in , , ,

Chelsea, Man U, City washinda

Mzunguko wa 25 wa Ligi Kuu ya England (EPL) umemalizika kwa ushindi kwa timu kubwa, huku kocha wa Aston Villa, Paul Lambert akifukuzwa kazi.

Chelsea walipata ushindi kwa tabu dhidi ya Everton kwa bao la dakika za mwisho la Willian, hivyo kujiweka pointi saba mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City.
Gareth Barry alipewa kadi nyekundu iliyozua mzozo na kocha wa Everton, Roberto Martinez alisema kwamba Chelsea wanajaribu kuwashawishi waamuzi.
Kadhalika Branislav Ivanovic wa Chelsea, katika hali ya kushangaza hakuadhibiwa licha ya kumkaba vibaya James McCarthy.

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alimwanzisha kipa wa zamani namba moja, Petr Cech badala ya yule aliyekuwa kwa mkopo Atletico Madrid, Thibaut Courtois.
Katika mechi nyingine, Manchester City waliwakandamiza Stoke 4-1.

baba

Mabao mawili ya City yalifungwa na Sergio Aguero, moja likiwa ni kwa penati na mengine yalitiwa kimiani na James Milner na Samir Nasri.
Manchester United nao walishinda, wakipanda hadi nafasi ya tatu kwa kuwashinda Burnley 3-1 kwa mabao mawili ya Chris Smalling na la Robin van Persie.

Hata hivyo, United walipata pigo baada ya kuumia kwa Phil Jones na Daley Blind. Burnley wameshinda mechi moja tu kati ya tisa walizocheza na inayofuata ni dhidi ya vinara wa ligi Chelsea. Bao lao lilifungwa na Danny Ings anayetajwa kuwania na klabu kadhaa kubwa.

man u

Matokeo mengine ya ligi hiyo ni kwa Southampton kwenda suluhu na West Ham, Crystal Palace kwenda sare ya 1-1 na Newcastle huku West Bromwich Albion wakiwafunga Swansea 2-0.
Katika tukio jingine, Aston Villa wamemfukuza kocha wao, Paul Lambert kutokana na mwenendo mbaya wa ligi, ambapo wametumbukia kwenye eneo la kushuka daraja, wakiwa nafasi ya 18 na pointi 22.

Wengine walio hatarini ni Burnley wenye pointi 21 na mkiani kabisa ni Leicester waliokwishazoea huko, wakiwa na pointi 17 tu. Villa ndio wana mizania mbaya zaidi ya mabao, yakiwa ni -21.
Chelsea wanaongoza ligi wakiwa na pointi 59, Man City 52, Man United 47 wakati Southampton wana 46 na Arsenal moja pungufu.

Tottenham Hotspur waliofungwa na Liverpool juzi wana pointi 43 katika nafasi ya sita wakati Liver wanawafuatia wakiwa na pointi moja pungufu. West Ham ni wa nane, Swansea wa tisa na Stoke wanafunga 10 bora.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal, Liverpool, QPR zatakata

Wachezaji Ivory Coast wapata mamilioni, nyumba