in , , ,

Chelsea, City hawajaonja chungu ya kufungwa

*Reading, Norwich, QPR hawajui tamu ya ushindi

*Man United, Everton katika nne bora, Spurs yaja

Mzunguko wa saba wa mechi za Ligi Kuu ya England (EPL) umemalizika, Chelsea wakiendelea kuongoza na Manchester United wakichupa nafasi ya pili.
Wamefanya vyema licha ya masahibu ya nahodha wao John Terry kupatwa na hatia ya kutukana kibaguzi na kupewa adhabu, huku beki Ashley Cole akiwatukana maofisa wa FA na kusubiri adhabu klabuni na FA.
Mwisho wa wiki Chelsea waliwakung’uta Norwich mabao 4-1 wakati United waliwashinda Newcastle kilaini kwa 3-0.
Ushindi pia ulielekea kwa mabingwa wa EPL, Manchester City dhidi ya Sunderland kwa idadi hiyo hiyo ya mabao.
Arsenal nao waliwatandika West Ham United 3-1, Olivier Giroud akifunguka na kupata bao la kwanza EPL. Tottenham nao hawakufanya ajizi mbele ya Aston Villa, na mabao mawili bila majibu yalitosha kupeleka kicheko White Hart Lane.
Chelsea hawajafungwa hata mechi moja, wakijikusanyia pointi 19. Wameacha pengo la pointi nne kwa timu zinazowafuata, ambazo ni zile mbili za jiji la Manchester.
Everton walionusurika kichapo na kutoka sare ya 2-2 na Wigan Jumamosi, wanashika nafasi ya nne. Hao wana pointi 14 sawa na Spurs wanaofundishwa na Andre Villas-Boas.
Kwingineko, Swansea walioanza vyema ligi na kuanza kufungwa walishindwa kuwatambia Reading, lakini walitoka nyuma na kusawazisha mabao mawili, hivyo mchezo kumalizika kwa 2-0.
Liverpool wameendeleza mwendo wa kinyonga, lakini walau safari hii hawakufungwa, wakitoka suluhu na timu ngumu ya Stoke City.
Kocha Brendan Rodgers anaona wamefanya vyema, kuweza kugangamala dhidi ya visiki hao. Bado wanahitaji kazi ya ziada, kwani wanashika nafasi ya 14 kwenye msimamo.
Southampton waliokuwa wamechapwa mechi sita na kushinda moja wamefanikiwa kutoa sare na timu isiyotabirika ya Fulham, hivyo kibindoni kuwa na pointi nne na kuwa nafasi ya 17.
Hiyo ni nafasi moja tu juu ya ule mstari wa kushuka daraja, kama timu zingekuwa zinashuka sasa hivi. Chini yake zipo Reading ambayo imekuwa kana kwamba eneo hilo ni lake tangu ligi kuanza.
Norwich ni ya pili kutoka mkiani, wakati Queen Park Rangers (QPR) ya Mark Hughes yenye wachezaji ghali aliowasajili msimu wa kiangazi wanaburuta mkia.
QPR walikubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa West Bromwich Albion Jumamosi hii, na kuzidi kumwacha tumbo joto Hughes, huku tetesi zikitoka kwamba wenye klabu wanatafuta kocha mwingine.
Reading, Norwich na QPR hazijapata kushinda mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi hii wakati Chelsea na Manchester City ndio hawajapata kuonja chungu ya kufungwa.
Timu zote zimecheza mechi saba, isipokuwa Reading na Sunderland waliocheza mechi sita kila moja, kwani mechi dhidi yao kwenye Stadium of Light iliahirishwa kutokana na uwanja kujaa maji.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal strike late to win at West Ham

Kagera Sugar shock Yanga