in , , , ,

Chelsea chali kwa Basel


*Arsenal wawanyuka Marseile kwao

Ligi ya Mabingwa wa Ulaya imeshuhudia Chelsea ya Jose Mourinho wakiangukia pua katika uwanja wa nyumbani wakati Arsenal wakishinda ugenini.

Chelsea walioanza kuongoza kwa bao la Oscar katika dakika ya 45 walipunguzwa kasi kabisa kipindi cha pili na Basel ya Uswisi kwa kupachikwa mabao mawili yaliyoonekana kumvunja moyo Mourinho.

Mohamed Salah ndiye alisawazisha bao kipindi cha pili kwa kufyatua shuti kali lililomshinda kipa Petr Cech, kabla ya Marco Streller kuweka kimiani bao la ushindi kwa kichwa safi.

Mourinho aliondoka haraka haraka uwanjani baada ya kipenga cha mwisho, huku mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich akionekana kwenye eneo lake analotazamia akiwa hana raha.

Kwa upande wa Arsenal, kiungo wao Aaron Ramsey aliendeleza umahiri wake mchezoni msimu huu kwa kufunga bao sambamba na Theo Walcott walipotoka mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya Marseile.

Huu ni ushindi wa jumla wa 10 ugenini kwa Arsenal. Ramsey alifunga akiwa umbali wa yadi 16 kutokana na pasi ya Kieran Gibbs, na hili ni bao lake la sita katika msimu huu.

Katikati ya kipindi cha pili Walcott alifunga bao zuri, huku Arsenal wakianza kuudhibiti mchezo baada ya kuwapo kashikashi kadhaa dhidi yao mwanzoni.

Penalti ya dakika ya 90 iliyofungwa na Jordan Ayew iliwafutia machozi. Arsenal wameshinda mechi ya sita mfululizo tangu walipopoteza ile ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Aston Villa.

Katika metokeo mengine, Barcelona waliwafunga Ajax 4-0, Ac Milan wakawapiga Celtic 2-0 wakati Atletico Madrid walifungwa nyumbani na Zenit St P’sbg 3-1.

Aust Vienna wasifungwa nyumbani kwao na Porto bao 1-0, Napoli wakawapiga Borussia Dortmund 2-1 huku Schalke 04 wakawakung’ura Steua Bucharest 3-0.
Jana Manchester United walipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

UWAKILISHI KWENYE MKUTANO MKUU TFF

SIMBA KUWAKABILI MBEYA CITY VPL