Menu
in , , , ,

CHAN; ni nchi gani kuweka rekodi hizi?

Tanzania Sports

Benjamini Mkapa Sradium, Dar-Es-Salaa, Tanzania

Mashindano yanayoendelea katika nchi za Afrika Mashariki za Kenya, Uganda na Tanzania yamekuja na rekodi ya aina yake katika ulimwengu wa kandanda.  Kutoka jijini Kampala kwenye dimba la Namboole hadi Moi Kasarani, kisha Benjamin Mkapa na Amaan Zanzibar vipaji vya soka vinazidi kunguruma huku nyasi zikiumia na mashabiki wakipata burudani. Kwenye mashindano ya CHAN, imebainika kuwa zipo rekodi ambazo zinavutia na kuzua mjadala ikiwa zinaweza kujirudia ama itakuchukua muda mrefu kuvunjwa.

Rekodi ya kwanza.

Kulingana na taarifa za CAF, mashindano ya AFCON yamewahi kuandaliwa na zaidi ya Taifa moja mwaka 2000. Mataifa mawili ya Ghana na Nigeria yalikuwa mwenyeji mwaka 2000 katika mashindano hayo. Wakati Nigeria na Ghana zikiwa zinaandaa mashindano hayo hapawahi kutoka nchi mbili kuwa mwenyeji. Hata hivyo kutoka AFCON hadi CHAN ambayo inahusisha wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya nchi, CAF wamdhihirisha inawezekana nchi tatu kuwa mwenyeji wa fainali hizo. Hivyo basi Tanzania , Kenya na Uganda zinabaki kuwa nchi za kwanza kuandaa CHAN na baadaye mashindano ya AFCON mwaka 2027 kwa ushirikiano.

Rekodi ya pili

Tanzania ni taifa la kwanza la Afrika mashariki kutinga hatua ya robo fainali huku likiwa limesaliwa na mechi moja mkononi. Taifa Stars iliweka rekodi baada ya kushinda michezo mitatu ya mwanzo dhidi ya Burkina Faso (2-0), Mauritani (1-0) na Madagascar (2-1). Taifa Stars pia imeweka rekodi ya kuruhusu lango lake kutikiswa mara moja pekee. Nchi ya pili inayotarajiwa kuungana na Tanzania ni Kenya ambao wanaongoza kwenye kundi lao. Lakini Uganda nayo inayo nafasi ya kutinga robo fainali ya mashindano ya CHAN. Endapo wenyeji wote watatu watatinga robo fainali maana yake wataweka rekodi ya aina yake kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Rekodi ya tatu

Kenya ndilo taifa linaloongoza kwa kulimwa kadi nyekundu kwenye mashindano ya CHAN hususani kwa upande wa wenyeji. Kenya ilipoteza wachezaji wake mara mbili kwenye mechi tofauti ambapo walilazimika kucheza pungu kwa takribani dakika 70 za mechi zao mbili baada ya nyota wao kutolewa. Kwahiyo vijana wa Benni McCarthy wanaonekana wameandaliwa kukabiliana na changamoto ya kucheza pungufu. Akizingumza na vyombo vya habari baada ya michezo yote miwili wakiwa pungufu na kushinda, kocha McCarthy alisema, “nimecheza chini ya kocha Jose Mourinho pale Porto FC, kucheza wachezaji pungufu ni kitu tulichoandaliwa vyema na Mourinho. Ni jambo gumu lakini tulikuwa tayari kiakili na kimwili. Kwahiyo vijana wangu wapo tayari, nimewaandaa kwa hili, najua nani atolewe kama sadaka ili kulinda.”

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version