza mechi vyema na kupata bao dakika ya nne tu kupitia kwa Ramires ambaye amesaini mkataba mpya wa miaka minne hivi karibuni.

Hata hivyo, kibao kiligeuka kuanzia dakika ya 45 pale Coutinho aliposawazisha kabla ya kuongeza bao la pili dakika ya 74 na Christian Benteke kupiga la tatu katika dakika ya 83.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alifurahia kupata ushindi huo, ukiwa ni wa pili tangu kuichukua timu, ambapo alianza kwa sare tatu mfululizo.

Chelsea ambao ni mabingwa watetezi sasa wanashika nafasi ya baada ya kuwa wamepoteza mechi sita kati ya 11 walizocheza, na lolote linaweza kutokea kwa kocha huyo ambaye amekuwa akiungwa mkono na mmiliki wa klabu, Roman Abramovich, ambapo wamebakia katika nafasi ya 15.

Pamekuwa na tetesi kwamba kuna mpasuko klabuni, ikielezwa ni kana kwamba kuna uasi, hasa miongoni mwa wachezaji waandamizi, matatizo yakianza tangu Mourinho alipomshusha hadhi daktari wa kikosi cha kwanza, Eva Carneiro. Liverpool wamepanda hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi.

ARSENAL WAWAPOPOA SWANSEA 3-0

Joel Campbell
Joel Campbell

Arsenal wameendelea vyema licha ya kuwa na majeruhi wengi, ambapo wanawapumulia vinara wa ligi – Manchester City baada ya kuwachabanga Swansea 3-0.

Wakicheza ugenini, vijana wa Arsene Wenger walimaliza kipindi cha kwanza bila kupata bao, lakini moto wao ulianza kipindi cha pili.

Kwa ushindi huo wanafungana kwa pointi 25 lakini City wana mabao manne zaidi katika uwiano wa kufunga na kufungwa. Wafaransa wawili – mshambuliaji Olivier Giroud na beki wa kati Laurent Koscielny waliendeleza mtindo wao wa kufunga.

Mshambuliaji ambaye hutumika kwa nadra, Joel Campbell alifunga bao lake la kwanza tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi, akichezeshwa kutokana na kukosekana wachezaji muhimu walioumia kama Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain. Majeruhi wengine wa Arsenal ni Aaron Ramsey, Mikel Arteta, David Ospina, Jack Wilshere, Danny Welbeck na Tomas Rosicky

Kwa Swansea, matokeo hayo ni mabaya kwa sababu ndio kwanza walijikomboa mechi iliyopita kwa kumaliza mfululizo wa mechi sita bila ushindi kwa kuwafunga Aston Villa. Wameporomoka hadi nafasi ya 13.

Ushindi wa Arsenal ulishuhudia wakifikisha idadi ya mabao 2,000 tangu Wenger ajiunge na kikosi hicho.

MANCHESTER CITY MWENDO MDUNDO

Man city....moto
Man city….moto

Manchester City wameendeleza wimbi la ushindi, japokuwa safari hii walifanya kazi ya ziada kwa kupata bao la ushindi dakika ya 90 dhidi ya Norwich waliokomaa muda wote wa mchezo.

Alikuwa ni Yaya Toure aliyefunga bao la pili, ambapo wangeenda 1-1 kutokana na mabao ya Nicolas Otamendi wa City na Cameron Jerome. City walikosa bao la tatu, baada ya Aleksandar Kolarov kukosa penati.

MAN UNITED WABANWA NA PALACE

rooney....
rooney….

Manchester United wameshindwa kwenda na kasi ya vinara wa ligi, baada ya kwenda suluhu na Crystal Palace.

Vijana hao wa Louis van Gaal walitawala vyema mchezo, lakini walishindwa kufunga, kutokana na uimara wa timu ya Alan Pardew.

Katika mechi nyingine, Newcastle walikwenda suluhu na Stoke, Watford wakawafunga West Ham United 2-0 huku West Bromwich Albion wakilala nyumbani kwa 2-3 dhidi ya Leicester.

Advertisement
Advertisement

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

FIFA: Nani kuwa rais?

Tanzania Sports

LIGI YA MABINGWA ULAYA: