in

CHAMA CHA MPIRA WA WAVU-TAVA

CHAMA CHA MPIRA WA WAVU – TAVA Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) kina kina miaka takriban 40 tangu kisajiliwe rasmi na msajili wa vyama vya michezo nchini Mei 19, 1972. Mkutano wake mkuu wa kwanza ulifanyika katika Chuo cha Walimu Kigurunyembe, Morogoro, Agosti 1973. Mwenyekiti wake wa kwanza alikuwa hayati Novati Rutageruka. TAVA ina historia ya pekee nchini, wavu ukawa mchezo wa kwanza ambao timu yake ilifanikiwa kucheza fainali za Afrika. Fainali hizo zilifanyika mjini Benghazi, Libya mnamo mwaka 1979. Kushiriki huko kunatokana na ushindi waliopupata wachezaji wetu mjini Kitwe, Zambia katika ngazi za mitoano  kanda ya sita wakati ule. Mchezo uliofuata ulikuwa mpira wa miguu, uliofanyika Lagos Nigeria mwaka 1980. Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania kilijiunga na Shirikisho la Mpira wa Wavu Duniani (FIVB) mapema mwaka 1982 kule Buenos Aires, Argentina na kuthibitishwa rasmi mwaka 1984 kule Tokyo Japan. TAVA ilishiriki mkutano wake wa kwanza wa FIVB kule Prague, iliyokuwa  Czechoslovakia mwaka 1986. Chama cha mpira wa wavu nchini ni miongoni mwa vyama vichache nchini vilivyopata kuwa maarufu sana nchini mwishoni miaka ya themanini. Umaarufu huo ulitokana na umahiri wake wa kuendesha mashindano mengi, yakiwemo ya Kombe la Bonite na KLM.  Mashindano hayo yaliweza pia kuzivutia timu za nje, hususani nchi jirani za Kenya, Uganda na Zambia. Mashindano maarufu ya Kombe la Bonite yalianza mwaka 1988 pale chuo cha Polisi, Moshi chini ya uratibu wa ndugu Marandu, yaliendelea kukua na kusimamiwa vizuri sana na ndugu Gilbert Uiso. Kombe la KLM lilianza rasmi mwaka 1984 chini ya udhamini wa Shirika la ndege la KLM la Uholanzi. Mashindano haya pia yalishika kasi sana na hata kuvutia timu za Kenya na Zambia kushiriki mashindano hayo kila mwaka. Pia TAVA iliweza kuendesha mafunzo mengi ya walimu chini ya FIVB. Kozi ya kwanza ilikuwa mwaka 1987 kule mjini Morogoro, iliyoendeshwa na mwalimu Nick Moody kutoka Scotland. TAVA imekuwa ikipokea mafunzo mbalimbali kutoka Shirikisho la Mpira wa Wavu  Duniani kila mwaka. TAVA ni miongoni mwa vyama venye wataalamu au watu waliopitia mafunzo ya mchezo huo, lakini chama hakina takwimu zozote muhimu. UONGOZI Hadi sasa chama kimeshaongozwa na marais Novati Rutageruka, Meja Jenerali Roland Makunda, Vinoo Vanza, Balozi Abdul Cisco Mtiro, Balozi Juma Volter Mwapachu, Patric Sombe, Herman Mwakasola na Augustino Agapa. Pamoja na kuwa na uongozi imara, bado mchezo huo hadi sasa haujaleta heshima yoyote kwa taifa. TAVA imeshindwa kuandaa timu ya taifa ambayo huwa kielelezo halisi katika kukua kwa mchezo kwa taifa. Inaelekea uongozi umeridhishwa na hali inayoendelea kwa kutoshirikisha vilabu katika mashindano ya Afrika. Hakuna juhudi zozote hadi sasa za kuhakikisha nchi inakuwa na timu ya taifa. Ukiwaondoa mwenyekiti, makamu na katibu msaidizi, wajumbe wote waliobakia katika uongozi wa chama hicho wameacha kufanya shughuli za chama hicho tangu wachaguliwe mwaka 2006 mkoani Tanga. Suala la ukwasi wa fedha nalo linachangia sana, kwani chama hakina chanzo chochote cha mapato. Kutokuwapo kwa katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu pia huchangia kudorora kwa mchezo huo. NINI KIFANYIKE KUOKOA MCHEZO  Pamoja na matarajio ya kuendesha uchaguzi mkuu Desemba mwaka huu, wadau wa mchezo wahahakishe wanafanya mabadiliko makubwa katika safu ya uongozi. Wadau wasioneane haya katika kuchagua viongozi wa kuendesha mpira wa wavu nchini. Wajumbe wachague watu wenye shauku ya maendeleo ya mchezo (passion of the sport), uelewa mkubwa katika masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na utafutaji fedha kuendesha mchezo, uadilifu na hata kuwa tayari kugharimia mchezo. Suala jingine ni kutumia kikamilifu fursa zinazotoka FIVB na CAVB. Wajumbe wote watakaochaguliwa wawe tayari kutumia angalau theluthi moja  ya muda wao kwa mwaka kwa  maendeleo ya mpira wa wavu. Chama kisiwe kinafanya shughuli zake kwa ubabaishaji. Kiwe na mipango inayoeleweka  na kutekelezeka. Mkazo mkubwa uwe katika shule na wakati huo huo kuwa na timu ya taifa ikishiriki mashindano ya kimataifa.  Timu za taifa ziwe katika sura zote mbili za kijinsia. Pia ziwe za watoto na watu wazima, yaani ‘Under 17’ na ‘Under 20’. Kushiriki katika mashindano mbalimbali pia kutachangia kukua kwa mchezo. TAVA ihakikishe pia mashindano yote makubwa nchini, yaani ngazi ya taifa  kama UMISETA, SHIMIWI na kadhalika yanashirikisha mpira wa wavu pia. Kuanzisha uhusiano na nchi rafiki na zenye uwezo kama Marekani, Brazil, Cuba, Uingereza na Urusi iwe moja ya mikakati kwa viongozi wapya ili waweze kuinua mchezo nchini kwa kubadilishana utaalamu kama vile mafunzo kwa timu zetu. Kurejeshwa kwa wafadhili kama vile Bonite na KLM iwe moja ya mikakati mipya katika kuinua mchezo huo. Walimu wote wanaofundisha mpira wa wavu shuleni wawe watu waliopata mafunzo yanaoeleweka. Kianzishwe kisima mahsusi cha takwimu ili kufahamu wataalamu wote wanaopata mafunzo ya TAVA. Kuwepo na mserereko wa madaraja kwa walimu, wakufunzi na waamuzi wote nchini ili kuongeza ufanisi

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Olympics 2012, London, Watanzania

UMITASHUMTA ni chemchemi ya vipaji