in , , , ,

Chelsea, City, Spurs mbendembende

Hatua ya nne ya michuano ya Kombe la FA imezidi kuacha wadau vinywa wazi, baada ya Chelsea na Manchester City wakicheza nyumbani kutupwa nje na timu za madaraja ya chini.
Chelsea walifungwa 4-2 na Bradford, katika matokeo ya kushangaza zaidi kwenye historia ya michuano hii, kwani kwa sasa Chelsea ndio wanaoonekana kuwa timu nzuri zaidi nchini England na hadi dakika ya 30 walikuwa wakiongoza kwa 2-0.

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alisema ni aibu kubwa kwake na kwa wachezaji kutolewa na timu hiyo ndogo iliyo nafasi 49 chini ya Chelsea na hii ilikuwa mara ya kwanza katika miaka 18 kwa Bradford kuingia hatua ya tano ya michuano hii.

Kutupwa nje huko kumezima ndoto za Chelsea za kutwaa mataji manne msimu huu, ambapo mabao ya Ramires na Garry Cahil yalirejeshwa na wageni kutundika mengine mawili kupitia kwa Jon Stead, Filipe Morais, Andy Halliday na Mark Yeates ambao walionekana kutoamini hata kile walichofanya.

Msimu huu Chelsea wameshinda mechi zao zote 10 walizocheza nyumbani, hivyo washabiki hawakujua kufungwa kukoje, hadi vijana hao walipofika na kuwaaibisha. Hii imekuja siku moja tu baada ya Manchester United kulazimishwa suluhu na Cambridge United na sasa watarudiana Old Trafford.

MANCHESTER CITY CHALI

Katika matokeo mengine ya aina yake, mabingwa watetezi wa England, Manchester City wakicheza mbele ya washabiki wao Etihad, walilambwa 2-0 na Middlesbrough walio Ligi Daraja la Pili (Champions).
City walicheza baada ya kutoka Abu Dhabi walikokwenda kufanya mazoezi na hii ni mara ya pili mfululizo wanatolewa na timu za daraja hilo, kwani msimu uliopita walitolewa na Wigan.

Walianza kupigwa Jumamosi hii na mshambuliaji Patrick Bamford dakika ya 53 kutokana na kosa lililofanywa na Fernando wa City. Lee Tomlin wa wageni aligonga mlingoti kama ilivyokuwa kwa Frank Lampard wa City. Tomlin alifunga bao lililokataliwa kwa maelezo alikuwa ameotea.

Wakati City wakijaribu kila namna kusawazisha ili walau waje kurudiana siku zijazo, mchezaji Kike aliyetokea benchi alipigilia msumari kwenye jeneza la Man City dakika ya 90.

WENGINE WALIOLIZWA HAWA

Katika matokeo mengine, Tottenham Hotspur walipokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa Leicester walio kwenye hatari ya kushuka daraja, huku wenzao wabovu Crystal Palace wakiwang’oa Southampton kwa 3-2 naLiverpool wakashindwa kuwamaliza Bolton hivyo kwenda suluhu..

Swansea nao walionja joto ya jiwe kutoka kwa timu ya daraja la chini ya Blackburn baadaya kukandikwa 3-1, Sunderland wakaenda suluhu na Fulham, Birmingham wakafungwa 2-1 na West Bromwich Albion, Cardiff wakalala 2-1 kwa Reading, Derby wakawafunga Chesterfield 2-0 na Preston wakienda sare ya 1-1 na Sheffield United.

Jumapili hii mabingwa watetezi wa FA, Arsenal wanakipiga ugenini na Brighton, West Ham wanakuwa wageni wa Bristol City wakati Aston Villa wanawakaribisha Bournemouth.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Man United wabanwa na ‘watoto’

Kundi D lajifunga AFCON